Binafsi Bado nina imani na Rais Samia kutuletea Tanzania iliyo bora zaidi

Binafsi Bado nina imani na Rais Samia kutuletea Tanzania iliyo bora zaidi

Binafsi Bado nina Imani na Rais Samia kutuletea Tanzania iliyo bora zaidi
Kwa imani yako hiyo Rasterman, una tofauti gani na fisi ambao hadi leo wana imani kwamba huo mkono wa binadamu lazima tu kuna siku utadondoka? Kama hiyo ndio imani ya Watanzania walio wengi basi tunayo safari ndefu ndugu zangu.
Kabisa mkuuu
Chama cha mambuzi ni lazima wafe wote kwanza. Hakuna mtu pale katika kile chama mwenye dhamira ya kuleta mageuzi yenye tija. Ni mambo ya zimamoto na kucheza na akili za wadanganyika. Imeisha hiyo
Yaani mtu alikuwa makamu wa Rais kwa miaka zaidi ya mitano, halafu bado wapo wanaotutaka tumpe muda. Kibaya zaidi anatoka chama kile kile, mawazo yale yale na akili zile zile...kwa hakika nachoka na wadanganyika!
 
Ndugu zangu pamoja na mambo mengi yaliyopita tangu Tupate uhuru ni wazi kuwa kwa sehemu fulani Rais Samia amekuwa Rais Bora miongoni mwa waliokuwa bora.

Hili linakuja kutokana na mchango wake mkubwa hasa ktk kuleta ajira, na kuongeza fedha ktk mzunguko wa miradi ya kitaifa. Kama miradi hiyo itaketa faida au la ni jambo lingine. Kama itakamilika kwa wakati au la ni mjadala mwingine.

Lakini pia nasikia kuna maridhiano yanaendelea (hatuna uhakika maana hatujatangaziwa), hili pekee kama linaendelea ni dalili njema ya kuipata Tanzania tuitakayo.

Ofcourse, mtu mwenye njaa ya hitajio la jambo fulani ataona kama muda unachelewa lakini kila lenye heri lahitaji kuvuta subira.

Naamini kinachoendelea kiko katika nia njema na muda ndio utaongea.

Hongera Rais Samia na wadau woote wanaosongesha Nchi katika mwelekeo sahihi.
Yaani jamaa wewe umeongea umbeya nilitaka nigonge like nimekunyima. Mambo ya maridhiano ni ujinga mtupu kwa sababu hawa viroboto wapinzani hawana nia njema kabisa na nchi yetu (mfano tu Zitto usipo mpatia hela ya rushwa atakusumbua kama alivyosumbua enzi za awanu ya 5, yaani mtu aliyetamani hata kumuua rais aliyepo madarakani kisa utofauti wa dini na kukataa ukoloni mambo leo, au mbowe ambaye ndani ya ngo yake hakuna demokrasia wala uhuru wa kuhoji). Ni muhimu kuua kabisa upinzani ili uzaliwe mwingine wenye maslahi na nchi.
 
Mimi namuona Raisi Samia kama Raisi mwanamageuzi, itaji la vijana ni ukuaji wa uchumi, kwa kuipa uhuru sekta binafsi kuwekeza na kufanya biashara, na ili ndilo analolipigania, kama akifanikiwa kwa haraka basi ajira na vibarua vitaongezeka, mzunguko wa hela utakuepo kwa kiasi fulani, vijana wataweza kujiajiri kwa kuzunguka uku na huko kutafuta fursa. Namuona pia kama Raisi asiependa ubabe wa kisiasa, namuombea atembee katika haki kwa vyama vya kisiasa.
Bimkubwa yuko smart sana binafsi namkubali sana atatuvusha!

Kinachotakiwa ni Bimkubwa kumaliza SGR haraka na kutandaza reli za kawaida kuunganisha nchi nzima na kukamilisha Nyerere dam na kubuni vyanzo vingine vipya vya kufua umeme basi uchumi utapaa wenyewe!

Anatakiwa kujua baadhi ya watendaji wake muhimu wanautaka urais wake na wanamkwamisha kwa makusudi na ni mafisi maji awatambue na awatoe kwenye safari yake!

Reli na umeme ni chachu ya economic growth sio siasa na hotuba! Hayo asiyape kipaumbele!

Maridhiano hayana faida wala kazi yoyote kwenye maendeleo.

English iwe medium of instruction kuanzia chekechekea ili nchi izungumze lugha ya dunia ya biashara na kuingia katika nchi zinazohusika na international transfer of capital and technology kwasasa hatumo na tutabaki nyuma na umaskini milele na kiswahili chetu mashuleni! Watoto waanze primary na miaka 5 (wa kwangu alianza na miaka 5) na wasome miaka 6 tu mnawachosha tu na masomo lukuki ya siasa za ujamaa na kujitegemea zisizo na faida kwenye maisha yao ya baadae ya kibepari (self employment)

Mikopo iendelee kwa nguvu ila bimkubwa aisimamie!

I pray for her😂

I have advanced education for economic development kwahiyo najua ninachosema!
 
Yaani jamaa wewe umeongea umbeya nilitaka nigonge like nimekunyima. Mambo ya maridhiano ni ujinga mtupu kwa sababu hawa viroboto wapinzani hawana nia njema kabisa na nchi yetu (mfano tu Zitto usipo mpatia hela ya rushwa atakusumbua kama alivyosumbua enzi za awanu ya 5, yaani mtu aliyetamani hata kumuua rais aliyepo madarakani kisa utofauti wa dini na kukataa ukoloni mambo leo, au mbowe ambaye ndani ya ngo yake hakuna demokrasia wala uhuru wa kuhoji). Ni muhimu kuua kabisa upinzani ili uzaliwe mwingine wenye maslahi na nchi.
Ni kwa vile tu kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni. Lakini kiukweli maoni yako ni tofauti na matakwa ya watanzania walio wengi
 
Ni mpiga dili tu, mpaka leo hajasema wafadhili wa Royal Tour ni watu gani, Rais anayefanya biashara Ikulu ni hatari sana
 
Watoto waanze primary na miaka 5 (wa kwangu alianza na miaka 5) na wasome miaka 6 tu mnawachosha tu na masomo lukuki ya siasa za ujamaa na kujitegemea zisizo na faida kwenye maisha yao ya baadae ya kibepari (self employment)
Hakuna faida ya mtoto mdogo kuanza shule mapema. Kikubwa ni achievement regardless ameipata na umri gani. Watoto wadogo wanakosa haki zao za kucheza, kukua vizuri na kuburudika nyumbani kwa sababu ya matakwa na Fashion za wazazi.

Kimsingi mtoto anakosa uhuru badala yake anatwishwa zigo la malengo na matarajio ya Mzazi bila kujali ina mwathiri mtoto kiasi gani.
 
Ni kwa vile tu kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni. Lakini kiukweli maoni yako ni tofauti na matakwa ya watanzania walio wengi
Hapana ungejua watanzania wengi Rais Samia hawampendi ungesaidia sana Rais Samia kujirekebisha. Tatizo lake kazalisha matatizo mengi sana ambayo kuyatatua inawezekana CCM inahitaji mtu mwingine.
 
Hapana ungejua watanzania wengi Rais Samia hawampendi ungesaidia sana Rais Samia kujirekebisha. Tatizo lake kazalisha matatizo mengi sana ambayo kuyatatua inawezekana CCM inahitaji mtu mwingine.
Can you give some examples Bwana Mudawote
 
Ndugu zangu pamoja na mambo mengi yaliyopita tangu Tupate uhuru ni wazi kuwa kwa sehemu fulani Rais Samia amekuwa Rais Bora miongoni mwa waliokuwa bora.

Hili linakuja kutokana na mchango wake mkubwa hasa ktk kuleta ajira, na kuongeza fedha ktk mzunguko wa miradi ya kitaifa. Kama miradi hiyo itaketa faida au la ni jambo lingine. Kama itakamilika kwa wakati au la ni mjadala mwingine.

Lakini pia nasikia kuna maridhiano yanaendelea (hatuna uhakika maana hatujatangaziwa), hili pekee kama linaendelea ni dalili njema ya kuipata Tanzania tuitakayo.

Ofcourse, mtu mwenye njaa ya hitajio la jambo fulani ataona kama muda unachelewa lakini kila lenye heri lahitaji kuvuta subira.

Naamini kinachoendelea kiko katika nia njema na muda ndio utaongea.

Hongera Rais Samia na wadau woote wanaosongesha Nchi katika mwelekeo sahihi.
Kama uliyo andika ni kweli basi watz nia wote na sisi tuanze kunya akili na kubakisha [emoji90][emoji90][emoji90] ili na sisi tuwe wananchi bora
 
Kwa imani yako hiyo Rasterman, una tofauti gani na fisi ambao hadi leo wana imani kwamba huo mkono wa binadamu lazima tu kuna siku utadondoka? Kama hiyo ndio imani ya Watanzania walio wengi basi tunayo safari ndefu ndugu zangu.

Yaani mtu alikuwa makamu wa Rais kwa miaka zaidi ya mitano, halafu bado wapo wanaotutaka tumpe muda. Kibaya zaidi anatoka chama kile kile, mawazo yale yale na akili zile zile...kwa hakika nachoka na wadanganyika!
Ndio maana tunasisitiza maridhiano na Katiba Mpya ili tuepukane na mawazo ya watu wale wale.
 
Back
Top Bottom