Binafsi siwezi kuishi na mtu anayeenda kwa Waganga wa kienyeji na Mchawi

Binafsi siwezi kuishi na mtu anayeenda kwa Waganga wa kienyeji na Mchawi

N
Ni ngumu kumjua mtu huyo...

Wanakuwaga wasiri sana...

NB: Uchawi na uganga ni Siri pia vyote ni sawa...
i wasiri kweli, mostly ni watu wa karibu tunao wa trust. And when unapowafahamu sasa, dissapointment strike
 
Yakikukuta yale ya noway out utaanyooka, nyie mnaojiapiza ni wepes kbs kulko wale neutral [emoji1625][emoji1625]
 
Wanaoenda Kwa waganga nikishakujua tu nakufuta kwenye list yangu, labda ufanye kimya kimya nisijue
 
Ahsante sana Mkuu kwa kunitakia kheri ya kuzaliwa.

Usiombe ukajikuta kwenye familia za washirikina, hakika utakuwa mtu asiye na bahati. Sio kwa mume au kwa mke. Yeyote kwenye familia akishakuwa na mambo ya kishirikina familia hiyo ipo kwenye shida kubwa.

Watibeli kuoa/kuolewa ni lazima sio hiyari. Labda mtu afariki akiwa mdogo lakini kama amefikisha miaka 40 lazima awe ameshaoa/ olewa
Haya tibeli
 
Ni ngumu kumjua mtu huyo...

Wanakuwaga wasiri sana...

NB: Uchawi na uganga ni Siri pia vyote ni sawa...
Hapana kuna kipindi inafika wanakuwa na confidence sana wanaamini waganga ndio kila kitu.
 
Ni vigumu sana kwa Tanzania hii kupata mwenza asiyeamini hayo mambo!

Hata humu JF tusioamini hayo mambo yawezekana hata watano hatufiki!

Nyani ngabu huko sahihi. Tunapenda tupate wenza wenye dini ila hatutaki wanaoamini uchawi.

Tunasahau dini ndio zinasema uchawi upo.

Dini na uchawi ni kama simba na yanga.

Watu wasio amini dini wapo wachache sana Tanzania. Hao ndio hawaamini uchawi
 
Ni ngumu kumjua mtu huyo...

Wanakuwaga wasiri sana...

NB: Uchawi na uganga ni Siri pia vyote ni sawa...
Atagundulika hata awe msiri namna gani. Labda aende mara chache sana na asirudie tena. Ila kama ni tabia yake aliyoizoe, basi kuna siku atajigonga na kujulikana. Ni sawa na uchepukaji. Kama ana tabia ya uchepukaji basi ni suala la muda tu atagundulika.
 
Nyani ngabu huko sahihi. Tunapenda tupate wenza wenye dini ila hatutaki wanaoamini uchawi.

Tunasahau dini ndio inaseme uchawi upo.

Dini na uchawi ni kama simba na yanga
Tena wachungaji wa siku hizi wanatumia mahubiri ya kutishia watu mambo ya uchawi ili waone kwamba bila hao wachungaji, basi hawawezi kuishi kwenye hii dunia iliyojaa uchawi. Kwa kifupi wanaoamini kwenye dini, hasa walokole wamekuwa ndiyo wenye hofu ya uchawi kuliko hata wasioamini.
 
Ni vigumu sana kwa Tanzania hii kupata mwenza asiyeamini hayo mambo!

Hata humu JF tusioamini hayo mambo yawezekana hata watano hatufiki!
We mwenyewe Kwa sababu upo Marikani huko Vilinge ni vya kutafuta.....Wasukuma mnavyopenda kuchanjana chale nyie.🤣🤣🤣
 
Na kibaya zaidi wengi wanakuwa wacha Mungu na unaweza shinda nao kanisani kabisa!
Huwezi hata kuwadhania.
Tena ukimsikia mtu anaendekeza maji ya upako siku mafuta, sijui makombe......ogopaaaa.
 
Sasa mbona ndoa nyingi zitavunjika, hivi kuna wanaume ambao sio washirikina bongo hii??
Hawa wenye chale mpk kwenye mstari wa pumbunyo!!! Labda useme mataifa ya magharibi huko
Kuna wengine walichanjwa wakati wakiwa wadogo lakini baada ya kukua na kusoma, hawana imani hizo tena.
 
Huwezi hata kuwadhania.
Tena ukimsikia mtu anaendekeza maji ya upako siku mafuta, sijui makombe......ogopaaaa.
Mamy K siku hizi washirikina wakubwa ni hawa walokole. Hili ni kundi linaloendekeza ushirikina hakuna mfano. Wachungaji na manabii wengi wanajua kuwa bila kuwajaza waumini wao hofu ya uchawi, hawatanunua mavitu yao ya upako. Kwa kifupi ni kuwa hawa manabii na wachungaji wa kilokole ni waganga wa kienyeji wanaotumia biblia badala ya vibuyu na matunguli wengine.
 
Nakuunga mkono asilimia mia,kaka epuka dada anayependa ushirikina mara ana tudawa amechanganya na mafuta kimbia,kuna siku atakulisha nyama ya bundi.
Dada chunguza vizuri familia unayotaka kuolewa usije ukaolewa kwa washirikina,wanao wanaweza kufanyiwa kitu siyo.
Namshukuru mama yangu na shangazi yangu nilipowambia nimepata mchumba waliniambia kwa msisitizo niwe makini,niijue familia nakotaka kuingia nisije olewa familia ya wachawi ama washirikina.
N.B
Happy 30 years kaoe sasa
Tulioolewa tufanyeje sasa? Mi ukweni kwangu kila mtu na mganga wake🤣🤣🤣🤣🤣
Ila mume wangu hajawahi kunionesha Kama Shabiki wa hizo mambo🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom