Bingwa wa kusilimisha Wakristo ameingia Qatar Wakristo wengi wahofiwa kusilimu. Eneo la FIFA lapambwa kwa maneno ya Mtume Muhammad S.A.W

Hajir Hakuwa Hawara , bali mke kamili wa Ibrahim ambaye Sarai limpa Ibrahim Mumewe ili awe mkewe.
Naye Ismail na Uzao wake wamebarikiwa wote.

Biblia kitabu cha Mwanzo MLANGO 16​

Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.
2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.
4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.
Unasoma biblia kinyumenyume kama quran!?
 
ROBERT HERIEL
Huo ni uongo mkubwa kwamba Qur'an ilikopi maandiko ya kiyahudi.

Kwanza yakupasa ujue kwamba Qur'an ni maneno kamili ya Allah mwenyewe (word to word) , kwa upande mwingine Zaburi ya Daudi as,na Injili ya nabii Yesu (Isa as) hayo yalikuwa ni mahubiri ya hao manabii kwa wana wa Israeli, mahubiri hayo yalikuwa ni mafundisho ya sheria mama ya Taurati ya nabii Musa as, Manabii hao Musa, Daudi, Isa (Yesu) Muhammad (saw) nk, wote hao walitumwa na (Allah, Mungu, Yehova, Mnungu) mmoja hivyo mafundisho yao msingi wake ni kutoka kwa huyo Mungu na ndio maana utakuta hakuna tofauti katika sheria za msingi katika mafundisho ya hao manabii kwani mafundisho yao yametoka kwa huyo Mungu mmoja, mfano Taurati inakataza zinaa Qur'an nayo halikadhalika inakataza nk, na hata zinaa imekatazwa kwenye vitabu vya Wahindu je hapo mtu unaweza kudai kwamba Taurati ilikopi sheria ya zinaa kutoka kwa wahindu?? Wahindu walikuwepo kabla ya Nabii Musa.

Kifupi ni kwamba manabii wote ni familia moja kwani wanetumwa na Mungu huyo mmoja na ndio maana utakuta baadhi ya mafundisho yao ya msingi yanafanana.
 
Hivi mpira sio haram kwa waislamu.....maana dini inawahitaji wavae makanzu na pia mwanaume asionekane kwenye magoti, sasa wachezaji wa mpira wanapoonyesha hadi mapaja mbona QATAR hawajaja na aina ya sare kwa wachezaji wa kiume.
 
Hili tulishahadili Mkuu.

Uislam ni Dini ya kiarabu, na kitabu Chao ni Quran, Mungu wao ni Allah, Waandishi wake ni waarabu.

Uyahudi ni Dini ya Wayahudi na waisrael.

Hawa wanavitabu vingi, kitabu chao kikuu ni Torati, ingawaje vipo vitabu vidogo kama Zaburi, waandishi wake ni mayahudi wenyewe. Mungu wao ni Yehova.

Ukristo ni Dini ya kimataifa lakini imejengwa zaidi na Wazungu, ingawaje wao wameiba maandiko ya Kiyahudi na wahusika wa kiyahudi Kama walivyofanya Waarabu. Vitabu vyao wame- combine Torati, Zaburi na Injili.
Mungu wao Yehova mwenye ushirika na Yesu Kristo.

Huo ndio muhtasari wa dini hizo tatu zenye Asili ya Abrahamu.

Ukristo na uislam hauwezi kukataa kuwa haujafanya copy na ku-paste baadhi ya visa vya Mayahudi.
Labda ushabiki uendekezwe Ila huo ndio ukweli
Katika vitabu ulivyotaja kimoja aliandika mungu akamkabidhi mtu, je mungu alikopi? Maana umezungumzia vitabu kukopiana
 
Hahaaaaa
 
Hakuna shida huko kwani wachezaji hawatavaa makanzu tu bali pia watavaa majoho kama ya wale maaskofu wa kanisani.
 
Hapana Mkuu.
Mpira sio haramu na hakuna Aya inayoelezea mambo ya michezo sio tuu kwenye Quran Bali hata kwenye Biblia
 
ROBERT HERIEL
Huo ni uongo mkubwa kwamba Qur'an ilikopi maandiko ya kiyahudi.

Kwanza yakupasa ujue kwamba Qur'an ni maneno kamili ya Allah mwenyewe (word to word) , kwa upande mwingine Zaburi ya Daudi as,na Injili ya nabii Yesu (Isa as) hayo yalikuwa ni mahubiri ya hao manabii kwa wana wa Israeli, mahubiri hayo yalikuwa ni mafundisho ya sheria mama ya Taurati ya nabii Musa as, Manabii hao Musa, Daudi, Isa (Yesu) Muhammad (saw) nk, wote hao walitumwa na (Allah, Mungu, Yehova, Mnungu) mmoja hivyo mafundisho yao msingi wake ni kutoka kwa huyo Mungu na ndio maana utakuta hakuna tofauti katika sheria za msingi katika mafundisho ya hao manabii kwani mafundisho yao yametoka kwa huyo Mungu mmoja, mfano Taurati inakataza zinaa Qur'an nayo halikadhalika inakataza nk, na hata zinaa imekatazwa kwenye vitabu vya Wahindu je hapo mtu unaweza kudai kwamba Taurati ilikopi sheria ya zinaa kutoka kwa wahindu?? Wahindu walikuwepo kabla ya Nabii Musa.

Kifupi ni kwamba manabii wote ni familia moja kwani wanetumwa na Mungu huyo mmoja na ndio maana utakuta baadhi ya mafundisho yao ya msingi yanafanana.

Yehova na Allah ni miungu wawili tofauti MKUU. Kwa nini mnapenda kuwafanya kuwa kitu kimoja ilhqli kuna ushahidi wa wazi kuwa ni miungu wawili tofauti?

Unataka tuanze kuwachambua uone utofauti wao?
 
Katika vitabu ulivyotaja kimoja aliandika mungu akamkabidhi mtu, je mungu alikopi? Maana umezungumzia vitabu kukopiana

Vitabu vinawezaje kukopiana??, how can a book copy another book??!!.

Ni hivi; maneno matakatifu yote yametoka kwa Mungu mmoja, mfano Zaburi, na Injili vyote hivo katika uasilia wake yanayo maneno matakatifu kutoka kwa Mungu waliyopewa manabii Daudi na Yesu ili kuja kuwafundisha Waisraeli kuhusu Taurati ya Nabii Musa, kimsingi ni hivi; Zaburi na Injili ni mafundisho au ufafanuzi waTaurati ya Nabii Musa kwa wana wa Israeli, Daudi, Yesu na Musa (as) hao ni manabii kutoka kwa Mungu huyohuyo mmoja, hatimaye akatumwa Nabii Muhammadi (saw) naye akashushiwa (revealed) Qur'an kwa watu wote neno kwa neno kutoka kwa Mungu huyohuyo aliyewafundisha Taurati, Zaburi na Injili manabii hao niliowataja hapo juu sasa kama kuna jambo linafanana ndani ya hivyo vitabu au maneno yao utasemaje vitabu vyao "vimekopiana" ilhali kimsingi manabii wote hao walitumwa na Mungu huyo huyo mmoja??--- Tofauti ni hii; Qur'an ni neno kwa neno ufunuo wa Mungu kwa nabii Muhammad (saw) kwa ajili ya dunia yote na Taurati ni funuo zisizokuwa neno kwa neno kwa nabii Musa (as) kwa wana wa Israeli halikadhalika Zaburi ni mafundisho ya Nabii Daudi kutilia nguvu Taurati ya Musa kwa Waisraeli ni hivyo hivyo Injili ya Yesu ni habari njema za Taurati ya Musa (as) kwa wana wa Israeli , Zaburi na Injili zilikuwa mbingu za ufundishaji wa Taurati ya Nabii Musa (as), sasa ukikuta kuna habari iliyomo ndani ya Taurati, Zaburi , Injili na Qur'an ujue kwamba habari hiyo ni ya kweli na imetoka kwa Mungu kwani manabii wote ni familia moja ya Mungu na Mungu huyo mmoja ndiye Mwalimu wao Wote na ndio maana sisi Waisilamu kuamini manabii wa Mungu ni nguzo moja ya Imani yetu.
 
Yehova na Allah ni miungu wawili tofauti MKUU. Kwa nini mnapenda kuwafanya kuwa kitu kimoja ilhqli kuna ushahidi wa wazi kuwa ni miungu wawili tofauti?

Unataka tuanze kuwachambua uone utofauti wao?

Hayo ni majina ya kitu kimoja japokuwa jinsi anavyokuwa portrayed ni tofauti kulingana na Sources husika na dhamira kusudiwa, mfano, Yesu wa Biblia ndiye yule yule Isa bin Mariam wa Qur'an, lakini kuna BAADHI ya utofauti wa jinsi anavyokuwa portrayed katika Biblia na Qur'an, au Yona wa Biblia.na Yunus wa Qur'an majina tofauti somehow lakini historia yao inafanana sana na tofauti ni ndogo kiasi kwamba huwezi kusema kwamba huyo sio mtu yule yule, ni hivyo hivyo Allah katika Qur'an ndiye huyo Yehova kwa kiebrania au Mnungu katika lugha za kibantu nk.
 
Kuna mambo ya Msingi bado unapaswa kujifunza kuhusu Miungu.

Yehova kamwe hawezi kuwa Allah.

Embu nitajie sheria za Allah alizompa Musa pale mlimani. Zile amri 10 za Mungu Kwa mujibu wa Quran, kama unazijua au kama zipo.
 
Hili tulishahadili Mkuu.

Uislam ni Dini ya kiarabu, na kitabu Chao ni Quran, Mungu wao ni Allah, Waandishi wake ni waarabu.

Uyahudi ni Dini ya Wayahudi na waisrael.

Hawa wanavitabu vingi, kitabu chao kikuu ni Torati, ingawaje vipo vitabu vidogo kama Zaburi, waandishi wake ni mayahudi wenyewe. Mungu wao ni Yehova.

Ukristo ni Dini ya kimataifa lakini imejengwa zaidi na Wazungu, ingawaje wao wameiba maandiko ya Kiyahudi na wahusika wa kiyahudi Kama walivyofanya Waarabu. Vitabu vyao wame- combine Torati, Zaburi na Injili.
Mungu wao Yehova mwenye ushirika na Yesu Kristo.

Huo ndio muhtasari wa dini hizo tatu zenye Asili ya Abrahamu.

Ukristo na uislam hauwezi kukataa kuwa haujafanya copy na ku-paste baadhi ya visa vya Mayahudi.
Labda ushabiki uendekezwe Ila huo ndio ukweli
Umesoma shule gani weye. Yaana mtu ameacknowledge sources wewe unasema ameiba. Kumbuka pia Ukristo sio separate from
 
Hakuna shida huko kwani wachezaji hawatavaa makanzu tu bali pia watavaa majoho kama ya wale maaskofu wa kanisani.

Mbona sijaona wakivaa hayo makanzu ya waarabu na mtume wenu.
 
Kuna mambo ya Msingi bado unapaswa kujifunza kuhusu Miungu.

Yehova kamwe hawezi kuwa Allah.

Embu nitajie sheria za Allah alizompa Musa pale mlimani. Zile amri 10 za Mungu Kwa mujibu wa Quran, kama unazijua au kama zipo.

To cut story short, kwa Mantiki yako hata Mungu hawezi kuwa Yehova, kama suala ni majina.

Halafu kumbuka Taurati ilikuwa ni kitabu cha sheria kwa ajili ya Bani Israel katika zama hizo, Qur'an ni kwa dunia nzima hadi Qiyama.
 
Niambie ukristo imeiba nini ktk uyahudi wakati ukristo ni combination ya two episodes. Yaani umejiibia.
 
Back
Top Bottom