Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Kwema Wakuu!

Hii inavunja moyo kwa wanaume walioamua kuoa single Mothersl.
Haiwezekani binti umelelewa tangu ukiwa mtoto, ukasomeshwa na Baba mlezi(wakambo) ukamaliza mpaka chuo cha usimamizi wa fedha.

Miaka yote huyo Babaako mzazi hakuwepo. Hakujua unakula nini wala unavaa níni. Wala hakuonyesha kujali,

Umefikisha miaka 25 ndio anajitokeza.
Siku ya harusi unampa heshima kipaombele huku ukimpuuza baba wa kambo aliyekulea.

Nimeumia sana. Hii sherehe imefanyika jana jioni.
Mzee wa Watu katia huruma kweli. Mama mtu naye ni kama hakuonyesha kujali zaidi ya kufurahia sherehe ya binti yake huku aliyemlea sura yake ikiwa haina furaha.

Hata kutambulishwa tuu.

Aiseeh!

Hata kula sikula nilirudi kula makande yangu.

Hekima ni kitu muhimu sana.

Jioni njema
Hapa unawaambia Vijana wakae Mbali na single mother sababu ni wake za watu
 
Hata mimi nimehisi hivyo kwa sababu

1. Mwanaume hawezi kujishtukiza harusini bila kupewa kadi. Hii ina maanisha alialikwa ndio maana alihudhuria kwa ujasiri wote.

2. Kama mama mzazi aliendelea kuwa kawaida, hiyo ina maana alilitarajia na pengine ana mawasiliano na mzazi mwenzie au la anajua uwepo wa mawasialiano kati ya mwanae na baba yake mzazi. Mwanamke aliyeletelelezewa mtoto kwa miaka 25 hawezi kukenua kenua meno, hicho kitendo kingemkata mood

3. Kukosekana kwa utambulisho wa baba mlezi inaonesha kutokuwepo kwa bond strong kati ya binti na baba yake mlezi maana mtu unaempenda huwezi kumsahau kwa issue kubwa kissi hicho. Hii lia inaashiria kuwepo kwa sintofahamu kubwa kwenye hiyo familia

Kukuzwa na kusomeshwa haitoshi kutoa shukran
 
Una information za ndaani za hiyo familia au unayatazama Mambo kwa nje nje tu
 
Huwezi jua huyo baba alikuwa anamtendea vitu gani huyo binti.
 
Mtu hadi anafikisha umri wa kuolewa hana akili ya kujua kipi kizuri na kipi kibaya?
Wakae Mbali na single mother wasije wakalilia CHOONI wamemwaga mamillion alafu toto linakuja kulipa credit Jamaa lilikua mbali nae miaka 25 halijui mtoto anavaa nini wala anakula nini
 
Binti amefanya jambo sahihi kabisa kwasababu Baba yake atabaki kua Baba yake na uyo mlezi atabaki kua mlezi na hakulazimishwa.
Haya mambo yapo bara la giza ila kwa mtu mwenye akili huwezi kuondoa umuhimu wa gharama na uwepo wa mtu kwenye maisha yako. Yaani uisahau Miaka zaidi ya 25 kwa sababu ya mtu ambaye pengine alikupata kama ajali kwenye starehe zake na wala hana upendo na wewe. Hiyo ni haiwezekani
 
Umelilea toto la single mother miaka 25 yote umejipinda toto linaolewa credit kwa Baba aliemtia Mimba Mama yake Wewe Baba Mlezi Fala tu kimbelembele chako cha upwiru kimekuponza ukamwaga noti
 
Umelilea toto la single mother miaka 25 yote umejipinda toto linaolewa credit kwa Baba aliemtia Mimba Mama yake Wewe Baba Mlezi Fala tu kimbelembele chako cha upwiru kimekuponza ukamwaga noti
Unajua si kila baba anamwaga noti wengine wapo tu kuonyesha kuwa huyu mwanamke kaolewa.
Yule aliyeachwa na yule msanii shilole si mkewe anasema alikuwa anamwachia pesa mezani? Sasa kwenye harusi kati yake na aliyetungisha mimba nani ana uzito?
 
Umelilea toto la single mother miaka 25 yote umejipinda toto linaolewa credit kwa Baba aliemtia Mimba Mama yake Wewe Baba Mlezi Fala tu kimbelembele chako cha upwiru kimekuponza ukamwaga noti
Single mother mmesikia 😁
 
Nadhani ume elewa ila unataka kuuliza vitu ambavyo kila mwanaume ashawahi kushauriwa asifanye hivyo.
Kuwa straight, Kila mwanaume wa wapi? Kushauriwa na nani? Kama ni humu JF ina watu laki 6 sijui, sasa haya mahubiri yamefikiaje kila mwanaume? Huyo mzee inawezekana hajui hata kama kuna wahubiri wa usioe single mother.
 
Kukuzwa na kusomeshwa haitoshi kutoa shukran
Kuondoa umuhimu wa mtu kabisa kwanza imefunua aibu za familia ukweni maana nina uhakika, mahari na kila mchakato uliendelea kwa usimamizi wa baba mlezi.

Hivyo kama siku ya harusi anatambulishwa mwingine ni lazma kengele zilie kichwani mwa upande wa mume maana inaonesha mkwe waliompata na mama yake, wana hulka zipi. Hivyo, mtoto wao ajiandae kwa lolote kwenye uzao wake
 
Back
Top Bottom