Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Kwema Wakuu!

Hii inavunja moyo kwa wanaume walioamua kuoa single Mothersl.
Haiwezekani binti umelelewa tangu ukiwa mtoto, ukasomeshwa na Baba mlezi(wakambo) ukamaliza mpaka chuo cha usimamizi wa fedha.

Miaka yote huyo Babaako mzazi hakuwepo. Hakujua unakula nini wala unavaa níni. Wala hakuonyesha kujali,

Umefikisha miaka 25 ndio anajitokeza.
Siku ya harusi unampa heshima kipaombele huku ukimpuuza baba wa kambo aliyekulea.

Nimeumia sana. Hii sherehe imefanyika jana jioni.
Mzee wa Watu katia huruma kweli. Mama mtu naye ni kama hakuonyesha kujali zaidi ya kufurahia sherehe ya binti yake huku aliyemlea sura yake ikiwa haina furaha.

Hata kutambulishwa tuu.

Aiseeh!

Hata kula sikula nilirudi kula makande yangu.

Hekima ni kitu muhimu sana.

Jioni njema
Inasikitisha sana.
 
Ndio ujue uchawi upo!
 
Haya mambo yapo bara la giza ila kwa mtu mwenye akili huwezi kuondoa umuhimu wa gharama na uwepo wa mtu kwenye maisha yako. Yaani uisahau Miaka zaidi ya 25 kwa sababu ya mtu ambaye pengine alikupata kama ajali kwenye starehe zake na wala hana upendo na wewe. Hiyo ni haiwezekani
Iwe ajari isiwe ajari Baba ni Baba tu Binti kafanya sahihi kumpa heshima Baba yake wa kumzaa hapo ata Mungu atambariki kwenye ndoa yake
 
Yule aliyeachwa na yule msanii shilole si mkewe anasema alikuwa anamwachia pesa mezani? Sasa kwenye harusi kati yake na aliyetungisha mimba nani ana uzito?
Sijaelewa kwa hio unazungumzia Mario's au?
 
Kuondoa umuhimu wa mtu kabisa kwanza imefunua aibu za familia ukweni maana nina uhakika, mahari na kila mchakato uliendelea kwa usimamizi wa baba mlezi.

Hivyo kama siku ya harusi anatambulishwa mwingine ni lazma kengele zilie kichwani mwa upande wa mume maana inaonesha mkwe waliompata na mama yake, wana hulka zipi. Hivyo, mtoto wao ajiandae kwa lolote kwenye uzao wake

Hii ndoa sijui
 
Umeongea point kubwa sana. Iwapo mchakato wa mahari ulifanywa na baba mlezi hata muoaji angeomba kumtambua ili vita ianze kabla honeymoon haijaanza.
 
Mm naamini sana kwny Karma, baba mlezi yy atulie tu atapata majibu.
 
Sijaelewa kwa hio unazungumzia Mario's au?
Wapo mkuu na huwa wanazeeka pia, wamekaa hapo wanalishwa mpaka uzee kinachowalinda ni woga wa binti kufikiri jamii itamuonaje wakiachana.
 
Nahisi bro hujui tu. Utakuta mama alikuwa anapokea kila kitu cha kumhudumia mzee ila akaamua kuendelea kumtegemea baba wa kambo. Siku hizi watoto wanaweza kuwa mtaji ujue
 
Nahisi bro hujui tu. Utakuta mama alikuwa anapokea kila kitu cha kumhudumia mzee ila akaamua kuendelea kumtegemea baba wa kambo. Siku hizi watoto wanaweza kuwa mtaji ujue
Umemaliza kila kitu yani kwakifupi uyo binti alikua ana hudumiwa na Baba yake mzazi na wanawasiliana vizuri tu bila shida ila Mama ake akawa hasemi kwa Baba mlezi
 
Ukiona ivyo ujue kabisa binti alikua ana hudumiwa na Baba yake nyuma ya camera zenu kwaio tulia
Baba Fala sio Baba labda Mama kacheza fyongo kwa hio sioni ajabu Ila Baba Mlezi ilibidi asikanyage hio harusi apambane na hali yake single mother kipengele kingine
 
Back
Top Bottom