Binti wa miaka 17 ajinyonga baada ya kuachika mara tatu kwenye ndoa

wanawake mlio kwenye ndoa tulieni kwenye ndoa zenu, hii ni hatari kubwa sana.
 
Kwamba ilishindikana kabisa kuishi pasipo kuwa na ndoa...
 
Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.

A divorced daughter is better than a dead daughter.

Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Umeongea ukweli Sana. ukute alikuwa anasimangwa kila saa.... Jamii za ki Africa zifike mahali ziache kupima thamani na utu wa mtu kwa kugezo cha ndoa..
 
Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.

A divorced daughter is better than a dead daughter.

Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Na kwa nini binti usiolewe?
 
wanawake mlio kwenye ndoa tulieni kwenye ndoa zenu, hii ni hatari kubwa sana.
Hivi umeelewa kweli?? Yeye kajinyonga kisa kuachika sio kisa kukimbia ndoa....kwamaana iyo alikuwa akiingia kwenye ndoa mambo yanakuwa ndivyo sivyo wanatengana anabaki anaumia....
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Rebecca Benjamini Mkazi wa Kata ya Izunya Wilaya ya Nyang'hwale mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa anaachwa kila anapoolewa "Ameachika mara tatu kwenye ndoa"

Mwaibambe amesema hayo alipokutana na Kamati ya Amani na Maadili ya Mkoa wa Geita, ambapo amesema chanzo cha kifo cha Rebecca ni msongo wa mawazo ambao ulikuwa ukisababishwa na yeye kuolewa na kuachika mara kwa mara.

"Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu"

Baadhi ya Viongozi wa Dini aliokutana nao leo kutoka katika Madhehebu mbalimbali ili kutokomeza matukio ya Watu kuua na kujiua, wamesema Wananchi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu.

Millard
ila mademu bwana mimi miaka hiyo nilikua nawaza kupiga na kusepa sio kuoa
 
Kwamba ilishindikana kabisa kuishi pasipo kuwa na ndoa...
Miaka 17 bado ni mtoto sana.
Umri huo ni wa kujifunza, na elimu kubwa inatokana na mtindomaisha (lifestyle) pia mazingira ambayo yamemzunguka mhusika.

Inaonesha wazi kwamba kwenye mazingira ya Rebecca, ili mwanamke aheshimike inategemea na uwezo wake wa kuhimili na kudumu ndani ya ndoa.
Kushindwa kwake kudumu kwenye ndoa, kwa umri wake aliona amepotoka sana na kwamba kuendelea kuishi kwenye jumuiya hiyo kwake ni fedheha.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Rebecca Benjamini Mkazi wa Kata ya Izunya Wilaya ya Nyang'hwale mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa anaachwa kila anapoolewa "Ameachika mara tatu kwenye ndoa"

Mwaibambe amesema hayo alipokutana na Kamati ya Amani na Maadili ya Mkoa wa Geita, ambapo amesema chanzo cha kifo cha Rebecca ni msongo wa mawazo ambao ulikuwa ukisababishwa na yeye kuolewa na kuachika mara kwa mara.

"Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu"

Baadhi ya Viongozi wa Dini aliokutana nao leo kutoka katika Madhehebu mbalimbali ili kutokomeza matukio ya Watu kuua na kujiua, wamesema Wananchi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu.

Millard
mshitakiwa namba moja hapo ni wazazi wa huyo binti mtamuozeshaje mtoto wa miaka kumi na saba hata viungo havijakomaa ataweza kuhimilki mwanaume kweli?ndiyo maanajamaa walikuwa wakiona hajiwezi wanamuacha
 
Leo tu hapa mtaani kuna brother kajinyonga kisa mapenzi. Mpaka muda huu naandika hii comment bado ananinginia juu ya mti polisi hawajafika kumtoa.
#Inasikitisha sana kujiua kisa mwanamke wakati wanawake wamejaa hadi wanamwagika🚶🚶🚶
Hata mi nashangaa. Msiwe mnawang'ang'ania wanawake mwisho wa siku mnajiua mwanamke anabaki akila maraha
 
Tuseme kila ndoa alikua nakaa mwaka mmoja mmoja itakua alianza kuolewa akiwa na miaka 14
 
Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.

A divorced daughter is better than a dead daughter.

Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Umesema jambo la msingi sana.Jamii yetu inapasa kubadilika.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom