Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Timu gani sasa inayostahili kushushwa daraja?
Tusubiri maamuzi ya CAS lakini kwa faida yako tafuta sauti ya mwenyekiti wa bodi ya Ligi kama una uwezo mzuri wa kutafsiri taarifa utapata jibu
 
Kwani si mlitoka hadharani mkanadi adui wenu namba 1 ni YANGA anafuatiwa ni SINGIDA BIG STAR?
Haya sasa UBAYA UBWELA UBAYA UBWEGE.
Hakuna lolote mwisho wa siku hii issue itaisha kizembe kabisa yanga acheni kujisumbua
 
Fuateni sheria ,kanuni na taratibu za soka sio kufuata busara
 
Hakuna kanuni inaipa mamlaka Bodi kuvunja mchezo bila sababu za msingi
Siku ile hakukuwa na sababu yoyote ya msingi kuahirisha mchezo.
1. Simba walizuiliwa kufanya Mazoezi.
Kanuni imeenda mbali, imesema ikiwa timu itazuiliwa kufanya mazoezi basi timu iliyozuia itapigwa faini mil 2.
Hapo hakuna option ya kuahirisha mechi maana kanuni imetoa adhabu ikiwa mtazuiliwa.

2. Adhabu inatolewa baada ya Mchezo, hivyo hiyo kanuni inakuonesha wazi mchezo utaendelea lkn wewe uliyemzuia mgeni kufanya mazoezi unapigwa faini ya Mil 2.

3. Unapotoa hoja TUMIA AKILI
 
Azam ilipozimiwa taa uwanja wa Kaitaba ikashindwa kufanya mazoezi, hawakususia mechi bali walicheza na kushinda mchezo ule. Vile vile SImba walipofanyiwa fujo huko Mwanza CCM Kirumba, wakati wanafanya mazoezi hawakususia mechi, bali walicheza na wakashinda. Safari hii hwa Simba baada ya kuona hawatatoboa, wakalzimisha mambo ambayo sasa yanaivunjia heshima ligi yetu.
 
Taja kanuni inayoizuia bodi kuahirisha mechi kwa mazingira yoyote inayodhani inafaa kuahirishwa.
 
Naunga mkono hoja Bodi kujiuzulu na yeyote anayeunga mkono utendaji mbovu wa Bodi hii.
 
Kusema haujafanya maamuzi wakati tayari ulishafanya maamuzi ya kuahirisha pambano ni maamuzi pia.

Hii hekima na busara ingetumika tokea awali, wasingefika hatua hii.
Heshima yako kaka .
Naiona meseji yako ila shida sina uwezo wa kujibu wala kusoma mpaka mwisho meseji yoyote huko Private meseji .
Tafadhali ikiwa hautajali naomba nitumie namba kama kichwa cha habari huko Pm na mimi nitakupigia .
Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…