Boksi la ajabu ladaiwa kutelekezwa barabarani Mwenge, Dar es salaam

Huo mkusanyiko, kama ni bomu, likilipuka litauwa wengi.
Ndiyo maana kuna wengine hapo wamesimama ki machale, kuna hisia inakuambia labda kuna kitu cha thamani ndani ya box, lakini nafsi pia inawaza huenda watu wenye nia mbaya wametegesha vilipuzi.
Rai wana kiu kuona kuna nini
 
PoliCCM wanajifanya wanajua sana. Mbona hawalifungui sasa?
 
Mwenyekiti anasema hilo boksi lilitupwa jana jioni, sasa imekuwaje liwe la maajabu leo hii
 
Kwamba ulitaka lifunguliwe hapo hapo?
Wapi uliwahi kuona jeshi linafanya kazi hvy?
Linafanya kazi hivyo kipindi linavyowakamata wanachadema. Limawakamata papo kwa papo hata bila kufanya upelelezi wowote.
 
Sijashangazwa na sanduku Wala watu wanaotizama sanduku maana najua hawana kazi za kufanya,kilichonishangaza ni huo mtaro mchafu hapo na bila shaka hata wewe umeshahisi harufu yake,ila Kuna hawa ******* wanakula mishahara ya bure na posho Kila mwezi wanajiita mabwana na mabibi afya,mpaka leo huwa nashindwa kuelewa majukumu yao ni yapi!!! Hawa watu wangekuwa wanatimiza majukumu yao japo kwa asilimia 25 tu basi miji yetu isingekuwa michafu kama tunavyoiona hivi yaani miji mingi mikubwa Tanzania ni madampo yaliyochangamka,MIJI YETU INANUKA VINYESI lakini watu waliopewa jukumu la kusimamia usafi wala hawana habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…