Tunafanya masikhara na haya mambo,kidogo kidogo tunaanza kuona mtu kajeruhiwa,tukaanza kuona mtu kauliwa,mara mmoja, Mara watatu sasa inapoelekea tutasikia bomu limeuwa mtaa mzima, haita ishia hapo tutasikia kundi moja lenye silaha limeshambulia kundi fulani.
Serkali inapaswa kwanza kubeba lawama, pili vyombo vya dola (jeshi la polisi, intelligence unit na Mahakama pia) bado watanzania hawajaona u serious katika kuchunguza, kuzuia na hata kuamua juu ya matukio yote hatarishi yaliotokea hapa nchini.
kuruhusu mambo haya kutokea Mara kawa mara na kutaka kuwafanya watanzania wayazoee, hii ni fursa tunayo wapa maadui wa taifa letu, kujipenyeza na kutekeleza matukio Kama haya na kutufanya tushikane mashati Sisi kwa sisi ambayo itapelekea uvunjifu mkubwa wa amani na nchi kutotawalika.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!