mama yangu weeeee! nchi yangu Tanzania ni nini hiki?
Sijui hata pa kuanzia!
mabomu tena? tena kwenye mikutano ya kisiasa! lol hatari sana hii ndugu zanagu watanzania wapenda nchi
maana tunapozungumzia bomu moja kwa moja ni kwamba hiyo ni zana ya kijeshi na mwananch wa kawaida hawezi kukimiliki. Mwenye kukimili ni either a terrorist group au vyombo vya usalama - in this matter polisi.
Kwa kuanzia tua kwanza kabisa hatuaminiani kiasi cha kutojua tuanzie wapi au kwa nani katika kutafuta ukweli wa mambo haya.
Tukisema vyombo vya dola vifanye uchunguzi tatizo ni kwamba haviko huru na hawawezi kufanya kazi yao kwa weledi. Katika mauaji ya nyuma yaliyotokea yenye harufu ya kisiasa vyombo vya dola vilihusika moja kwa moja tena kwa ushahidi usio na shaka (rejea Iringa kwa daudi mwangosi, arusha Jan 2011, Morogoro etc). Kwamba leo hawajahusika katika hili ni ngumu kutuaminisha just because katika mengine yaliyokwishatokea walihusika asilimia zote.
sasa swali ni kwamba kama ni chama dola kwa maana ya CCM imeamua kutumia polisi na vyombo vingine vya dola kufanya unyama huu usio na maelezo, je lengo lao la msingi ni nini? Je, tukisema kwamba labda wanalenga kujenga hofu na chuki kwa wakazi na wapenzi wa CDM wa arusha, na ikibidi kesho wasijitokeze kwa wingi ili kupiga kura kwa kuhofia usalama wao na hivyo basi CCM ikapata ushindi labda kwa kudhania kuwa wanachama na wapenzi wao watajitokeza kwa wingi zaidi na kuipa chama chao kura za kutosha? Je CCM mefanyia kazi nadharia hii? Kumbuka katika kampeni za CCM Mwigulu Nchema 'sera' kubwa ya chama achake ilikuwa kuwaambia watu ni jisni gani CDM walivyo wabaya kwa kusababisha mauaji n.k. Tena walikuwa wanatembea na kijana wa igunga na kutangaza kwenye mikutano yao kwamba amemwagiwa tindikali na CDM na hivyo basi CDM ni wabaya saaaaana, tena na kule Iringa, Moro waliu watu! Haya sasa mwisho wa siku mauaji yametokea kwenye mikutano ya CDM hapa CCM watachomokaje katika uhusika wao?
Au tuseme nchi yetu sasa imepata maadui wengineo wenye maslahi pana zaidi ya kisiasa au hata ya kisiasa tu? Mpaka sasa bomu la Olasiti uchunguzi bado hauonekani kuonesha lolote zaidi ya kumkamata kijana Ambrose ambaye binafis naamini kwamba Polisi imeamua 'kumtosa'ili waonekane angalau wanaweza kufanya 'kitu'. Nadharia hii ya kuwepo maadui wengine wa nje ya nchi au hata nadani wenye maslahi tofauti nakataa simply kwa sababu hawana sababu yeyote ya kushambulia mkutano wa kisiasa tena wa chama pinzani, simply kwa sababu gaidi akifanya ugaidi wake anatangaza kuwa amefanya hivyo ili maslahi au madai yake au status yao ijulikane. Hawawezi tu kushambulia watu kwa siri na wasitaje au kuweka agenda yao wazi. Hapo hapana. Ndio maana nasema katika hili chama dola CCM haiwezi kukwepa kunyooshewa kidole moja kwa moja.
By the way on the other hand, ni kwa vipi, ni mafunzo gani ya kipolisi ambayo yana-direct kwamba mlipuko ukitokea katikati ya kundi kubwa la watu basi polisi inabidi kurusha mabomu ya machozi ndani ya kundi hilo la watu ambao tayari kuna taharuki kubwa? je, hapo si tayari kuna risk kubwa ya watu kukanyagana na vifo zaidi kuweza kutokea? Did the police force do this out of knowledge or it was a per-determined orchestra, I mean part of the conceived plan. Hapa napo polisi wetu hawachomoki katika hili. Lawama ni nyingi na nzito kwao.
Swali ni kwamba sasa watanzania tukamlilie nani? je, kesi ya ngedere (polis) tumpelekee nyani (serikali? Maana sasa naona habari na kungóa kucha na meno bila ganzi haitoshi. Sasa ni mabomu katikati ya watu ambao kimsingi wameenda kusikiliza sera mbadala ya chama cha siasa.
CCM kwa kuona hawana chao kesho Arusha wakaamua kufanya malipizi. Haya ndio tumeyaona. kwa kifupi bado safari yetu ya demokrasia na uhuru kamili ni ndefu......
By a very grieved citizen