Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Mkuu,
Kumbuka bomu la kanisani, watu waliwaingiza Waislam lakini kumbe ukweli ni tofauti kabisa.

Sijui na kwenyewe ungeuliza kwanini mabomu hayalipuki kwenye misikiti?

Hili suala la mabomu ni janga la nchi nzima. Ni muhimu wote tushirikiane kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Lakini tukiingiza itikadi za siasa au dini, kweli Tanzania yetu itaangamia.
Mkuu waliingizwa waislam kwa sababu yule mchonganishi alitumia sumu aliyoipanda mwanzoni ndie huyu huyu anaeendelea kufanya haya matukio,swala la udini linaonekana lilianzia kwenye siasa na alietumia kuipandikiza hiyo sumu anahistoria ya kupandikiza kila kinapotokea au kunapotokea MPINZANI MKUBWA kwake na haishii kwenye dini hadi ukabila,hili la katiba mpya kuhusu serekali3 linapita chini ya utawala wa Kikwete na litaleta maafa kupitia serekali hiyohiyo ya sumu ambayo imepandwa na sasa iko neutralize,sasa limepigwa chadema,mkuu ccm hawakwepi hili hata kwa dawa
 
Nasubiri kusikia Rais Kikwete amekatisha ziara yake London na kurudi nyumbani kufariji wafiwa na majeruhi. If it will happen though.

Poleni sana Watanzania wenzangu mliokumbwa na kadhia hii
 
Nawapa pole nyingi sana wananchi wa Arusha. Ni janga ambalo litabaki ktk akili na mioyo ya watu. Ni janga ambalo linatakiwa liangaliwe kwa moyo wa kizalendo bila kuweka ndani yake itikadi za hivi vyama, ingawa sina hakika kama hilo litaepukwa.
Hivi, mkuu wa kaya ataweza kukkatisha tena ziara? Kwa kweli inabidi akatishe ziara ili hili lipatiwe nafasi yake.
 
Poleni sana ndugu zetu wa Arusha bila shaka hu mchezo ccm na makuwadi wake wanaujua mwanzo mwisho ila M/Mungu atalipa tu ila ccm wakae na kujua mwisho umefika hata wafanye nini..
 
Mwingulu kwanini unatuua wana arusha tumekukosea nini. Au kuikataa ccm ndio mmeamua kutumaliza. Naamini ipo siku nawewe yatakukuta2.
 
Huu si muda wa porojo tutajieni hao watu ili washikishwe adabu. hizi siyo kesi za kuripoti polisi.

Malota sielewh kwanini polisi walifyatu mabomu ya machozi!! Walitaka kutawanya watu au mleta uzi kakosea. Au ndo kwenye ugaidi atakaye hisiwa afe ka boston? Vituko vya hali ya juu kabisa. Poleni wafiwa na waliojeruhiwa.
 
nacho amini ccm wana husika na hili tukio...na wametumia nafasi hii kufanya haya kwa lengo kuwa kulisha wai tokea tukio kama hili tena..ushauri wangu mwingulu, shoza, mwapamba na timu yote ya ccm wakionekana wananchi wawe na maamzi magumu juu yao kwa sababu ni hatari sana juu ya maisha ya wana arusha
 
Mwingulu kwanini unatuua wana arusha tumekukosea nini. Au kuikataa ccm ndio mmeamua kutumaliza. Naamini ipo siku nawewe yatakukuta2. MUNGU YUPO
 
MACCM yanakufa vibaya

yameishiwa sera:faint::faint:
 
mkuu unachoongea ni sawa na kujaribu kina cha maji kwa miguu miwili tumeshuhudia maeneo mengi chadema wakifanya siasa za matukio ya kuuwa watu na vurugu kwa hiyo wanaweza kuhusishwa pia;lakini mantiki hapa siyo kutupiana mpira ni kutafuta ukweli.
Unasema tusitupiane LAWAMA na hapohapo unatupia lawama zako kwa chadema. eti tumeshuhudia matukio ya kuua.Acha UMALAYA wa siasa wakati watu wamekufa.
 
Kamanda mbona unawagawa wananchi unavyosema wakiristo serikalini wanawasaliti unamaanisha waamie Chadema.

Wewe ni kama ridhiwani j.k naomba ulifikishe hili kwa mshua. Kwanini hv vitu vinatokea kipindi cha mshua? Je siasa za mwigulu, shonza na mwampamba yeye kama mwenyekiti anazijua? Hebu pitia tanuru la fikra uone comments za hao watu. Mwambie mshua history itamuhukumu.
 
Hizi ishu za milipuko na mabomu TZ tunazitilia mbolea kwa nini?????
 
Wana Arusha,

Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha.

Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile.

Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi.

Roho za Marehemu zipumzike kwa Amani.
 
Ee Mwenyezi Mungu, tujalie Neema yako ukatuokoe na majanga haya.., hatuwezi kuyastahimili!!!
 
Nasubiri kusikia Rais Kikwete amekatisha ziara yake London na kurudi nyumbani kufariji wafiwa na majeruhi. If it will happen though.

Poleni sana Watanzania wenzangu mliokumbwa na kadhia hii

Kila siku watu wanakufa na kuumia kwenye ajali mbalimbali hata akiwa nje. Sasa kwani hii ni maalum sana hadi akatishe ziara yake na kuja kuwafariji wafiwa na majeruhi?
 
Back
Top Bottom