Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Mimi naona uchunguzi unatakiwa, na kukurupuka kwamba CCM ndio waliotega bomu kabla ya uchunguzi hakufai.

Je vilaza wa CCM ambao wanasema kwamba CHADEMA wamefanya njama unaona ni sawa??
 
Juliana Shonza 28 minutes ago ·

Nimesikitishwa sana na mauaji yaliyosababishwa na chadema leo katika mkutano wao. Hivi hamuwezi kufanya mikutano bila damu za watanzania kumwagika?imeshindikana kabisa? Watanzania sio wajinga hivyo kwamba msingizie ni ccm imefanya hivyo wakati ni nyie mmetegesha bomu kwenye mkutano wenu ili muonewe huruma kesho. Chadema muogopeni Mungu,nimeumia sana sana kwakweli mtaendelea kumwaga damu hivi mpaka lini?

Duuuh hv huyu dada yuko sawa kweli?
 
Mungu ibariki Tanzania...

Majeruhi wapone haraka

Marehemu, Mungu waweke mahali pema peponi, amen

Wauaji na wapanga mauaji wafahamike, wapate aibu na wapate adhabu wanayostahili
 
Huyu mtoto aliyerusha bomu amekamatwa?
 
Natoa pole zangu za dhati kwa watu wa Arusha waliopoteza ndugu zao kwa mlipuko wa bomu katika mkutano wa CHADEMA.
Damu iliyomwagika bila hatia hakika haitamwagika bure,MUNGU anasikia kilio cha watu wake,ipo siku wanaofnya mambo haya atawaweka hadharani.Nalaani vikali kitendo hiki cha kinyama.
Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu,amina!!
 
Nasikia CCM wanahangaika kutawanya kura feki muda huu,maana wanajua kuwa CDM wamechanganyikiwa na tukio hili!
 
Wewe ni kama ridhiwani j.k naomba ulifikishe hili kwa mshua. Kwanini hv vitu vinatokea kipindi cha mshua? Je siasa za mwigulu, shonza na mwampamba yeye kama mwenyekiti anazijua? Hebu pitia tanuru la fikra uone comments za hao watu. Mwambie mshua history itamuhukumu.

Mkuu Name Calling unajua kama unafanya makosa?
 
Mtu huyo anajua kuwa akiyatenda haya mtawaza kwa hasira na kuanza kupigana. Huyu mtu (au kikundi cha watu) wana akili. Kwanza wanapiga risasi na kushambulia viongozi wa dini, kisha anashambulia watu kanisani na kwenye mikutano ya hadhara. Kwenye dini anajua ushindani uliopo kati ya wakridtu na waislamu, ksenye vyama anajua ushindani uliopo kati ya CHADEMA na CCM. Ni rahisi sana kupigana. Ombi langu ni kuwa sisi wanan chi tukatae kuchonganishwa, lakini pia vyombo vyetu vya usalama wafanye kazi bila kuwa na upande.
Mkuu kwa mfumo huu tulionao ambao huhitaji kuwa chama chochote kuona mapungufu hatuwezi mkamata muhusika,serekali yetu mfano issue ya Dr.ULIMBOKA ambae mwenyewe kwa akili timamu akatoa tamko kuhusu wahusika na ushahidi akaweka wazi kupitia wakili wake mpaka leo hakuna jipya,hivi ni kipi kipya na chenye manufaa kwa nchi hii unachotegemea kutoka kwenye mfumo wa serekali hii..
 
Polisi watawezaji kufanya uchunguzi bila kupendelea upande wowote wakati mauaji yenyewe yanasimamiwa na TISS na polisi wenyewe? Watawezaji kufanya uchunguzi bila kuegemea upande wowote wkati uchunguzi wanaoufanya lengo lake ni kuwafanya watanzania wafarakane ili wasiwe na umoja wa kuiondoa CCM madarakani?

Hakuna uchunguzi wowote unaoweza kufanywa na hawa polisi wetu kwa sababu wanafanya mauaji kwa kutumwa, wanafanya uchunguzi kwa kutumwa na kwa kuelekezwa majibu yawe namna gani.

Mtu huyo anajua kuwa akiyatenda haya mtawaza kwa hasira na kuanza kupigana. Huyu mtu (au kikundi cha watu) wana akili. Kwanza wanapiga risasi na kushambulia viongozi wa dini, kisha anashambulia watu kanisani na kwenye mikutano ya hadhara. Kwenye dini anajua ushindani uliopo kati ya wakridtu na waislamu, ksenye vyama anajua ushindani uliopo kati ya CHADEMA na CCM. Ni rahisi sana kupigana. Ombi langu ni kuwa sisi wanan chi tukatae kuchonganishwa, lakini pia vyombo vyetu vya usalama wafanye kazi bila kuwa na upande.
 
Kukiwa na uchaguzi halafu kwenye kampeni ukamwona MWIGULU MCHEMBA lazima utegemee damu za watu kumwagika.
 
Wana Arusha,
Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha. Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile. Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi. Roho za Marehemu zipumzike kwa Amani.
Mheshimiwa Mungu atukuzwe.....kuna taarifa pia kuwa sasa viongozi wa CDM ndio target..haswahaswa Lema....wamefikia mahali pa kueneza umbea umbea kuwa Lema haweziuongozi lema atulie sasa ili awaongoze watu na mambo mengine.Ila mbaya zaidi...kuna taarifa za polisi kuwa siku ile pale Chuo cha Uhasibu kuna bomu la kwanza kurushwa lililengwa alipokuwa amekaa Mh Lema.Naomba CDM itoa taarifa kitaifa kuhusu style ya Lema na jinsi gani haina shida kwa wana harusha zaidi ya ukombozi.
 
Huyu mtoto aliyerusha bomu amekamatwa?

Akamatwe na policcm ambao wanashirikiana na wauaji kama Mwingulu. Wakukamatwa mpaka sasa hvi ni Mwingulu kwani ndio mpangaji wa mauaji. Hata dingi yako JK ANALIFAHAM.
 
Back
Top Bottom