Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

JK atacheza km DJ ila mwisho wake ni km wa IDD Amin...IDD amin aliwahi kuwa mwenyekiti wa OAU..alijitokeza ktk mikutano,na ususluhishi wa issue za wengine, ila alijikuta akiwa uchi pale wayahudi walipotekwa...akachukua upande wa magaidi.

Jk itabidi atupe taarifa ya wahalifu wa olasiti......kwani ahay yatamkumbusha sana.Hata polis nao watachoka haya itabidi wawe wakiwaua tuu hawa mamluki wa mauaji hapa nchini.

Kesho wanyimwe kura zote kama ujumbe wa kwanza.
 
Mkuu,
Kumbuka bomu la kanisani, watu waliwaingiza Waislam lakini kumbe ukweli ni tofauti kabisa.

Sijui na kwenyewe ungeuliza kwanini mabomu hayalipuki kwenye misikiti?

Hili suala la mabomu ni janga la nchi nzima. Ni muhimu wote tushirikiane kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Lakini tukiingiza itikadi za siasa au dini, kweli Tanzania yetu itaangamia.

Wewe baada ya kufanywa kitu mbaya sana na Mwakyembe na ukaenda kujificha uvunguni leo ndio umeona furaha kwa vifo vilivyotekea na kijifanya kuweka uharo wako hapa ehe!
 
New update kutoka kwa mwenyekiti wa chadema wilaya!
Tupo kwenye kikao,
Watu waliohusika na tukio la bomu wamefahamika na tutawaweka wazi!
 
Mkuu kama yupo anaefitinisha vyama basi anakifanya chama kimoja kionekane hakifai na kile kitakachoonekana kinafaa ndipo anakotokea yeye,hata kwa Mungu na Shetani hakuna mguu pande lazima mguu sawa sehemu mojawapo...
Mtu huyo anajua kuwa akiyatenda haya mtawaza kwa hasira na kuanza kupigana. Huyu mtu (au kikundi cha watu) wana akili. Kwanza wanapiga risasi na kushambulia viongozi wa dini, kisha anashambulia watu kanisani na kwenye mikutano ya hadhara. Kwenye dini anajua ushindani uliopo kati ya wakridtu na waislamu, ksenye vyama anajua ushindani uliopo kati ya CHADEMA na CCM. Ni rahisi sana kupigana. Ombi langu ni kuwa sisi wanan chi tukatae kuchonganishwa, lakini pia vyombo vyetu vya usalama wafanye kazi bila kuwa na upande.
 
hebu tpe taarifa kamili kamanda
Nilisikia breaking news kupitia Radio One Stereo juu ya mlipuko huko Arusha lakini cha ajabu ni kwamba kwenye taarifa ya habari ya saa mbili kamili habari hiyo haijatajwa hata kidogo. Sijui kwa nini hawajaitaja hiyo habari.
Pamoja na kutotaja lakini naona tunaenda kubaya. Hali si njema ndani ya nchi juu ya usalama wetu. Watanzania hatujazoe mambo ya mabomu sasa haya mabomu kila kukicha hayana tija na kama ni siasa basi zinatupeleka kubaya. Turudi kwenye sense zetu tusiibomoe nchi yetu.
 
sio IGP.naanza kuhisi hatari mbeleni.watz me siamini kama miaka miwili iliyobaki ya jamaa kuwa madarakani hatutaimaliza salama.kuna ugomvi ambao unaendelea hapa na walipaji wakuu ni wananchi wa kawaida.mafahari wawili wagombanapo....?hapa kuna mawili coz naona ni dhahiri jk ameshindwa kuwadhibiti wabaya wake ambao wanayumbisha nci na inavyoonekana hawako tayari kugiveup,either jamaa ajiuzulu au jeshi lichukue nchi.otherwise,trust me mabibi na mabwana,tutazipiga kabla ya next election.
kila kitu kinamwisho mkuu hawa wanaofanya hii mipango watajulikana tu mbona wa mtwara wamejulikana na wao za kwao zinahesabika.
 
Huo ni udiwani tu, bado ubunge na urais mwaka 2015, kama watanzania wanataka mabadiliko wajiandae baadhi yao kuuawa sana, ccm ni hatari kuliko ukoma!
 
"kijana mdogo kabisa ameuwawa. Ana tundu sehemu ya kifuani kushoto. Kwenye moyo. Inadhaniwa ni risasi. Hospitalini Mount Meru wanasema wamempokea akiwa amekufa tayari.

Kijana mwingine mdogo amejeruhiwa sana kichwani, kiasi kwamba ubongo unatoka yuko Mount Meru. Watu walioumia ni wengi sana sana. Mwenyekiti Mbowe amekwenda Selian Hospitali na Mount Meru Hospital na sasa pamoja na Lema wako eneo la tukio.

» Kuna maganda ya risasi za moto hapa yameokotwa pia mabomu ya machozi. Why bullets na canisters! Swali la muhimu sana, kwa nini polisi wapige risasi"?
 
Jamani baada ya bomu kulipuka jeshi la polisi badala ya kuokoa majeruhi wamekuwa bussy kuwapiga wanaokimbia. Leo nimetambua jeshi lipo kutetea serikali iliyopo madarakani. Watu wameumia, na waliowazima mnajitahidi kuwaumiza kwa kuwapiga? Real sad!
 
Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Elerai, Judith Molley naye amethibitika kufa. Yuko AICC Hospitali. Ana majeraha makubwa kichwani na mguu wa kushoto. Hapa ICC pia wamepokea vijana wengine 2 wamejeruhiwa vibaya, miguuni ma mikononi.

Mmoja ana miaka 5.5 na mwingine ana miaka 14. Wamekimbizwa KCMC.
 
Ni mambo mengi sana yanayosababisha hali hii. Hata bajet pia inwezekana ikahusishwa maana Hawa CCM wanataka isijadiliwe kisawasawa. wanatakwa watu tuwe bussy namabomu
 
Jamani baada ya bomu kulipuka jeshi la polisi badala ya kuokoa majeruhi wamekuwa bussy kuwapiga wanaokimbia. Leo nimetambua jeshi lipo kutetea serikali iliyopo madarakani. Watu wameumia, na waliowazima mnajitahidi kuwaumiza kwa kuwapiga? Real sad!:thumbup:😕😕
 
Nasema hv "MBWA AKIKARIBIA KUFA HUWA ANAREFUKA"! CCM wamerefuka kupita kiasi!! Hv wanadhan watu wamesahau ya Mwangosi? MASHAIRI YA MWIGULU yasiyokuwa na vina wala mizani sasa mwisho. Matokeo yake tumeyaona sasa!!
 
Hala hala jaman tanzania sasa imekuwa ni kama jehanam kama wananchi wamewakataa si mkae kando, ccm achen hizo ipo siku hamtatembea mtaani
 
Sifurahishwi kabisa na siasa za lema nitapingana naye daima anavitendo viki vya rafu hata hili yawezekana kunamkono wake.
Wewe ndio umesema rafu kwa sababu kitumbua kinaingia mchanga ila huo umati wa watu umeiona kazi yake,pole sana bredda
 
Hivi Tanzania Usalama wa Taifa (TISS) upo? kama upo yapo wapi majibu ya haya 1.Nani alimteka na kumtesa Dr.Ulimboka?2.Nani alimtesa na kumuumiza Kibanda? 3.Nani alimpiga risasi Padre Zanzibar? 4. Nani alimuua padre Zanzibar? 5 Nani alimuua Mwangosi? Nani alirusha bomu kanisani Arusha?6.Nani amerusha bomu leo kwenye mkutano wa chadema?nani wameficha pesa Uswiss?KAMA MPO tupeni sisi wananchi majibu angalau ya haya machache!!
 
Back
Top Bottom