Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Sorry bro kama nimekosea ila am so sad pitia tanuru la fikra! Vijana wameandika mambo ya ajabu na wamesha conclude kwamba cdm wamefanya hivyo. Kifupi chuki inazidi kuwa kubwa kwa namna hiyo. History itamuhukumu mzee wetu. Fikisha ujumbe wangu.

Mkuu mbona unielewi mimi ni Ritz, JF.
 
Last edited by a moderator:
Hawa washenzi wanaua watanzania wenzetu ili Obama asije! Lazima aje na tutamwambia mmempa mchina dhahabu na gas, imekula kwenu!
 
Polisi watawezaji kufanya uchunguzi bila kupendelea upande wowote wakati mauaji yenyewe yanasimamiwa na TISS na polisi wenyewe? Watawezaji kufanya uchunguzi bila kuegemea upande wowote wkati uchunguzi wanaoufanya lengo lake ni kuwafanya watanzania wafarakane ili wasiwe na umoja wa kuiondoa CCM madarakani?

Hakuna uchunguzi wowote unaoweza kufanywa na hawa polisi wetu kwa sababu wanafanya mauaji kwa kutumwa, wanafanya uchunguzi kwa kutumwa na kwa kuelekezwa majibu yawe namna gani.

kweli sasa nalazimika kuamini kuwa kwenye haya mambo kunachama cha siasa kinahusika kwa nini wanachadema waliopo humu kwenyee mitandao ya kijamii wanakimbilia kuilaumu na kuituhumu ccm hawa watu kunahaja ya kuwatafakari tena kwa nini wakimbilie kuwataja ccm kunashida hapa yawezekana wameratibu mpango huu.
 
Mmmmmh..Nasikia harufu ya ugaidi hapa hasa ukizingatia Chadema wanahusishwa na dini flani.So sad
 
Hawa Ni Ccm Kupitia Magaid Wao Mwigulu Na Wengine Wakishikiana Na Jeshi La Polis

Uchaguzi wowote ambao Mwigulu Nchemba amefika sijui kwanini watu wanakufa.
Igunga watu walikufa
Arumeru watu walikufa
Arusha sasa.

Daraja mbili hakuja uchaguzi ulikuwa wa amani sana.
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Elerai, Judith Molley naye amethibitika kufa. Yuko AICC Hospitali. Ana majeraha makubwa kichwani na mguu wa kushoto. Hapa ICC pia wamepokea vijana wengine 2 wamejeruhiwa vibaya, miguuni ma mikononi. Mmoja ana miaka 5.5 na mwingine ana miaka 14. Wamekimbizwa KCMC.
Mohamedi watanzania wanahitaji kuwa Vigilant sana.CCM sasa wameamua kuzidisha zaidi ya kuwekea wengine vitumbua vyao mchanga.Sasa wanafanya mauaji km "Game Hunting..hunting for Fun".
 
Leo nilikuwa kwenye mkutano wa cdm ktk viwanja vya soweto ambambapo nilishudia mkutano ukiisha kwa bomu kurushwa karibu na jukwaa la viongozi wa cdm. Mkutano ulikuwa umefurika watu wengi na kusababisha mikutano ya vyama vingine ccm na cuf kukosa watu na kujihutubia wenyewe. Zifutazo ni picha na damu iliyomwagika baada ya mlipuko.
 
Inawezekana kabisa ni CCM, lakini semeni hivyo kwa ushahidi uliotokana na uchunguzi wa uhakika.

Mkianza habari za "Kwa vile Mwigulu yuko Arusha hapo hakuna shaka kabisa hao ni CCM tu" mtaonekana mnatapatapa bila ushahidi wala uchunguzi, hata kama ni kweli Mwigulu ndo katega bomu.

Ukiritimba uliopo kwenye jeshi la polisi unafanya Private Investigation kuwa ni ndoto hapa Tanzania. Hivyo basi kesho wao wenyewe Polisisiemu watadominate uchunguzi na upelelezi wa tukio na ndio watakaotoa majibu ya nani kahusika. Ukweli ulio wazi bila shaka yoyote anayehusika na hili tukio ni Mwigulu Nchemba. Unapata doubt kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa asilimia 90 ya watanzania hatuaminiani, otherwise ungekubaliana na mimi
 
Ndugu wapenda amani, njia pekee ya kuwadisappoint hawa wanaotenda haya(iwapo ni wanasiasa) ni kulipiza kisasi kupitia sanduku la kura.Vinginevyo tutaingia kwenye machafuko ambayo wenzetu(wanaotenda haya) na familia zao wamejiandaa kwayo.
 
Nilijua tu.Sehemu yeyote ambayo Mwigulu anaweka kambi haiwezi kuisha bila vifo. ''Hongera'' Mwigulu

Hongera sana Mwigulu, hongera sana Nape. Ndiyo maana nape alikimbilia kuweka kinga kwa kuongea na vyombo vya habari na kusema kuna watu wanapanga kufanya fujo. Hongereni kwa kuua watu wasio na hatia! Lakini iko siku hizo damu mnazomwaga zitatembea juu ya vichwa vyenu!
 
Kusema ni Mshikaji Mwigulu si sawa -- ni propaganda. Nikitathmini kwa undani ni intellijensia changa za wenyewe Chadema na reference zipo kama case ya Rwaka, kifo cha yule jamaa akitokea Dodoma kwa ajali na somebody Mushi saga etc. Mimi naweza iita "cheapest intelligency ever". Motive ikiwa kuchafua nchi na ionekane kuna mabaya na uvunjifu wa amani kwa ulimwengu na kwa ujinga inatuadhiri wenyewe.

CCM haina hizi cheap manipulative strategies pengine miaka 30 iliyopita na wakati kulikuwa hamna vyama vingi, so it has never done that.

With free mind unaweza kuona hivyo. CCM ni chama cha siasa proper na CDM ni chama cha harakati. Kwa sasa huwezi kutofautisha CDM na vyama kama TUCTA etc.

Vuta kumbukumbu ni chama gani kitakatazwa kufanya maandamano na kumbuka same Arusha walishakufa, kupoteza mali, kujeruhiwa wengi kutokana na CDM na hata kumbuka mke wa Slaa. It is a a small discrepancy; kushindana na vyombo vya dola. Hili ndilo tatizo kuu.

Tufike mahali CDM kibadilike na kuwa chama cha siasa badala ya kuendesha harakati na kutegemea ruzuku huku wakipoteza maisha ya Watanzania.

CDM itasemekana ni chama chenye wafuasi wengi lakini inawafanya wafuasi kuwa desperate na kushindwa kujiuliza nini mfuasi anaweza kufanyia CDM. Matokeo yake wafuasi wanakuwa wanategemea CDM kuwafanyia miujiza. Hamna jipya baadae na time will tell baada ya kubaini CCM kuendelea kupanga na kuchagua mikakati bora ya maendeleo. Maji, Barabara, Afya, Elimu, na hatimaye masiha bora kwa kila Mtanzania.

CDM acheni HARAKATI sasa hivi ni jioni mtapoteza mkimtafuta mchawi na harakati zetu. Wachavi kwa CDM ni CDM wenyewe.

Naomba kuwasilisha - Kubwa kabisa najiunga na Watanzania wenzangu kuomboleza msiba huu mkubwa na kuwatakia kupona haraka kwa majeruhi na uchaguzi mwema hiyo kesho kwa wana Arusha.
 
Back
Top Bottom