Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Asante kwa taalifa na Picha Kiongozi kwa dalili hii ushindi tayali. CDM wakishindwa tu basi ujue (nyie em) wametumia mwanya wa maafa hayo kuvuruga uchaguzi.
 
Siasa za kijinga zinatuharibia utulivu wetu kutafua sifa za ajabu kwa kuchezea maisha ya watanzania kazi tunayo ndugu zangu.
 
Mwigulu tunafahamu unahusika kwa asilimia miamoja na ndo maana uliwatahadharisha wananchi wa arusha wasihudhurie mkutano wa cdm, umeamua kutumia mbinu km uliyotumia kuanzisha vurugu kwenye mkutano wa cdm jimboni kwako
 
why, why, why, poleni wanaarusha na watanzania. Hiki ndiki ndicho kizazi cha walalamikaji. Everything serikali!!. Wewe umefanya nini ili kulinda amani. Jf members wengi ni finger pointers. No reasoning. CCM, POLICE, SERIKALI! Haya ndio maneno ya JF, NO FUTURE FOCUS. Hata chadema ikishika nchi Police will be there. Why, why, why. Kuna wengi humu jf wemeenda chuo kikuu na pass 1E. Reasoning O. Critical thinking O. Ee MUNGU UIKOMBOE NCHI HII KWA AINA HII YA VIJANA.
 
Ccm na roho za kishetani. Mungu atawaadhibu tu hasa huyu mwigulu ambaye anajiona kuwa ataishi milele. Ccm wanaona fahari lakini mam,bo haya wanayoyafanya wajue watanzania wanaumia ni sehemu ya wanaotaka kura zao. Kama wameamua kutumia mpaka mabomu kwa uchguzi tu wa udiwani, itakuwaje uraisi? Hii inadhihirika pia kule igunga walimwagia yule kijana tindikali na kuchoma banda wakisingizia chadema. Ccm wawe na hofu ya mungu waache kufuru hizi za kuangamiza watu wasiowaunga mkono. Wametengeneza mpaka cd za ugaidi bado waliosingiziwa wanaumia moyoni wawa kina mwigulu tena wametekeleza mauaji. Is this fair? Ccm kuweni na roho za utu na ubinadamu na muone thamani ya maisha ya binandamu wengine. Udiwani tu????hii ni laana kwenu na mtakufa kwa dhuluma na mauaji haya.
 
So sad,...hizi siasa za maji taka zinaumiza watu sana.
 
Wana Arusha,

Kwa masikitiko makubwa, Mimi na mama Slaa tumepokea tukiwa Munich Ujerumani kwa masikitiko makubwa tukio la kulipuliwa Bomu katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Arusha.

Tunatoa pole kwa familia zote za waliopoteza maisha katika tukio Hilo na pia tunamwomba kwa namna ya pekee Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioumia kwa namna mmoja au nyingine na kuwapa faraja na neema kubeba maumivu waliyopata.

Chadema tunaanza na Mungu, tunaendelea na Mungu na tunamaliza na Mungu. Kama mtu asiye na dhamira na ubinadamu, awaye yeyote, na kwa sababu yeyote ile amefanya hivyo, katika hatua hii ni Imani yangu kuwa Damu ya ndugu zetu hao haitapotea bure. Kwa damu hiyo watanzania tushikamane zaidi, kuwaombea waliotutangulia mbele ya haki, lakini damu hiyo ituunganishe zaidi katika kupigania Tanzania isiyo na maonevu ya aina yeyote ile.

Hali hii sasa haivumiliki tena. Nchi inayoyoma, na hatuwezi kuendelea kutazama nchi inaporomoka. Tukiisha kutoa tahadhari miaka miwili iliyopita hawakutusikiliza. Hakuna Maisha ya Mtanzania hata mmoja kupotea katika mazingira yanayopaswa kuwa ya Amani. Uchaguzi kimsingi unapaswa kuwa tukio la Amani. Jukumu la kuhakikisha Amani ni la serikali na hakuna sababu ya kigugumizi Serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa msingi.

Roho za Marehemu zipumzike kwa Amani.
Tupo nyuma yako Kiongozi....
 
ccm wamepita na msururu wa askari maagari ya polisi, zimamoto, washawasha tangia asubuhi ya leo gari zisizopungua 25 mji mzima walikuwa wanapita sasa cha kujiuliza kupiga kura ni vita au?
 
Najua upelelezi,uchunguzi juu ya mlipuko wa bomu huko Arusha utafanyika kwa kina na kwa haraka zaidi. Lakini ombi langu kubwa kwa jeshi la polisi ni kuweka wazi juu ya uchunguzi utakaofanyika.
Imekuwa ni desturii ya jeshi la polisi kutokuja na majibu kwa wananchi juu ya matukio yanayotokea.
Ni matukio mengi ya kinyama mfano kuumizwa kwa Dr Ulimboka,Kibanda,Kifo cha mwangosi.Tume zilizoundwa kuchunguza matukio haya hazijaja na majibu yanayojibu maswali hususan ya wananchi.Hii inapelekea jamii kukosa imani na serikali pamoja na jeshi la polisi.
Hali hii inapelekea wananchi kulituhumu jeshi la polisi kuwa halifanya kazi na likifanya kazi basi ni kwa maelekezo ya wanasiasa wa chama tawala. Wananchi hawana imani na jeshi la polisi na serikali hivyo kufanya wananchi waihusishe serikali na matukio haya.
Ushauri wa bure-lakini ilivyo kawaida ya magamba na serikali yake,huku yakijiita serikali SIKIVU kumbe ni UNAFIKI yatapuuzia.
 
Tulipofikia ni pabaya sana,hivi kweli jeshi la polisi halina mafunzo ya kuwawezesha wanajeshi kutambua kuwepo kwa silaha za hatari katika maeneo wanayokuwepo.Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa jeshi letu,IGP una jipya katika hilo?
 
Sitaki nomtuhumu mtu aliehusika na bomu hilo. Ila hapa najiuliza kama ni CCM wamefanya hivyo kwanini wasingetupa alipo mboe? Naamini CCM hawawezi kifanya hivyo kwasababu direct itaonekana ni wao. Ila kuna mpango naona kama umesukwa ili kupata kura za huruma na pia watu kujenga chuki upande wa pili. Nahisi hivyo.

Ukisikiliza kauli za mwigulu akiwa arusha hasa baada ya kuona mikusanyiko ya chadema ina watu wengi zaidi ya ile ya ccm, kuna uwezekano mwigulu anafanya hivyo ili kuogopesha watu wasiende kwenye mikusanyiko ya chadema.
Kauli kama 'nzi hata wakusanyike wengi vipi hawawezi kutengeneza asali' ina maana ametambua kuwa amezidiwa na chadema kwenye kuvuta watu mikutanoni Jaribu kufuatilia hotuba za mwigulu arusha na tulia sikiliza na upambanue kwa makini utagundua kitu.Mwigulu alienda china kama nani kwa nchi hii na alienda kujifunza nini? mpaka anavaa ile nyota maana yake amehitimu kitu fulani kule china, sijui kama unafahamu siasa za china na russia zinavyoendeshwa.
 
Watakuja na propaganda CHADEMA waliwategeshea wananchi wao bomu kwenye mkutano wao...

Yote yanawezekana kwa Chamdomo kwani nao kwa siasa chafu ni vinara wa kubwa, any way tusubiri taarifa kamili tusije tukapakana matope kumbe hasidi yu wazi.
 
Inasikitisha kuona udhalimu wa namna hii....waliofanya kitendo hiki ni cowards, ningependa wapate kipimo hicho hicho cha ubaya wao hapa duniani
 
Sijui E.Lowasa nae atafanyaje km issue ni Kaskazini?Wenye chama wa pwani wanataka chama chao na nchi ya watanzania weote.
 
Nilijua tu.Sehemu yeyote ambayo Mwigulu anaweka kambi haiwezi kuisha bila vifo. ''Hongera'' Mwigulu

Hongera sana Mwigulu, hongera sana Nape. Ndiyo maana nape alikimbilia kuweka kinga kwa kuongea na vyombo vya habari na kusema kuna watu wanapanga kufanya fujo. Hongereni kwa kuua watu wasio na hatia! Lakini iko siku hizo damu mnazomwaga zitatembea juu ya vichwa vyenu!
 
hueleweki! fafanua.
Usalama wa taifa kazi kwenu kuwafichua waovu bila woga.Mimi sitaki kuamini kama ni suala la kisiasa.Huu bila shaka utakuwa ni ugaidi wenye muelekeo wa kufuata matukio kupindisha ukweli.Ni mtazamo wangu tu mkuu.
 
Back
Top Bottom