Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Mkuu mimi nahusika vipi na hili suala la kigaidi?
Una uhakika gani na unayoyasema kwa kuilaumu CCM
Sitaki kusema mengi lakini ujue kuwa kuna watu wanataka madaraka kwa gharama yoyote ile. Wanaweza kutumia mbinu zozote zile hata kuua raia wasio na hatia ili kupata attention na kuchonganisha raia na serikali iliyopo madarakani.

Lakini mengi yanawezekana, inawezekana pia watu wasiotutakia amani wakawa wanafanya hayo makusudi wakijua kuwa badala ya kutafuta mchawi sisi tutakuwa bize kunyoosheana vidole, usisahau juzi tu bomu limelipuka kanisani na leo linalipuliwa kwenye mkutano wa chadema ili kuchanganya watu wasahau ya udini wadhani ni siasa.

Lolote lawezekana. Tuwaachie polisi waendelee na uchunguzi na kama kuna anye jua lolote litakalo wasaidia polisi atoe msaada kwa kupiga simu tu sio lazima uende kituoni.

Tuweke siasa pembeni tuwaombee majeruhi wapone haraka na tuungane na familia za waliofiwa kuomboleza, hili sio suala la kulumbana kisiasa, lazima tukae tujiulize nani anatuletea hofu kwenye nchi yetu tuliyokuwa tunaishi kwa amani.

NAWAPA POLE NDUGU ZANGU WA ARUSHA, TUOMBE MUNGU ATUWEZESHE KUMPATA ADUI

Mnafiki nambari wani

keleb...
 
Kuna taarifa kuwa Mwigulu amekimbia Arusha, usiku huu, please wana Arusha, mkamateni huyu jamaa, asiotoke! Kama ni Airport tupeni taarifa akifika Dar tumdake!
 
Kuna taarifa kuwa Mwigulu amekimbia Arusha, usiku huu, please wana Arusha, mkamateni huyu jamaa, asiotoke! Kama ni Airport tupeni taarifa akifika Dar tumdake!


mwishoni CCM watamtumia halafu na KUMUUA
 
wanaohusika na hii gharika ni chadema wenyewe ili mpate huruma ya wananchi wala msitafute mchawi
 
Nadhani umenisoma....nimekuambia upo wapi ujitazame upime mchango wako wa kushangilia na kutetea uovu navyotafuta watu wako.Nasema watu wako kwa vile ktk kia watu kuna watu wengi sana unaoweza jinasibu nao km watu wa kundi lako..arusha kuna wanyalu wengi tuu wanaoipenda CDM huku wakifikiri jinsi ya kurudi na kuinua mkoa wao,kuna aksari polisi wengi tuu ambao na wewe uliwahi kuwa polisi, kuna watu wa dini yako, kuna watu wa rika yako, kuna watu wenye interest ningi km zako, na watu wote ni binadamu km wewe mabo ungeweza watetea mkia ktk kundi la simba....Leo upo too naive hujaona wapi ulikosea njia.Hujaona wapi maisha yako yangenkwenda bila "Jisalimisha kwa adui".

Ni kipindi cha kujirudi na kufikiri mara mbili maamuzi yako.....ujisamehe mwenyewe kwa kuwa mbio sana.Umlaumu sana shetani aliyekupeleka mbio..."piga magoti tumu ulipo" halafu nenda mbele ukiwa tofauti.

Tusubiri asakari wepi tena?Wewe si ulikuwa polisi nini hukijui kuhusu utamaduni wao wa siku nyingi?Chris km umekwenda ulaya bado maisha yako yanategemea bahati nasibu ni wazi huwezi tena kutoka.unahitaji Mungu sasa."UTANIKUMBUKA SIKU MOJA UTALIA SANA".Unampigania usiye mjua,vita ikikaribia kufanikiwa upande wa adui "utamsikia adui kwa kauli yake atakuja ili achukue ushindi" roho yako itakuuma sana.Ila utakuwa umechelewa sana.Na wewe utakuwa huna tena kazi zaid ya kuwa mzigo,kwani hutakuwa wa kudni lao.
Kwa hiyo ulitaka nani afanye uchunguzi?
Ukase ukijua hao wanaopanga haya mauaji iko siku mmoja wao ataimba tu. Subiri wanyimwe malipo au wazungushwe utasikia tu.

Mwisho wa mpangaji wa haya mauaji utafika tu siku moja
 
Pole kwa wahanga pole kwa wafiwa,haya mambo yanaenda taratibu itafika hatua wataanza kulipua daladala,,zilizojaa abiria
 
Mungi nilikua eneo la tukio, kitu kilicholipuka kimerushwa kutoka kwenye usawa wa zile nyumba za soweto hususani kichochoro kilichokua kinaangaliana na mgongo wa jukwaa kuu(Hii inamaanisha mtupaji alikusudia kulenga kwenye jukwaa kuu).

Nlipokua nimesimama mimi ni karibu meter 20 kutoka alipokua amesimama mrushaji bomu husika, nimeshuhudia mfuko mdogo mweusi(mifuko milaini mara nyingi hutolewa bure dukani) ukirushwa kutoka kwenye usawa wa nyumba za soweto na akilini mwangu nikajua kuna mtu kaamua kurusha mfuko wenye mabaki ya chakula or else, soon na sambamba na mfuko huo uliopdondoka mahala husika ukatokea mlipuko mkubwa na kuna baadhi ya watu wamemuona jamaa aliyerusha mfuko uwo akiwa anakimbia.
kabla sijaondoka eneo la tukio nimewaona makamanda wa chadema waliomuona muhusika wakishirikiana kuvunja geti na kujaribu kuingia kwenye nyumba ambayo mrushaji wa boom anahisiwa ameingia.
sikuweza kuendelea kuwepo eneo husika kwani polisi walianza kutupa mabomu ya machozi.
 
UCHAGUZI wa Arusha ni zaidi ya uchaguzi!MAFISADI wako tayari kutumia kila mbinu kuhakikisha CHADEMA haiongozi halmashauri ya jiji ili waendelee kuiba chini ya MAGAMBADamu ya mwanadamu huwa inajiteteaSubiri tuone wahusika watakufa vichwa vikitoa funzaR.I.P waliopoteza maisha na kwa majeruhi Mungu awape faraja
 
Tatizo we have impotent government, which does not play its role as required. We tanzanians if surely we need to live in peace and love, ccm must go!!
 
Ndugu wana jamvi,binafsi napata wakati mgumu na nashindwa kuelewa haya yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa na kusababishwa na siasa zetu za maji machafu ' naomba kuuliza hivi ni kwanini kila mikutano au maandamano ya CHADEMA huwa hayaishi kwa amani?? Hata hapa jamvini vijana wa CHADEMA wakikosa cha kujibu huishia kutukana na kutoa lugha chafu kwa CCM na wanachama wake,tupimane kwa hoja na si kwa matusi na kuchafuana' au ndo ukosefu wa maadili na busara kwa vijana wao au ndo kusema hawajafundwa' Chondechonde Watanzania tuilinde aman tuliyo nayo kwa gharama yoyote ile"
 
...nahakika Mungu atasema NENO na NENO LITATIMIA .....walaaniwe waliotenda huu unyama....
 
Inatia uchungu sana.
Ninaichukia sana CCM na serikali yake.

Please watanzania we should eradicate CCM very fast.
Tusicheke na hawa wendawazimu, watatumaliza kabla. Ni lazima tuchukue hatua sasa.

Kila mtanzania popote ulipo ni lazima kwa nafasi yako usimame kwa wazi au kwa siri kuhakikisha CCM na serikali yake vinatokomezwa kabisa hapa Tanzania.
Hatuitaki kabisa kabisa CCM na vibaraka wake wote.
 
Tukio la mwanzo walikuwa wanahisiwa waislam na Waarabu,Sasa hili nani? Nchi mzuri tunantaka kuiaribu,inaniuma sana kila nikifikiria.
 
Kuna taarifa kuwa Mwigulu amekimbia Arusha, usiku huu, please wana Arusha, mkamateni huyu jamaa, asiotoke! Kama ni Airport tupeni taarifa akifika Dar tumdake!

unafikiri kwa kutumia kiungo gani cha mwili wako? Ukiambiwa thibitisha utathibitisha? Una habari huu ni uchochezi na ni upotoshaji? Chadema mjichunge sana....mnayafanya matukio ya umwagaji damu kisha mnakimbia kuwahadaa watanzania...mmeshastukiwa
 
Back
Top Bottom