Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Nimekuwa speachless, kitendo hiki hakielezeki maana kimeshinda unyama, ni juu ya ushetani. Moyoni mwangu ninayo huzuni kubwa.

Jambo moja najua na nina hakika nalo ni kwamba kitendo hiki kimefanywa na watu waliokataliwa na wapiga kura. kimefanywa na group la the killers. Nchi hii bado kitambo kidogo itaingia kwenye record mpya kimataifa.

Maadamu vichaa ndiyo viongozi wa kile chama, tutashuhudia mengi sana kuelekea 2015. Hivi CCM haina watu wengine weledi zaidi ya hawa Wanajeshi kushika hatamu ndani ya chama?
 
Poleni sana ndugu wahanga wa hili tukio baya kabisa, kutokea katika nchi inayo semekana kuwa ya amani.
 
Mkuu,
Kumbuka bomu la kanisani, watu waliwaingiza Waislam lakini kumbe ukweli ni tofauti kabisa.

Sijui na kwenyewe ungeuliza kwanini mabomu hayalipuki kwenye misikiti?

Hili suala la mabomu ni janga la nchi nzima. Ni muhimu wote tushirikiane kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Lakini tukiingiza itikadi za siasa au dini, kweli Tanzania yetu itaangamia.

...Mkuu Mtanzania, sitaki kuamini kuwa jeshi la polisi linawafahamu waliolipuka bomu kanisani kwani kama lingewafahamu basi hili la leo lisingetokea kwani naamini matukio haya yanahusiana...

...Jeshi letu la polisi limekuwa zembe kupita kiasi, naamini huu ni wakati wa kufanyika mabadiliko makubwa kwenye jeshi letu hili, , haliwezekani matukio haya yajirudierudie na kama nchi yet hatumjui ni nani adui huyu, hili halikubaliki...
 
Ninyi mnaolaumiana kwa vyama, hivi mmeshafikiria kuwa yawezekana kabisa kuna mtu nje ya hivi vyama anayetafuta njia ya kutufitinisha Watanzania? Nafikiri huu ni muda wa kuungana na kuwa kitu kimoja kumtafuta huyo adui, awe ndani ya vyama vyetu au nje.

Think outside the box! Fikra mgando.
 
Jiulize kwanini Leo na siyo Jana? Hivi miaka yote AR ilikuwa kisiwa cha Amani Leo hii duu Lima kaharibu kila kitu. Mambo hayaendi AR, uchumi umedorora na wasipoangalia utakufa kabisa. Lima ni janga kubwa la AR
You mean Lema not Lima!
 
polisi wanatumika.

usiku huu Mwingulu Mchemba amehamishwa HOTELINI na maaskari kwa usalama wake alikuwa hapa Sterio Hotel chumba namba 214 na haijulikani amehamishiwa wapi na walizima taa zote wakampitisha Jikoni na kuelekea kusikojulikana
 
Nchemba na CCM wanahusika na tukio hili na sasa si wakati wa kuendelea kuwachekea wauaji. Serikali kama imeshindwa kulinda wananchi iondoke na kupisha wengine. Hatukio limetokea tena JK akiwa nje ya nchi nini maana yake, wale wabishi sasa wayaelewe maana ya Pengo kuhusu mlipuko wa bomu Arusha. Hii ni ajabu walinzi wa raia wanaolipwa kwa kodi za wananchi kushindwa kuwalinda watanzania halafu tuendelee kuamini kuwa tuna serikali.
 
ccm au cuf hawataki twende kwa mikutano ya cdm,ngoja nisome kutengeneza explosives plus na poison wanaofanyaga hz mambo will pay the price
hivi kamanda kouva upo humu?umeshatuma kikosi cha mashushushu waliobobea kwenda kuwakamata wauaji wa leo huko arusha?
 
• Hadi sasa hakuna kiongozi hata mmoja wa serikali amefika eneo la tukio wala hospitalini!

• Ni masaa 4 sasa baada ya tukio, tukio limetokea around 12 kasoro robo hivi, hadi sasa hakuna mahali wameonekana. Je ni guilty consciousness?

Kwanza pole sana kamanda Mtoi, MUNGU awabariki kwa kazi iliyotukuka ya kutahabarisha ktk wakati huu mgumu na muhimu wa safari ya ukombozi wa Tanzania.

Niombe tu kusema pole kwa kila aliyeadhirika na unyama huu, wafiwa na majeruhi MUNGU awape faraja na kupona haraka.

Muda huu CCM na serikali yake wanatumia mazingira waliyotengeneza ili kuchakachua uchaguzi kesho, so makamanda msilale. Ugaidi, dhuluma na unyama havina nafasi ktk Tanzania.

Nawaomba sana watu wa Arusha hiyo kesho kwa umoja na uwezo wenu mkaiwajibishe hii serikali na CCM kwa unyama huu usio na kifani dhidi ya wananchi wa Tanznia.
 
Hii ni taarifa ya msemaji wa jeshi la Polisi.

" kufuatia tukio lililotokea maeneo ya Soweto mkoani Arusha la mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ametuma timu maalum kutoka Makao Makuu ya Polisi ikiongozwa na kamishina Chagonja na kamishina Mngulu kwenda kuongeza nguvu mkoani Arusha. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa eneo la tukio mkoani Arusha.
Advera Senso- Msemaji Jeshi la Polisi".
 
Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.

Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa.

Baadhi ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa wa Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo watoto waliofika mkutanoni hapo.

Mkutano wa leo ulivunja rekodi ya mahudhurio viwanjani hapo, lakini ulikuja kuharibika baada ya kutokea mlipuko huo hotuba zikiwa zimeshamalizika na baadhi ya watu wakiwa wanatawanyika kuelekea majumbani huku zoezi la kuchangisha pesa likiendelea, kitendo kilichowazuia hata wakusanyaji michango kushindwa kumalizia zoezi hilo.

Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.

Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza kuwa, aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba zilizo jirani.


Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni Jijini Arusha jioni ya leo katika Mkutano wa Chadema kufunga kampeni zake.
Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
 
imeripotiwa hapa na mtoa baadhi ya maiti yana matundu ambayo yanasadikiwa ni risasi that means kwenye hyo saga kuna snipers walikuwemo humu ili vurugu za mabomu zikianza wawa target mbowe na lema sema walimiss target wakalenga watu wengine aisee hii ni hataree.
Please jambo hili la matundu ya risasi lichunguzwe kwa umakini sana maana si jambo dogo na linaashiria kuwa kulikuwa na mpango mbaya zaidi
 
kweli sasa nalazimika kuamini kuwa kwenye haya mambo kunachama cha siasa kinahusika kwa nini wanachadema waliopo humu kwenyee mitandao ya kijamii wanakimbilia kuilaumu na kuituhumu ccm hawa watu kunahaja ya kuwatafakari tena kwa nini wakimbilie kuwataja ccm kunashida hapa yawezekana wameratibu mpango huu.
nafikiri ukiwa na akili timamu huwezi kuhisi kuwa chadema ndio wanaoratibu haya mambo ila kama unatumikia mabwana zako ccm wanao kupa posho kwa kuwatetea hata wakifanya mambo ya kikatili na kama ni kweli cdm wanahusika naamini wahusika hawata chukua round watakamatwa coz naamini policcm watafanya juhudi kubwa sana ila kama ni kinyume chake tutaona kusua sua na porojo nyingi sana katika upelelezi wa swala hili.
 
Back
Top Bottom