Mkuu mimi nahusika vipi na hili suala la kigaidi?
Una uhakika gani na unayoyasema kwa kuilaumu CCM
Sitaki kusema mengi lakini ujue kuwa kuna watu wanataka madaraka kwa gharama yoyote ile. Wanaweza kutumia mbinu zozote zile hata kuua raia wasio na hatia ili kupata attention na kuchonganisha raia na serikali iliyopo madarakani.
Lakini mengi yanawezekana, inawezekana pia watu wasiotutakia amani wakawa wanafanya hayo makusudi wakijua kuwa badala ya kutafuta mchawi sisi tutakuwa bize kunyoosheana vidole, usisahau juzi tu bomu limelipuka kanisani na leo linalipuliwa kwenye mkutano wa chadema ili kuchanganya watu wasahau ya udini wadhani ni siasa.
Lolote lawezekana. Tuwaachie polisi waendelee na uchunguzi na kama kuna anye jua lolote litakalo wasaidia polisi atoe msaada kwa kupiga simu tu sio lazima uende kituoni.
Tuweke siasa pembeni tuwaombee majeruhi wapone haraka na tuungane na familia za waliofiwa kuomboleza, hili sio suala la kulumbana kisiasa, lazima tukae tujiulize nani anatuletea hofu kwenye nchi yetu tuliyokuwa tunaishi kwa amani.
NAWAPA POLE NDUGU ZANGU WA ARUSHA, TUOMBE MUNGU ATUWEZESHE KUMPATA ADUI