Nani wa kufanya huo "uchunguzi"? Kiranga, kwa matukio yaliyopita na yenye kufanana kimuadhui na hili la jana umewahi kusoma taarifa/ripoti za "uchungzi"? Kama ndio zinasemaje? Kama jibu ni hapana....kwa nini status quo?
Swali la nani afanye uchunguzi nimechukua muda kulijibu, kwani kwangu si swali rahisi.
Ni swali gumu, tofauti na lile la kuwepo kwa uchunguzi ama la ambalo kwangu ni rahisi sana, it is a no brainer kwamba uchunguzi uwepo.
Ama tukirudi kwenye nani afanye uchunguzi, ukweli kwamba swali hili ni gumu haubadilishi umuhimu wa kuwapo kwa uchunguzi.
Kuna mawazo mengi, na nitayataja mawili makuu hapa pamoja na mapungufu yake kwa kutumia milinganyo ya Kiranga inayotafuta uwiano wenye kina na kukomaa kwa kufikiri.
Kuna watakaosema tutumie vyombo vya nje nyenye uzoefu zaidi na ambavyo vinaweza kuwa na kutofungamana na upande wowote kuzuri zaidi. Hapa kuna maswali kibao yanaibuka kuhusu sovereignty, kuhusu security system penetration, kuhusu kama kweli vyombo vya nje vinaweza kuwa na uzoefu zaidi katika masuala yanayofanyika Tanzania - hata kama vikiwa na technological/ forensic superiority-, kuhusu ukweli kwamba hata hivyo vyombo vya nje vikimaliza kazi vinaweza kutakiwa kukabidhi taarifa kwa serikali yetu hii hii ambayo itakuwa na maamuzi ya kuikalia au kuitangaza taarifa. Tukirejea uchunguzi wa kifo cha Dr. Robert Ouko wa Kenya tunaweza kuona mazuri na mabaya mengi ya kuvishirikisha vyombo vya nje.
Kuna wanaoweza kusema kwamba tutumie vyombo vyetu vya usalama, pamoja na mapungufu yavyo yote, bado ni vyombo vyetu. Na kinachotakiwa kufanyika ni kuwa na ufuatiliaji wa uhakika na kujenga utamaduni wa "ownership". Tutumie polisi na idara za upelelezi vizuri, tufuatilie kuhakikisha idara hizi na vyombo hivi vya dola havitumiki kwa maslahi ya wachache kwa misingi ya vyama/ kisiasa negatively. Kwamba huu ni wakati muafaka wa kuviasa vyombo hivi kwamba wananchi wanafuatilia na kama vikitaka kutuchezea shere vitakuwa vinapanda mbegu za vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Then of course, the question being so complex, so new, so fluid, so formulating, and my knowledge regarding the ever changing specific being so limited and stagnantly left behind, there is always a possibility not apparent to me at this point that could be employed to enhance investigations.
If I do not know the specific answers as to who shall conduct the investigations, I know one thing.
There should be a thorough, transparent, credible investigation before any conclusions are drawn.
This is elementary, as Holmes would say.