Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Ndugu yangu mmoja alikua km wewe na akili za kindezi bi mkubwa akamuita chini akamshauri usiingie kwenye mikopo ndugu alivyo mjinga kasikiliza ushauri wa mkewe kadharau ushauri wa bi mkubwa kaenda bank katia saini M200 miezi 6 imekata yote nyumba kamaliza gari alikua anatembelea Alphard white ndio ilikua gari yake pendwa alienda kula mzinga k/koo gari ikafumuka mbele aliingia chini ya lori, bank kila mwisho wa mwezi wanakomba ½ na ¼ ya mshahara wake mpaka kichwa kikaanza kumuwaka moto watoto anasomeshwa shule za gharama mpaka akaanza kuwarudisha kayumba mmoja mmoja, usiombee yakukute
Huyu ndugu yenu hana akili ata mie namzidi🤣🤣🤣🤣🤣
 
People should just mind the business that pays them!

Kwa nini mnapenda kujishughulisha na mambo ya watu wasiowahusu?
Chuki na roho mbaya vinaeatesa wanataka kuona mafanikio ya wenzao si chochote wakati suala la mtu kujitegemea tu yani kuwa na gheto na ukamudu gharama za chakula na mavazi nk ni mafanikio makubwa sana kwa binadamu
 
Mafanikio ni swala pana. So inategemea hali uliokua nayo awali na ulipo kwa wakati husika.
Kwa mfano unaweza kuta mtu kwao kakulia kwenye nyumba ya udongo na shule amesomea 2km umbali kutoka nyumbani na anaenda kwa miguu kila siku, sasa mtu kama huyo akijenga nyumba ya milion 30 na kagar ni mafaniko makubwa sana kwake ila kwa mtoto wa mengi au bakhresa kwao mafanikio ni vitu tofauti na hivyo.
Ni kweli mafanikio ni relative term. Kila mtu na anavyoona yeye. Mwingine kuolewa au kuoa mtu sahihi ni amemaliza Yani ndo mafanikio yake
 
Mkuu huyu ni tajiri nyumba ya 30m na gari ya 20m huyu ni class apart wa Tanzania wanao weza kumiliki mali ya 50m hawafiki 10% plz mkuu heshimu juhudi za watu, sio kila mtu anaweza kumiliki gari na nyumba.
Mtoa mada utakuta bado anaishi kwao
 
Mafanikio ni swala pana. So inategemea hali uliokua nayo awali na ulipo kwa wakati husika.
Kwa mfano unaweza kuta mtu kwao kakulia kwenye nyumba ya udongo na shule amesomea 2km umbali kutoka nyumbani na anaenda kwa miguu kila siku, sasa mtu kama huyo akijenga nyumba ya milion 30 na kagar ni mafaniko makubwa sana kwake ila kwa mtoto wa mengi au bakhresa kwao mafanikio ni vitu tofauti na hivyo.
Sahihi
 
Mbona unatoa povu? Kwa hali ya kibongo kumiliki gari na nyumba si jambo rahis. Japokuwa hao sitowaita matajiri bado ni uchumi wa kati. Acha wajipokengeze kufikia hapo si kazi rahisi
Kama unamiliki gari na kanyumba halafu bado mafuta ya gari unabangaiza bado sio uchumi wa kati.
 
Back
Top Bottom