Bongo fleva top 5 yangu ya muda wote

Bongo fleva top 5 yangu ya muda wote

Hivi Bongo "flava" ni mziki gani hasa? maana naona kila kukicha unabadilika kukopi miziki ya nje Amapiano, Azonto nk.
Ni upi hasa Bongo Fleva?
 
Hunifahamu sikufahamu dada iweje Leo unipakazie.....
By Dully Sykes. Najua wengi wenu bado mlikuwa mnainjoi matiti ya mama zenu, nyambaf...
 
Hakuna hata moja ya Roma Mkatoliki!
 
Kuhusu wakali kwanza Kuna Ngoma ya makamua na enika Rudi nyumbani, Joseline na ticha, niite bas, umewezaje ukija kwa Q jay Sifai.

Hii inatoa tafsiri kwamba wakali kwanza kweli walikuwa wakali
Hao watu walikua hatari sana mkuu sema biashara ya muziki wa bongo inaua vipaji vingi sana... kundi lilivunjika wakati bado tunalihitaji yani... hizo ngoma ulizotaja zote zipo kwenye playlist yangu ya zilipendwa
 
Kuna wasanii waliwahi kuibuka wakatoa hit moja halafu wakaingia mitini... mtu kama pico (piko) na kikongwe.

Kuna ile ngoma Kidato kimoja (ilitumika sana hii kuwalaghai warembo)

MeziB nae alikuja kuja akapotea ila ako na hit yake moja ilipigwa sana club enzi hizo yupo na ray c (kama vipi nataka kwenda nawe) mnaokumbuka jina la wimbo exactly weka hapo.

Kuna tshirt na jeans nayo ilisumbua sana hii ngoma coz iliwafanya vijana wengi wakumbuke kuvaa hivo 😆😆😆.

Pia kuna jamaa aliitwa roho saba aliachia hit kadhaa kama pazia jeusi, waite polisi na kadhalika (moja kati ya rapa wenye floo za hatari sana, ila niliskia skia aliacha muziki ili aitumikie nchi)

Yupo jamaa mwingine nae wakuitwa Mr Paul alisumbua sana na hit yake ya zuwena (ngoma ilipigwa sana hii pale channel five).

Jafarai na ngoma yake ya unaoenda nini nayo ilisumbua sumbua sana (wimbo flani ambao ulikua mbele ya muda coz mada zilizopo mule ndio ambazo zinaimbwa na waimbaji wa sasa)

Samiri nae alisumbua na kinyuri nyuri yake na heat kadhaa Pia alikua nazo ila ghafla akapotea.

Kule mwanza kulikua na jamaa aliitwa siza madini nae alikuja na ngoma yake ya kifungo huru (moja kati ya vocalist arts tuliobarikiwa Tz ila sijui alipotelea wapi huyu kijana, Kidbwai aliwasaidia sana vijana wa mwanza)

Anyway, list ni ndefu ila hii itoshe kusema kwamba muziki uliibwa.
 
Stara Thomas- Mimi na wewe

Maunda -Nataka niwe wako

Ray C-Unanifuatia nini(una vijembe
makini sana kwa mtu wa kuitwa
ex)
Ray C wa hiyo umenikataa nila sababu nilikuja kumsikia tena kwenye Mama ntilie aliyoimba na wakina AT ni RayC fulani anayeshushua 😂😂
 
List nzuri kama ulivyosema ya kukumbuka moments ila kwa mimi nyimbo zote zitaimbwa ila mtazamo itabaki kuwa nyimbo bora ya bongo fleva upande wa hip hop.

Na wakali kwanza natamani utabaki kuwa wimbo bora wa RnB wa muda wote.

Chochote popote huu kwangu utabaki kuwa wimbo bora wa hip hop unaozubgumzia mapenzi (Joh makini aliuwa sana humo ndani).

Collaboration yangu bora ya bongo fleva naitupa kwenye dhahabu, ebhana e Dully, Blue na Joselin waliua sana mule ndani.

Prof na series yake ya ndio mzee ni moja ya ngoma zenye ubunifu na idea ya kipekee ambayo ilifanywa kuwa nyepesi na ya kuvutia sana na mwanalizombe.
Kamanda - Daz Nundaz ndio nyimbo ya Bongo Fleva ya wakati wote. Akifa mtu tu hio nyimbo ni relevant
 
Kamanda - Daz Nundaz ndio nyimbo ya Bongo Fleva ya wakati wote. Akifa mtu tu hio nyimbo ni relevant
Huu wimbo uliandikwa sana... nilikua nauogopa sana kuuskiliza enzi zile nakua kua 😅😅

Ila kati ya nyimbo zenye intro bora kamanda nayo imo... kaaaamaaaandaaaa eeeee yoooo 😅😅😅
 
T.i.d na Jidee Understanding
Mwana FA ft Jidee- Hawajui
Chid benz ft mzee yusuph
Joh makin ft Jidee -Kilimanjaro
 
Ismail -nachotaka.

Chid Benzi ft mzee Yusuphu -mashallah.

Yalaiti - mwanafalsafa ft Linah.

My top 3 bongo fleva songs
 
Baadhi ya nyimbo zinakuwa zina capture moments...yaani nyakati Fulani hivi ...na mood ya Taifa au ya walio Wengi wakati huo...

1. Nipe Tano - Daz nundaz..
Huu Wimbo unawakilisha nyakati ..kama birth hivi ...ndo kwanza Taifa linapata TV special Kwa bongo flava na vijana ...Nani angejua channel 5 ingekuwa chanzo cha TV zote zilizozagaa now?golden era..

2. Dushelele - Ally Kiba
Wengine wanamuona Ally Kiba kama the best ever bongo fleva singer ...huu Wimbo Una kitu unique sana...mashairi ambayo hayana lugha za vijana au matusi ..umeandikwa vizuri umeimbwa vizuri...kinacho ufanya uwe special ni kudhani kuwa kungekuwa na nyimbo kama hii nyingi ..but cha kushangaza ni kama imeshindikana kabisa kupata uandishi kama huu na Wimbo kama huu...umebaki Tu wa aina yake..

3. Mfalme -Mwana Fa
Wimbo unahusu Mungu kwenye bongo fleva na ndani ambae baadae anakuja kuwa waziri wa sanaa... something unique...

4. Muziki-Darasa..
Wakati ilionekana kama ngumu kutamba kwenye mziki bila kupitia wasafi au kupata sapoti ya Diamond...jamaa aliibuka na kutawala vibaya mno na Wimbo ambao unaitwa "mziki"...hakuna aliedhania wala kutegemea....

5.Single Again - Sikuwahi kupenda nyimbo yeyote ya Harmonise wala kumtegemea atakuja kutoa Wimbo utatamba Hadi nje ya Tz ..ila huu Wimbo alionesha ana kipaji.. na inawezekana kufika juu Sana ukiamua...

Wengine mnaweza taja za kwenu na sababu
Namba 3 ilifaa ikae kwenye namba zote katika hiyo list hapo, ingekuwa ni mimi.

Ova
 
Zali la mentali prof j ft juma nature

Mtazamo Afande ft Solo thang, Prof j

Tutakukumbuka daima Gk ft TID, hili song kila msiba maarufu lazima lipigwe

Hakunaga Suma lee

Nakupenda mpenzi Dudu baya
Zali la mentali kiboko bwana.
Kuna ule wimbo wa magonja na ukimwi sijui unaitwaje ukimwi ndio anafunga goli.
Amekoma amekomaa alidhani poa kumbe sio poa aahhh side mnyamwezi
 
Back
Top Bottom