Bongo Zozo ana hoja kuhusu uraia pacha kwa Watanzania

hili watu hawalioni........
na tunaweza kuwa na mawaziri nusu watanzania, nusu wamarekani...... sijui wata-serve interest za nani
Ujinga gani huu jamani kwani huwezi kuweka Sheria ya kuwazuia kugombea huo urais wenu! kwingine kukaachwa huru, waziri mkuu wa sasa wa uingereza Ana asili ya India,makamu wa rais wa marekani je?. Ni hasara Sana kuwa masikini Kisha ukawa masikini wa akili na mchoyo.
 
Hadi sasa bila hata kuwa na uraia pacha bado kuna mawaziri wana-serve interest zao na za wawekezaji!
Interest zao na ndugu zao hakuna mwekezaji mjinga atawekeza kwenye nchi yenye rushwa kwa sababu anakuwa anapoteza mali zake kwa hiyo usifikiri mwekezaji inabidi awe Mtanzania ndio awekeze hilo nalo ni maajabu ya Tanzania
 
Interest zao na ndugu zao hakuna mwekezaji mjinga atawekeza kwenye nchi yenye rushwa kwa sababu anakuwa anapoteza mali zake kwa hiyo usifikiri mwekezaji inabidi awe Mtanzania ndio awekeze hilo nalo ni maajabu ya Tanzania
Bila shaka hilo ni ajabu lako!
 
Waulize Wana siasa watakuambia madhara ya uraia pacha Ila ni Siri yao
Hao wanasiasa wanaogopa kuruhusu urai pacha kwani itabidi warudishe mali za watu waliowapora wakisingizia sio Watanzania hiyo ndio Siri kali kesi zitakuwa nyingi mno na wataumbuka
 
Kwani bongo zozo kasema anautaka? Anasemea wapwa zetu! Yeye hana shida nao.
 
Umakin
U makini gani unatakiwa hapa? Bongo zozo anauliza, mtoto mtanzania wa kuzaliwa, au mtanzania wa kuzaliwa, kwa nini umnyang'anye uraia wake wa asili kwa kuwa kapata fursa huko Ulaya? Anachokisema, utanzania wake unabaki palepale. Anasema, mtoto wake ni mtanzania, anapenda kuwa mtanzania, lakini anachukua uraia wa Uingereza ili atumie fursa zilizopo huko kama matibabu, shule nk nk nk. kwa hiyo anachukua passport ys Uingereza ili kuchukua hizo fursa, lakini roho na moyo wake bado ni mtanzania. Kwa hiyo serikali inachotakiwa kufanya ni kutoa kile kipengele cha mtanzania akichukua uraia wa nchi nyingine kwa ajili ya fursa, asiukane utanzania wake. Basi. Mgogoro unakuwa umeisha.
Haya mawazo ya kijamaa jamaa, ushushu shushu na wivu yameshapitwa na wakati. Unadhani wanaochukua uraiaa huko ulaya, wanapenda sana huko? NO ni fursa tu. wangekuwa wanapenda kwanini hizi kelele haziishi.
 
Waulize Wana siasa watakuambia madhara ya uraia pacha Ila ni Siri yao
Hivi ina maana kenya, ghana, bostwana, uk na spain hawaoni hayo madhara ya uraia pacha? Mpaka wakaruhusu?
 
Hivi ina maana kenya, ghana, bostwana, uk na spain hawaoni hayo madhara ya uraia pacha? Mpaka wakaruhusu?
Hawana sababu za maana ndio maana huwa wanakataa bila kutoa sababu
 
Awamu hii ni kokoro linabeba kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…