Bora Mbeya ikawa makao makuu ya nchi kuliko Dodoma

Eti ushamba wako wa kutokuzunguka [emoji1787]
 
Mbeya pamezidi uhovyo. Jiji lina zaidi ya miaka 30 lakini utadhani limetangazwa kuwa jini jana!!!

Jiji ambalo kila mtu ni nabii hadi wamama duh!!!
Nani kakwambia jiji la mbeya Lina zaidi ya 30 yrs?mwanza lenyewe halina umri huo
 
Vingine ni kweli na vingine umewaonea Mbeya. Baridi si rafiki wa Swimming pools na nightlife. Uingie kwenye swimming pools na lile baridi, au ulitaka yawe heated, kwa umeme huu?

Mbeya hakuna haja ya masupermarket, kuna masoko kila kona. Masafi na yana bidhaa fresh zinazouzwa. Na masoko ni mazuri sana kwa uchumi kuliko supermarket moja ya kampuni kubwa.

Na miji mingi utakuta maofisi na masoko yamerundikana sehemu moja. Mbeya pametengana, na ni jambo zuri. Sehemu za maofisi hazihitaji vurugu.

Kwenye suala la hotel bado sana. Nafikiri sababu hakuna watalii wala wageni wa kimataifa. Gym hakuna uhitaji, vilima vile ni gym tosha.
 

Mbeya mzunguko wa fedha hakuna? Are you serious or kidding? Bila ya Serikali Dodoma ni zero tena zero kabisa. Mbeya inajiendesha yenyewe
 

Tuchukulie uwekezaji uliofanyika na serikali pale Dodoma( maana Dodoma bila serikali, hata Mpanda patakua juu), kisha uwekezaji ule ungepelekwa Tanga au Mtwara na Serikali ikahamia huko, kwenye miji hiyo yenye bahari na manzari nzuri kabisa za fukwe, hali ingekuaje? Ifike mahali tukubali tu kuwa miji mingi kukua kwake pia Serikali ikiamua ku- boost inasaidia sana.
 
Athari za ukomunisti ndio zimetufisha hapo
 
mbeya ni mji wa hovyo sana huwez gundua mwanamke yupi mwanaume yupi wote wanafanana wanawake wamekomaa kama onyango
 
Naunga mkono hoja,..Ila Bora makao makuu yawe chuga tu..au kilimanjaro
 
Umefika mara ya mwisho lini Mbeya... Njoo new Mbeya pazuri... Ujionee.. uzuri wake kama ulifika mwaka jana kurudi nyuma usicoment hapa

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
do! hili umenikumbusha niliingia mgahawa mmoja wa kawaida kunywa chai sukari ikawa imeisha muhudumu akang'ata kwa meno kufungua pakiti ya sukari wakati nashaa mwingine akawa anatumia tena meno kufungua pakiti ya majani ya chai
Ukienda migahawa ya kawaida ya vichochoroni lazima upate huduma za vichochoroni... Nchi nzima iko hivyo

Hivi hukuona migahawa, restaurant au hotel Nzuri hadi uende vichochoroni ndio uje kuongelea Mbeya

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…