Bora Mbeya ikawa makao makuu ya nchi kuliko Dodoma

Bora Mbeya ikawa makao makuu ya nchi kuliko Dodoma

Utaendelea kuishi kwenye zama za Giza Hadi lini?

Miaka fulani ndio leo? Eti garage Soweto,kuna bonge la gereji ya wachina kubwa kabisa na la kisasa pale Uyole jirani na St.Aggrey..


Vi min market viko vingi sana ni ushamba wako tuu wa kutozunguka.

Hizo 4 star hotels ziko nyingi tuu mojawapo inaitwa Highlands Hotel ,

Mbeya ni kama Dar ina CBD 2 yaani Uhindini/City center na Mwanjelwa sasa sijui wewe hater unataka mjini kuweje..

Acha ushamba Mzee,Mbeya ya Leo sio ya juzi ulipokuwepo wewe.
Eti ushamba wako wa kutokuzunguka [emoji1787]
 
Mbeya pamezidi uhovyo. Jiji lina zaidi ya miaka 30 lakini utadhani limetangazwa kuwa jini jana!!!

Jiji ambalo kila mtu ni nabii hadi wamama duh!!!
Nani kakwambia jiji la mbeya Lina zaidi ya 30 yrs?mwanza lenyewe halina umri huo
 
Vitu vingi sana, kuna mwaka nilitafuta a colored printer nilikosa karibu stationery zote.

For 2yrs straight kuna mtu namjua anatafuta parts za gari lake Land rover Mby hamna hadi kaagiza mikoani japo hazikufit ila Mby hata za kujaribu tu alikosa. Infact Mbeya hakuna gereji hata moja I mean hata moja ya maana zote za kuunga unga tu kuanzia kwa Lena kule Mbalizi hadi Soweto.

Ukiacha swimming pool ya pale JM na Utengule kuna swimming pool nyingine Mby?

Ukitoa ile gym ya kienyeji pale Soweto kuna gym nyingine yenye hadhi Mby?

Viwanja vya michezo je? Bball najua bonanza pale mjini toka 90s hadi pamechoka, kipo kingine? Vya mpira wa miguu je achana na Sokoine ambayo nayo imechoka mbaya. Kuna golf course hata moja Mbeya?

Vp movie theatre?

Supermarket Mby ni kale ka store pale sheli Infinity zamani oilcom 😀 supermarket sio jambo la msingi ila Mby kuna hata a decent market kweli ambayo mtu unaweza pata vitu mbalimbali bila bugudha kweli?

Mbeya mjini ni wapi kule Uhindini au Mwanjelwa maana kote kupo kupo tu.

Kuna hata 4-star hotel in Mby?

Mambo mengine yanaweza kuonekana as petty ila ndo huduma zinazofanya jiji kuwa jiji.

Mkuu mambo ni mengi sana nayoweza kuorodhesha, naijua Mby nje ndani. Pamoja na yote naipenda Mbeya nikipata nauli nitakuja 🤣
Vingine ni kweli na vingine umewaonea Mbeya. Baridi si rafiki wa Swimming pools na nightlife. Uingie kwenye swimming pools na lile baridi, au ulitaka yawe heated, kwa umeme huu?

Mbeya hakuna haja ya masupermarket, kuna masoko kila kona. Masafi na yana bidhaa fresh zinazouzwa. Na masoko ni mazuri sana kwa uchumi kuliko supermarket moja ya kampuni kubwa.

Na miji mingi utakuta maofisi na masoko yamerundikana sehemu moja. Mbeya pametengana, na ni jambo zuri. Sehemu za maofisi hazihitaji vurugu.

Kwenye suala la hotel bado sana. Nafikiri sababu hakuna watalii wala wageni wa kimataifa. Gym hakuna uhitaji, vilima vile ni gym tosha.
 
Arial photo hiyo ndiyo Mtwara? Na ya Mbeya ikoje? Na hii ni ya mwaka gani!?
JamiiForums1766396085.jpg
 
Mbeya inazidiwa Hadi na iringa kimaendeleo ndo mje mlinganishe na Dodoma kweli??

Yaan mbeya ni Jiji la ovyo Sana kwanza miundombinu yake ya ajabu Sana akija kiongozi yoyote wa serikali jam itakayotengenezwa barabarani sio ya kawaida

Mbeya mzunguko wa pesa hakuna unakuta mtu anakaa mjini ila anamashamba huko milimani ko chakula analima huko milimani , anavuna analeta ndani hakuna kununua chakula na uyo anakaa mjini

Mbeya ni Jiji la ovyo saana sijawai kuona.

Mbeya mzunguko wa fedha hakuna? Are you serious or kidding? Bila ya Serikali Dodoma ni zero tena zero kabisa. Mbeya inajiendesha yenyewe
 
Miji hujengwa papaa,hulka ya wagogo na upore wao sio kikwazo,
Dubai ni jangwa,lakini ni bonge la mji,
Hakuna tofauti kati ya tanga na Dar,mtwara,zote Zina fukwe kwenye bahari ya Hindi,lakini mbona Dar imeendelea zaidi?
Hata Arusha hakuna bahari lakini pameendelea,
Kama wenyeji wa sehemu ni kikwzao Cha maendeleo,mbona Dar ni ya wazaramo lakini imeendelea?usikurupuke,miji inaendelea kwa vigezo vingi

Tuchukulie uwekezaji uliofanyika na serikali pale Dodoma( maana Dodoma bila serikali, hata Mpanda patakua juu), kisha uwekezaji ule ungepelekwa Tanga au Mtwara na Serikali ikahamia huko, kwenye miji hiyo yenye bahari na manzari nzuri kabisa za fukwe, hali ingekuaje? Ifike mahali tukubali tu kuwa miji mingi kukua kwake pia Serikali ikiamua ku- boost inasaidia sana.
 
By the way,tusitake miji mizuri huku wa kuitengeneza hayo majiji na sisi.Vipato vya Watanzania vinaendana na majiji yetu.

Ukienda tu hapo Nairobi ukilinganisha na Dar,unaweza ukasema Dar ni kijiji.

Mji kama Nakuru ambapo ni wa 4 kwa pale Kenya,inaizidi hata Mwanza ambapo ni Jiji letu la Pili.umaskini mbaya sana.
Athari za ukomunisti ndio zimetufisha hapo
 
mbeya ni mji wa hovyo sana huwez gundua mwanamke yupi mwanaume yupi wote wanafanana wanawake wamekomaa kama onyango
 
Naunga mkono hoja,..Ila Bora makao makuu yawe chuga tu..au kilimanjaro
 
Naipenda Mbeya ila Mbeya is no better.

Hizo pubs zenyewe Mbeya pazuri, City pub na Mwailubi ni utopolo mtupu. Majina makubwa ukifika utachoka huwezi kukaa hata dakika 5.

Mbeya hakuna viwanja classic. Hizo clubs ni more of vilabu vya pombe than clubs. Kifupi Mbeya hakuna nightlife.

Zamani ilikuwepo Pamodzi sijui iliishia wapi?

Mbeya service ndogo tu hakuna unaweza tafuta kitu cha kawaida kabisa mji mzima na ukakosa utasikia hadi tuagize Dar.

Naipenda Mbeya ila ule mji hauendelei kabisa.
Umefika mara ya mwisho lini Mbeya... Njoo new Mbeya pazuri... Ujionee.. uzuri wake kama ulifika mwaka jana kurudi nyuma usicoment hapa

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
do! hili umenikumbusha niliingia mgahawa mmoja wa kawaida kunywa chai sukari ikawa imeisha muhudumu akang'ata kwa meno kufungua pakiti ya sukari wakati nashaa mwingine akawa anatumia tena meno kufungua pakiti ya majani ya chai
Ukienda migahawa ya kawaida ya vichochoroni lazima upate huduma za vichochoroni... Nchi nzima iko hivyo

Hivi hukuona migahawa, restaurant au hotel Nzuri hadi uende vichochoroni ndio uje kuongelea Mbeya

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom