BoT: Ufafanuzi kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025.

Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika.

Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF.

Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
b1.jpg
B2.jpg
 
Ufafanuzi umekaa kisiasa zaidi
Haha tanzania watoa takwimu wa nje wakisifia wapiga zumari wanaungana nao. Watoa takwimu hao hao wakisema tofauti watawapinga... Kuna sehemu nimeona eti ni waona wivu mabeberu utadhani ndiyo mara ya kwanza wanatoa takwimu ya sarafu iliyofanya vibaya. Kumbe huwa zinatoka mara zote sema haikuwahi Tanzania kupata nafasi hiyo.
 
Urari!! Nitarudi
KAZI ni kipimo cha utu
 
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025. Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika. Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
Vibwengo wa samia bushiri na BOT yao
 
Hii chai tu ya asubuhi hamna kitu. Wameshindwa hata na Malawi?
Malawi Kwacha 1 = TZS 1.53

Wanasema wao ni wachumi wa 1st class wamejaa BoT
 
Kwa mwenendo wa shilingi yetu kuendelea kuwa ya hovyo Huwa muda mwingine natamani kuhamia Burundi au Rwanda kwenye Hela imara.
 
Maelezo meengi /mareefu, lakini hawajakanusha taarifa husika, kwamba "sarafu ya Tanzania ndio imeshika namba katika kufanya vibaya dhidi ya dola!
 
Gavana labda "anatetea" tu kibarua chake. Maelezo ni kwanini hasa shilingi imeporomoka vibaya ndani ya miezi mitatu hayatoshelezi. Kwa mujibu wa hiyohiyo BOT, January 6 mwaka huu USD 1 = shilingi za kitanzania 2367. Kufikia jana dola hiyo Moja ni sawa na shilingi 2618! Anguko la takribani shilingi 251 au 10.6%.

Kwa mwenendo huu ni nini mustakabali wa bei mpya ya mafuta hapo April 🤔
 
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025. Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika. Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
Maelezo meengi /mareefu, lakini hawajakanusha taarifa husika, kwamba "sarafu ya Tanzania ndio imeshika namba katika kufanya vibaya dhidi ya dola!
Waache masikhara kwenye mambo muhimu hawa, kila mtu anaona kinachoendelea mtaani

Tunapenda sana utetezi kulinda image ya watawala ilihali uhalisia uko tofauti.

Vibwengo wa samia bushiri na BOT yao

Huyo Gavana wa BOT naona anafanya Siasa kwenye masuala ambayo yapo serious, naona kama anaichezesha nchi kamali ya kifo, hususani kuhusiana na masuala haya ya Uchumi wa Fedha.
Thamani ya Sarafu ya Shilingi ya Tanzania imeporomoka Sana kupita kiasi. Mfumuko wa bei ni mkubwa sana, hali Kama hii iliwahi kutokea kule nchini Zimbabwe wakati ule wa Utawala wa Rais Robert Mugabe. Kufa kwa thamani ya Dola ya Zimbabwe ilianza kama hivi hivi, na hatimaye nchi hiyo ilikumbwa na janga kubwa sana la Mfumuko wa Bei za bidhaa pamoja na kufa kabisa kwa thamani ya Fedha za nchi hiyo. Mtu akitaka kununua Kilo moja tu ya mchele kutoka dukani ilimlazimu kubeba Fedha nyingi sana kiasi Cha Noti za Fedha zinazoweza kujaa kwenye Container moja lenye ukubwa wa futi arobaini!

Hyperinflation ya Zimbabwe ilianza hivi hivi.
 
Attachments

  • IMG_4781.jpeg
    IMG_4781.jpeg
    197.2 KB · Views: 41

Pale kawekwa kama kivuli kujaza nafasi, mtu alikuwa RAS mara KM wa Hazina ghafla Gavana wa BoT sehemu ambayo inahitaji mtu ambaye amefanya kwenye mashirika makubwa ya fedha duniani na siyo kumchukua mtu kisa ni ndugu wa Makamo.
 
Back
Top Bottom