BoT: Ufafanuzi kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025. Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika. Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
Majibu ya kiasiasa haya, wanajibu kirahisrahis , oh deni himilivu, oh hiv na vile
Bullshit, sarafu una flactuate halaf eti inafanya vizuri?
kwa ground mambo si marahis kama wanavyoona, wanadha watz ni wajinga hawafutalii?
 
Kabisaaa, ila ikishuka wapo kimya? Niliwaambia desemba kutokana na dynamics za soko la dunia ndio limefanya shiliing ionekane imepanda, chawaa wakabisha. Sasa imerudishwa mahali pake wako kimya
Si walisifia mama ni mwana uchumi no 1 duniani na mapambia ya kijinga kibao sahivi wanasema ni soko la dunia, wajinga wakubwa
 
Hata hivyo tunamshukuru sana mama kwa shilingi kuporomoka. Hakika amethubutu na ameweza
 
SINTA SAHAU YULE KAHABA ALIYE TUTOA UCHUMI WA KATI NA KUTURUDISHA WA CHINI NA KUTUAMBIA KUWA UCHUMI UTAPOROMOKA KIDOGO KISHA TUTARUDI UCHUMI WA KATI ...TOKA KIPINDI HICHO UCHUMI UMEPOROMOKA ATUJASIKIA WALA KUTANGAZWA TENA KUWA TUMERUDI UCHUMI WA KATI ....NDIYO MAANA DINI ZIMESEMA KAHABA NI KAHABA TU.
 
Gavana kilaza huyo hatoke hapo kuna Yule Profesa wa Mzumbe Morgogoro anafaq
 
Huyo Gavana wa BOT naona anafanya Siasa kwenye masuala ambayo yapo serious, naona kama anaichezesha nchi kamali ya kifo, hususani kuhusiana na masuala haya ya Uchumi wa Fedha.
Thamani ya Sarafu ya Shilingi ya Tanzania imeporomoka Sana kupita kiasi. Mfumuko wa bei ni mkubwa sana, hali Kama hii iliwahi kutokea kule nchini Zimbabwe wakati ule wa Utawala wa Rais Robert Mugabe. Kufa kwa thamani ya Dola ya Zimbabwe ilianza kama hivi hivi, na hatimaye nchi hiyo ilikumbwa na janga kubwa sana la Mfumuko wa Bei za bidhaa pamoja na kufa kabisa kwa thamani ya Fedha za nchi hiyo. Mtu akitaka kununua Kilo moja tu ya mchele kutoka dukani ilimlazimu kubeba Fedha nyingi sana kiasi Cha Noti za Fedha zinazoweza kujaa kwenye Container moja lenye ukubwa wa futi arobaini!

Hyperinflation ya Zimbabwe ilianza hivi hivi.

Baada ya uchaguzi, dola 1 itafika hata shilingi 5,000.

No REFORM NO ELECTION imepokelewa vizuri sana na umma wa wananchi. Lakini CCM ilivyojaa ushetani wa kudharau wananchi, haitakubali kufanya mabadiliko.

Mpaka sasa EU, individual European countries, USA; zote zimeona hoja za msingi za NO REFORM NO ELECTION, na kuahidi kutumia ushawishi wao kwa Serikali Kwa sasa wameshauri iandaliwe petition, ifikishwe Serikalini, kwenye balozi zao, na UN. Kama Serikali itagomea, hakuna dola itakayoingia nchini kupitia mikopo wala misaada.

Kwenye mazingira hayo, shilingi itachechemea kwa kiwango cha ajabu.
 
hii inaitaji kufanyiwa kazi haraka lakini siyo kuwapa nchi wapinzani
 
"Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022"
Kwanini wanafanya reference ya mwaka 2022 na siyo mwaka 2024 au 2023? Siku hii nchi ikiongozwa na wanao jitambua watendaji wa serikali watashika adabu.
 
Maelezo ya BOT hayajitoshelezi. Thamani ya shillingi imeporomoka sana ukilinganisha na wenzetu wa Afrika mashariki. Mfano leo hii. Mfano shillingi moja ya Kenya inabadilishwa kwa shillingi 20.40 ya Tanzania ambapo hapo mwaka 2024 shillingi moja ya Kenya ilibadilshwa kwa 16.00 ya Tanzania. Mfano wa pili moja ya Tanzania ilibadilshwa kwa shillingi 62.00 ya Uganda mwaka 2024. Leo hii shillingi moja ya Tanzania inabadilishwa kwa shillingi 72.00 ya Uganda. Hivyo na hata wenzetu wa Burundi ambayo ni nchi maskini kabisa shillingi yao ni imara kuliko shillingi ya Tanzania. Namshauri Mhe. Rais afanye uteuzi wa Gavana mwingine na kumuondoa huyu tuliye naye. Wachumi wabobezi wamejaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tafuta aliye na uwezo awe Gavana wa BOT.
 
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025. Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika. Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
Nunueni dhahabu iwe backup ya shilingi, punguzeni riba kwa mabenki ya biashara Ili watu wawekeze zaidi na tuuze kwa wingi inje, process za kupata mikopo ni ngumu sana, na masharti kama ya waganga wa kienyeji, na haitoki kwa muda. Kamateni wote walioficha fedha Ili kuwepo na mzunguko mzuri
 
Wana bodi heshima mbele.

Nakuja kwenu kulilia na kulalamika sana dhidi ya shilingi ya TANZANIA YANGU.Mimi nafanya biashara kati ya Tanzania na Kenya kwa kipindi cha miaka mitatu ya nyuma ,tangu kuanza biashara yangu sijawahi kushuhudia kuporomoka kwa dhamani kama kipindi hiki .Kwa muda wote ilikuwa ina poromoka na kuishia 1KES=20TSH. KWASASA HALI NI MBAYA SANA 1KSH=24TSH

Jamani BOT chini ya MUHA EMANUAL TUTUBA na chini ya wizara ya fedha ya MNYIRAMBA MWIGULU NCHEMA
kuna nini huko?Biashara zimekuwa ngumu huku
 
Ufafanuzi umekaa kisiasa zaidi

Subiri Maza atakapomwaga pesa za Wajomba kwa sjili ya kurudi mjengoji. Hapo ndipo Shilingi itashuka kama hsina mwenyewe. Hii pesa anayomwaga sasa sijui kununus bodaboda na msbango jk cha mtoto. Mambo yataanza rasmi siku akichukua fomu.
 
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MWENENDO WA SHILINGI YA TANZAΝΙΑ DHIDI YA DOLA YA MAREKANI​

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu iliyosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Taarifa hiyo, iliyochapishwa tarehe 19 Machi 2025, ilidai kuwa Shilingi ya Tanzania ndiyo sarafu inayofanya vibaya zaidi duniani. Taarifa hiyo ilitoa maelezo yasiyo sahihi, ikihusisha mwenendo huo na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, ongezeko la deni la taifa, nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, pamoja na utekelezaji wa miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, ambao bado haujaanza.

Kuhusu mwenendo wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita hadi sasa, Shilingi ilishuka kwa asilimia 3.6. Hata hivyo, ni vyema kufahamu kuwa, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2024, Shilingi iliongezeka thamani kwa asilimia 9.51, na kuwa sarafu iliyofanya vizuri zaidi duniani kabla ya kubadilika tena kuanzia Januari 2025.

Hali hii inatokana na mzunguko wa msimu wa mabadiliko ya fedha za kigeni nchini na sera ya fedha za kigeni ya Benki Kuu, inayoruhusu kubadilika kwa thamani ya sarafu kulingana na nguvu za soko. Chini ya sera hii, thamani ya Shilingi inaendelea kuamuliwa na nguvu ya soko na upatikanaji wa fedha za kigeni sokoni, huku Benki Kuu ikishiriki kwa kiwango kidogo.

Viashiria vya uchumi wa Tanzania vinaonesha ukuaji mzuri, utulivu wa bei, kupungua kwa nakisi ya urari wa malipo ya kawaida, na uimara wa sekta ya fedha inayosaidia utulivu wa Shilingi ya Tanzania kwa muda wa kati na mrefu. Uchumi ulikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika.

Mfumuko wa bei umeendelea kuwa thabiti na wa chini, ukifikia asilimia 3.1 mnamo Februari 2025, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2022. Kinyume na madai yaliyotolewa katika makala iliyochapishwa, deni la taifa bado ni himilivu, ambapo uwiano wa deni kwa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 41.1 mwaka 2023/24, chini ya kiwango cha asilimia 50 kinachopendekezwa na IMF.

Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 3.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.7 ya Pato la Taifa mwaka 2024, kutokana na kuimarika kwa mauzo ya nje, hasa katika sekta za kilimo, madini na utalii. Hii inafafanua kwa nini Shilingi iliongezeka thamani kwa kasi kubwa mwishoni mwa Desemba 2024. Zaidi ya hayo, mwenendo huu unalingana na ripoti zilizochapishwa na Benki ya Dunia, Benki inayowezesha Miamala ya Kimataifa (BIS), IMF, na mashirika ya kimataifa ya ukadiriaji wa mikopo.

Benki Kuu inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuhakikisha utulivu wa bei kwa kutekeleza sera za fedha zinazolenga kudumisha uthabiti wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utulivu wa Shilingi ya Tanzania.

Pia soma > Shilingi ya Tanzania yatajwa kama fedha iliyofanya vibaya zaidi Duniani dhidi ya Dola ya Marekani kwa mwaka 2025
BOT imekuwa taasisi ya Kisiasa, huyu Gavana uteuzi wake ulikuwa wa kitaaluma au kisiasa zaidi
 
Majukumu ndugu yangu Hadi nimesusa forum kwa muda
Ninakutakia maisha mema wewe pamoja na familia yako yote. Kikubwa uzima mkuu, masuala mengine (kama vile pesa) Mungu atatujalia tu one day.
 
Back
Top Bottom