Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe ni chai...!??Huu upuuzi ulishaletwa humu
hapana ndugu, bukta yangu sikuichukua. na kwakuwa nilikuwa naitumia usiku wakati wa kuoga tu, naamini majirani hawakuikariri.ko buktaa yko hukuichukua.?
😁😁😁 ndio mkuu. mimi hupendelea kuvaa bukta / pensi wakati naenda kuoga.
hapana kiongozi. si kitu cha kipuuzi kama unavyo dhani. najaribu kuvaa uhusika kama tukio hilo lingetukia kwangu.Kumbe ni chai...!??
yamkini taulo ni zuri, ila mimi ni mrefu kwa kimo, hivyo huwa navaa bukta na kubeba taulo begani.
Kuna ukweli ktk usemalo.Labda alikuwa anachepuka kweli na bukta ikawa sababu
Katika maisha kuna matukio huwa yanatokea ukifikiri umeharibu kumbe umeokoa
Hii chai ya jamaa imewekwa tangawizi. Boxer inanasaje kwenye neti wakati unaikung'uta afu iruke kama tenesi mpaka chumba cha pili afu ikatue kwenye switch chumba cha jirani?Aisee hata mm nimeshtuka, ila nimeshtuka zaidi boxer yenye maji kuruka kwenye neti kisha ikadunda na kwenda chumba cha pili 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Asante kwa ufahamu huo, ila ktk hili nadhani ni tabia ilijenga mazoea. kwasasa ni ngumu kuvaa taulo tupu wakati naenda kuoga.Sawa sana, ila tambua pia kuna mataulo makubwa...
Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
Hiyo sio boxer ni nyoka koboko...imagine unakung'uta bukta inarukia chumba cha pili tena ikiwa imeloa 🤣🤣🤣
Dah kuna kamtihani coz umechelewa kulitolea maelezo... lkn pia ni kwa namna gani jamaa atapokea maelezo yako kuusu kulichotokea akuelewe... lkn kwa mawazo yangu naona utafute watu wazima wenye busara ata wawili wa eneo lile mwende mkamueleze jamaa. Ili kuokoa ndoa yao..Habari wana JF.
Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.
Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.
Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.
Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.
Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.
Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.
Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.
ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.
Sio mara ya kwanza kusoma. Jamaa kaamua aulete hapa achangamshe jamviHuu upuuzi ulishaletwa humu
mtazamo wako wa ndani zaidi ndio uliokupa majibu hayo. ila nakuomba uniamini ktk hili kwasababu ni accidentally case.Hii chai ya jamaa imewekwa tangawizi. Boxer inanasaje kwenye neti wakati unaikung'uta afu iruke kama tenesi mpaka chumba cha pili afu ikatue kwenye switch chumba cha jirani?
niliomba ushauri huo kwa dada na shemeji yangu ila walinikatalia na kusema hii itawapa watu ukweli kwamba pengine mimi ni ndio dereva fulani wa maroli ambaye anasadikiwa aliwahi kulala chumba hicho wakati jamaa hayupo.Dah kuna kamtihani coz umechelewa kulitolea maelezo... lkn pia ni kwa namna gani jamaa atapokea maelezo yako kuusu kulichotokea akuelewe... lkn kwa mawazo yangu naona utafute watu wazima wenye busara ata wawili wa eneo lile mwende mkamueleze jamaa. Ili kuokoa ndoa yao..
Asante sana ndugu. naona ushauri wako ni njia ya kuanzia.mtihani mzito sana kwa huyo dada...pengine huyo jamaa pia alikuwa anasubiri tu mwanamke aingie kingi kwa njia yeyote ile ili ahalalishe alichokipanga
sasa cha kufanya tafuta namba ya huyo jamaa mweleze uhalisia wa hilo tukio mueleze kwa kina ili maamuzi yabaki kwake kusuka au kunyoa
Unataka jamaa auliwe? Mapenzi ni kitu kingine usijaribu kufanya masiharaKm wewe kweli ni mwanaume kamili na unajimini ulipaswa kumuitabmwanaume mwenzako na umwambie hali ilivyo
Umwambie uhalisia sababu hamna ukichokufanya na unaogopa kuvunja ndoa ya mwanaume mwenzako bila sababu.
Huwezi kuogopa kusimamia kitu kidogo km hicho.Yeye ndo achague kusuka au kunyoa.
Simu zinarekodiwa usijaribu huo mchezo utafunguliwa kesi na ushahidi utapatikana.Tafuta demu aliyeaxhwa umtafuneAsante sana ndugu. naona ushauri wako ni njia ya kuanzia.
naamini nikitumia njia ya simu itaniweka salama, hata jamaa akiwa na ghadhabu hata weza kunidhuru papo kwa hapo.
Nakushukuru.