Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Kumbe ni chai...!??
hapana kiongozi. si kitu cha kipuuzi kama unavyo dhani. najaribu kuvaa uhusika kama tukio hilo lingetukia kwangu.
nini ingekuwa hatma ya ndoa yangu?
that's why nimeomba ushauri ili nithubutu kutenda wema kama itawezekana.
 
Aisee hata mm nimeshtuka, ila nimeshtuka zaidi boxer yenye maji kuruka kwenye neti kisha ikadunda na kwenda chumba cha pili 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hii chai ya jamaa imewekwa tangawizi. Boxer inanasaje kwenye neti wakati unaikung'uta afu iruke kama tenesi mpaka chumba cha pili afu ikatue kwenye switch chumba cha jirani?
 
Habari wana JF.

Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.

Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.

Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.

Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.

Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.

Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.

Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.

ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.
Dah kuna kamtihani coz umechelewa kulitolea maelezo... lkn pia ni kwa namna gani jamaa atapokea maelezo yako kuusu kulichotokea akuelewe... lkn kwa mawazo yangu naona utafute watu wazima wenye busara ata wawili wa eneo lile mwende mkamueleze jamaa. Ili kuokoa ndoa yao..
 
Hii chai ya jamaa imewekwa tangawizi. Boxer inanasaje kwenye neti wakati unaikung'uta afu iruke kama tenesi mpaka chumba cha pili afu ikatue kwenye switch chumba cha jirani?
mtazamo wako wa ndani zaidi ndio uliokupa majibu hayo. ila nakuomba uniamini ktk hili kwasababu ni accidentally case.
sikutegemea nguo ichomoke mkononi wakati naikung'uta.
 
Dah kuna kamtihani coz umechelewa kulitolea maelezo... lkn pia ni kwa namna gani jamaa atapokea maelezo yako kuusu kulichotokea akuelewe... lkn kwa mawazo yangu naona utafute watu wazima wenye busara ata wawili wa eneo lile mwende mkamueleze jamaa. Ili kuokoa ndoa yao..
niliomba ushauri huo kwa dada na shemeji yangu ila walinikatalia na kusema hii itawapa watu ukweli kwamba pengine mimi ni ndio dereva fulani wa maroli ambaye anasadikiwa aliwahi kulala chumba hicho wakati jamaa hayupo.
hivyo hawakutaka niuchochee moto kwa kutafuta watetezi.
 
mtihani mzito sana kwa huyo dada...pengine huyo jamaa pia alikuwa anasubiri tu mwanamke aingie kingi kwa njia yeyote ile ili ahalalishe alichokipanga

sasa cha kufanya tafuta namba ya huyo jamaa mweleze uhalisia wa hilo tukio mueleze kwa kina ili maamuzi yabaki kwake kusuka au kunyoa
Asante sana ndugu. naona ushauri wako ni njia ya kuanzia.
naamini nikitumia njia ya simu itaniweka salama, hata jamaa akiwa na ghadhabu hata weza kunidhuru papo kwa hapo.
Nakushukuru.
 
Km wewe kweli ni mwanaume kamili na unajimini ulipaswa kumuitabmwanaume mwenzako na umwambie hali ilivyo

Umwambie uhalisia sababu hamna ukichokufanya na unaogopa kuvunja ndoa ya mwanaume mwenzako bila sababu.

Huwezi kuogopa kusimamia kitu kidogo km hicho.Yeye ndo achague kusuka au kunyoa.
Unataka jamaa auliwe? Mapenzi ni kitu kingine usijaribu kufanya masihara
 
Asante sana ndugu. naona ushauri wako ni njia ya kuanzia.
naamini nikitumia njia ya simu itaniweka salama, hata jamaa akiwa na ghadhabu hata weza kunidhuru papo kwa hapo.
Nakushukuru.
Simu zinarekodiwa usijaribu huo mchezo utafunguliwa kesi na ushahidi utapatikana.Tafuta demu aliyeaxhwa umtafune
 
Back
Top Bottom