BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

naona Mama anajaribu kuishi kama JK....good progress..

Angalizo: afahamu tu hawezi kumridhisha kila mtu...
JK ?! Una maana JK aliyeachia mchakato wa katiba uharibike pamoja na mabilioni ya pesa kupotea ??!! You must be joking !!
 
Tofauti ni zito Kabwe alikutana na Samia akaanza kuzungumzia kuhusu Chadema badala ya kuzungumzia maada waliyoendea pale Dodoma!Lissu kakutana na Samia wamezungumzia ya Chadema na Ccm au serikali, ktk hilo hamna shida yeyote
Nyie akili zenu finyu kweli!!

Unashindwa hata kutambua Zitto alizungumzia suala hilo kama nani.

Punguzeni sifa. Hakuna jipya, mlimzodoa Zitto kafanya yale yale na aliyemzodoa halafu mnashangilia.

Dah
 
Ni muda sasa tokea uchaguzi wa 2020 kwisha chadema walijiwekea msimamo wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi na hata serikali ya ccm iliyoundwa chadema walikwenda mbali hata kuwakataa wabunge wake wa viti maalum waliotokana na uchaguzi huo wajiwekea msimamo wa kutoshirikiana na viongozi wakuu wa ccm na kukataa mkutano wa vyama vya siasa wa dodoma kwa na kuwatuhumu viongozi wengine walioshiriki mkutano huo kua ni mamluki wa ccm.

Ukweli ni kwamba msimamo kama huo ni msimamo wa kitoto kwa kua hakuna uwezekano wa kufanya siasa kwa kutojihusisha na kushirikiana na serikali ilyopo madarakani vinginevyo watuambie watumie mtutu wa bunduki ni pia mnaweza kutofatiana na serikali ilyopo madarakani lakini siyo ktk mambo kitaifa kitendo alichokifanya tundu lisu jana kukutana na Rais samia ni tukio linadhihirisha ukweli ulifichika ndani ya chadema kuwa wana siasa siyo maadui.

 
kuna mijitu mijinga kweli, rejea press ya ikulu ya nani kaomba kuonana na nani. MMM na Maria wanawashika makalio
 
Ukweli ni kwamba asipotimiza aliyoambiwa na Lisu hakitaeleweka
 
Chawa chonganishi mmeanza kuteseka na wivu wenu wa mkyundu wazi
 
Mbowe aachiwe bila masharti na siasa za majukwaani ziendelee bila figisu. CCM bila police na tume ya uchaguzi ya ccm ni weupe kabisa

Ccm haipendwi tena na watanzania walio wengi
 
Acha ujinga ndugu! Rais katumia zaidi ya saa moja kumsikiliza Lissu na kuzungumza (sio kuhutubia) juu ya mambo mengi kulingana na aliyoyaleta Lissu kwa manufaa ya Tanzania kwa ujumla tena wakiwa ugenini.
Jambo hili sio dogo kiasi cha kutaka kulinganisha na utoto na unafiki ule uliofanyika Dodoma.
Mnatumia nguvu kubwa kupotosha wakati jambo la jana limechukuliwa kwa uzito mkubwa sana na vyombo vikubwa vya habari duniani.
 
Unavuliwaje koti tena mbele ya camera? Halafu wa nasema yeye ndio kaomba aonane the nae huyu mtu kichwani ziko sawa kweli?
 
kuna mijitu mijinga kweli, rejea press ya ikulu ya nani kaomba kuonana na nani. MMM na Maria wanawashika makalio
PhD, unakosea sana kujitambulisha kwa utambulisho huo maana unatupotosha kwa kudhani tutakuta umeandika ya maana kumbe ngumbaru!
Maombi ya "kuzungumza" na Rais ni ya tangu March 2021
 
CDM hawawezi kuja kupata kiongozi kama FAM. Mbowe atakumbukwa vizazi na vizazi vya wapenda haki na demokrasia ya nchi hii.
FAM atakumbukwa kwa kujipa UWENYEKITI wa CDM wa maisha na kutumia chama kama mradi wa kumuinguzia pesa
 
Mama anazidi kuonesha jinsi alivyo na moyo wenye hekima, utu na upendo.

Tazama, amesafiri kutoka Ufaransa kwenda Ubelgiji akiendelea na ziara yake barani Ulaya. Kufika Brussels, Ubelgiji anapokea maombi ya Lissu akiomba waonane.

Kwa moyo wenye upendo alionao Mama Samia unadhani angekataa? Akatae vipi wakati yeye ni Mama wa kila Mtanzania aliyepo ndani na nje ya Nchi yetu?

Akatae vipi wakati yeye habagui? Kwake kila mmoja ni sawa, uwe CCM, ACT au Chadema mbele ya Rais Samia kila mmoja ni sawa.

Wameongea Nini? Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema ni mambo yanayohusu ustawi wa Nchi yetu. Wooow just woow.

Hongera Rais Samia, Hongera Mama yetu, Tuko salama kwenye mikono yako.

Kazi zako, Mipango yako, Upendo wako tuufananishe na nini? Jibu ni hakuna. Wewe ni Samia, Rais wetu na Mama yetu.
 
Huko ndiyo kuomba msamaha kwenyewe sasa. Njia yeyote ya Mbowe kutoka rumande bila hukumu au kutoroka (jailbreak) ndiyo inaitwa msamaha.

Alichoongea TUNDU LISSU na aluchoongea Zitto Kabwe ni sawa kasoro mpangilio wa maneno
 
Huko ndiyo kuomba msamaha kwenyewe sasa. Njia yeyote ya Mbowe kutoka rumande bila hukumu au kutoroka (jailbreak) ndiyo inaitwa msamaha.

Alichoongea TUNDU LISSU na aluchoongea Zitto Kabwe ni sawa kasoro mpangilio wa maneno
Sema according kwa uelewa wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…