Nashangaa bado mnalazimisha Mbowe aonekane mkosaji bila kutuambia kosa lake ni lipi?
Kama Lissu kwenye mkutano wake na Samia amemwambia Mbowe aachiwe huru bila masharti yoyote hapa sioni tatizo lolote, hiki ndicho Chadema wanachokitaka, sio kutuma washenga wapeleke habari ya kuomba msamaha.
Nyie mnatengenezea watu matatizo kwa sababu za kisiasa halafu mnalazimisha wafanye mnavyotaka ili wawe huru, huu mtego Chadema waliugundua mapema sana.
Kesi ya Mbowe kwa mtazamo wangu ipo hivi:
Mens rea: ipo wazi na jamuhuri imethibitisha intentions ya wahusika kutaka kuleta taharuki.
Actus rea: serikali imeshindwa kuthibitisha pasipo shaka kulikuwa na hatari ya mipango kutekelezwa at anytime.
Criminal case inataka ushahidi wa hayo mambo mawili bila ya yote kwa pamoja hakuna kesi. Nakubali kabisa kwenye kuthibitisha ‘actus rea’ tumesikia vituko vingi mahakamani mpaka kuonekana kesi ya ovyo.
So Mbowe for his part ingekuwa busara kukubali his stupidity mapema ya kudhani angeweza isumbua serikali for a mission which wa bound to amount to nothing anyway. An apology may be would have helped aina maana awezi shinda hiyo kesi yake based on weak government evidence.
As for Lissu kumsikiliza na kumwamini huyo mtu inataka ujitoe ufahamu kweli kweli; leo ataponda posho za watu kadhaa. Halafu kesho na yeye atalilia posho hizo hizo akidai ni haki yake kisheria, sasa kwani posho za wenzake na wenyewe chanzo chake si ni sheria.
Leo atasema atambui serikali kwa sababu ya hila za kwenye uchaguzi, kesho atasema tum support raisi wetu.
Sababu za kususia bunge ilikuwa uchaguzi, sasa hivi waliopo bungeni sio wanachama wetu; si mlisusia hizo nafasi wenyewe sasa tatizo lipo wapi kuona wenzenu wamezichukua.
Mtu anaeweza sikiliza ushauri wa Lissu is reasoning is beyond me.