BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Wale waliokuwa wanagomea vikao na serikali hapa nchini wanachanganyikiwa, Lissu level nyingine, anajua maana ya Siasa, tofauti na mburura zilizo hapa nchini. Zitto kabwe alisema mapema...
Chadema hawakuhitaji mshenga (Msajili wa Vyama vya siasa na IGP) kuwakutanisha na Raisi.
 
Blessed are the peacemakers for they shall be called children of God. Asante sana mama SSH
 
Kuna Utaratibu upo ndani ya Chama Tawala kusifia chochote anachosema au kufanya Mwenyekiti wao.Toka Enzi za Baba wa Taifa, chini ya kauli mbiu ya "Zidumu Fikra za Mwenyekiti"

Ni jambo jema kusifia,lakini ni vizuri tuwe na msimamo! Leo Rais kakutana na Wapinzani unasifia,kesho amekataa kukutana nao unasifia pia! Tusiwe watu wa njia mbili,mpaka hatujulikani tunachokiamini na kukisimamia.

Tusifie kimantiki,sio kwa adhima ya kumfurahisha unayemsifia ili ujenge ukaribu na mazingira ya kupewa wadhifa!

Mungu ibariki Tanzania
 
MUNGU wetu wa mbinguni, ninakushuruku kwa jambo hili lililofanywa na viongozi hawa.

Ni wewe ndiye ulitupatia nchi hii sisi sote bila kujali itikadi zetu, ili ikawe makazi yetu na vizazi vyetu vyote. Ukazuie mipango miovyo ya mawakala wa ibilisi kukwamisha mchakato huu. Tendo hili likawe mwanzo mpya kwa siasa za kiungwana na kuchukuliana madhaifu yetu kwa ustawi wa Tanzania na sisi watu wake.​

AMINA 🙏
 
Kwani tatizo liko wapi mmezoea siasa za ubabe na visasi kwa hiyo nyie sukuma gang mtapata shida huyu Mama ni muungwana sana na mstarabu
 
Acha ujinga ndugu! Rais katumia zaidi ya saa moja kumsikiliza Lissu na kuzungumza (sio kuhutubia) juu ya mambo mengi kulingana na aliyoyaleta Lissu kwa manufaa ya Tanzania kwa ujumla tena wakiwa ugenini.
Jambo hili sio dogo kiasi cha kutaka kulinganisha na utoto na unafiki ule uliofanyika Dodoma.
Mnatumia nguvu kubwa kupotosha wakati jambo la jana limechukuliwa kwa uzito mkubwa sana na vyombo vikubwa vya habari duniani.
View attachment 2121678
Kama kuna mtu anaakereka kwa picha hii bora asage wembe anywe tu
 
Yaani kitu kidogo tu tuanasahau madhira yanayotukumba kila mwaka nenda rudi. Tumeshakuwa kama maboya yasiyojitaambua kabisa.

Leo naona kila kona mayoweee kibao. Makelele kibao mkiulizwa je kuna tija gani kwa chama chetu na watanzania kwa ujumla hakuna jibu.

Mnatia aibu sana.
 
Baada ya MH. Rais Samia kukutana na Tundu Lisu huko Ubeligiji ni dhahiri shahiri sasa uhasama ulio kuwapo kati ya Lisu na Serikali umeisha.

Picha zinaonyesha Lisu akiwa na furaha na tabasamu lisilo kifani mbele ya Rais Samia ni ishara tosha kuwa amemaliza chuki na uhasama.

Sasa ni wakati wa wanachama wote wa Chadema tuunge mkono Serikali hii ya awamu 6 chini ya Amiri Jeshi Mkuu Mama yetu Samia Suluhu Hassa.

Mungu Ibariki Tanzaania.
 
Ni mpaka pale mama atakapoanza kutekeleza sehemu ya yale matakwa saba lisu, moja ni linaanza kesho
 
Nashangaa bado mnalazimisha Mbowe aonekane mkosaji bila kutuambia kosa lake ni lipi?

Kama Lissu kwenye mkutano wake na Samia amemwambia Mbowe aachiwe huru bila masharti yoyote hapa sioni tatizo lolote, hiki ndicho Chadema wanachokitaka, sio kutuma washenga wapeleke habari ya kuomba msamaha.

Nyie mnatengenezea watu matatizo kwa sababu za kisiasa halafu mnalazimisha wafanye mnavyotaka ili wawe huru, huu mtego Chadema waliugundua mapema sana.
Kesi ya Mbowe kwa mtazamo wangu ipo hivi:

Mens rea: ipo wazi na jamuhuri imethibitisha intentions ya wahusika kutaka kuleta taharuki.

Actus rea: serikali imeshindwa kuthibitisha pasipo shaka kulikuwa na hatari ya mipango kutekelezwa at anytime.

Criminal case inataka ushahidi wa hayo mambo mawili bila ya yote kwa pamoja hakuna kesi. Nakubali kabisa kwenye kuthibitisha ‘actus rea’ tumesikia vituko vingi mahakamani mpaka kuonekana kesi ya ovyo.

So Mbowe for his part ingekuwa busara kukubali his stupidity mapema ya kudhani angeweza isumbua serikali for a mission which wa bound to amount to nothing anyway. An apology may be would have helped aina maana awezi shinda hiyo kesi yake based on weak government evidence.

As for Lissu kumsikiliza na kumwamini huyo mtu inataka ujitoe ufahamu kweli kweli; leo ataponda posho za watu kadhaa. Halafu kesho na yeye atalilia posho hizo hizo akidai ni haki yake kisheria, sasa kwani posho za wenzake na wenyewe chanzo chake si ni sheria.

Leo atasema atambui serikali kwa sababu ya hila za kwenye uchaguzi, kesho atasema tum support raisi wetu.

Sababu za kususia bunge ilikuwa uchaguzi, sasa hivi waliopo bungeni sio wanachama wetu; si mlisusia hizo nafasi wenyewe sasa tatizo lipo wapi kuona wenzenu wamezichukua.

Mtu anaeweza sikiliza ushauri wa Lissu is reasoning is beyond me.
 
😀😀😀wacha wafurahi na wao walikuwa wanatamani sema walikosa namna
 
Naona Mama anajaribu kuishi kama JK....good progress..

Angalizo: Afahamu tu hawezi kumridhisha kila mtu...

La muhimu atende haki amridhishe Mungu kwani ndio marejeo yetu kwake na ndiye hakimu
 
Hakuna asiyependa amani, hizo tabia za hovyo walifundishwa na jiwe pamoja na wafuasi wake kina Bashite. Binadam aliye na moyo wa nyama nahisi amefurahi jambo jema na lenye tija kwa Taifa.

KUSIFIA kilicho bora sio DHAMBI.
 
Kesi ya Mbowe kwa mtazamo wangu ipo hivi:

Mens rea: ipo wazi na jamuhuri imethibitisha intentions ya wahusika kutaka kuleta taharuki...
Hapa unajiona msomi wa sheria kumbe mjuaji wa KAWAIDA SANA. Tuoneshe point ya mens rea iliyothibidtishwa na seruskali toka kwa Mbowe.

Msg kwamba Mbowe na URIO walichart kwako ndo mens rea inapostand? Au maelezo ya onyo yaliyokanushwa na washtakiwa ndo mens rea ulipoiona?
 
Back
Top Bottom