Mama anazidi kuonesha jinsi alivyo na moyo wenye hekima, utu na upendo.
Tazama, amesafiri kutoka Ufaransa kwenda Ubelgiji akiendelea na ziara yake barani Ulaya. Kufika Brussels, Ubelgiji anapokea maombi ya Lissu akiomba waonane.
Kwa moyo wenye upendo alionao Mama Samia unadhani angekataa? Akatae vipi wakati yeye ni Mama wa kila Mtanzania aliyepo ndani na nje ya Nchi yetu?
Akatae vipi wakati yeye habagui? Kwake kila mmoja ni sawa, uwe CCM, ACT au Chadema mbele ya Rais Samia kila mmoja ni sawa.
Wameongea Nini? Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema ni mambo yanayohusu ustawi wa Nchi yetu. Wooow just woow.
Hongera Rais Samia, Hongera Mama yetu, Tuko salama kwenye mikono yako.
Kazi zako, Mipango yako, Upendo wako tuufananishe na nini? Jibu ni hakuna. Wewe ni Samia, Rais wetu na Mama yetu.