BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Tatizo la samia ni dogo tu bado anafuga majitu fulani yaliyo kuwa yanatumiwa na magufuli kuumiza watu
Uko sahihi kabisa. Kuna watu inafaa mama aachane nao. Simon Sirro awekwe pembeni, amemuaminisha mama uongo juu ya kesi ya Freeman Mbowe hadi mama akaongea na BBC (chombo cha kimataifa), kwamba Mbowe ni gaidi.

Hii list ya kina Kingai wanatakiwa wahojiwe vizuri baada ya hili la Mbowe na wenzake kufika mwisho
 
Asichokielewa Lissu ni kwamba Chief Hangaya anataka kuendelea kuwa Rais baada ya term hii, kwa gharama yoyote ile. Kwahiyo, kufikiria kwamba Chief Hangaya somehow atatengeneza a level playing field kabla ya uchaguzi wa 2025 ni kujipa matumaini hewa!
Hata asipotengeneza kabla ya 2025, anaweza kutengeneza kabla ya 2030, Tanzania bado ipo sana mkuu.
 
"Huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu na kuwa wamoja kama taifa, ni wakati wa kufarijiana, kuonyesha upendo, udugu wetu, kudumisha amani yetu, kuenzi utu wetu, uzalendo wetu na utanzania wetu.

Huu si wakati wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni wakati wa kutazama mbele kwa matumaini na kujiamini. Huu sio wakati wa kutazama yaliyopita lakini ni wakati wa kutazama yaliyo mbele.

Huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu. Si wakati wa kunyosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono. Ni wakati wa kufutana machozi ili tuweke nguvu zetu pamoja na tujenge Tanzania yetu, Tanzania mpya."

By Mhe. Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_19 Machi, 2021

 
Baada ya kuona kesi ya ugaidi inaenda kumchimbia kaburi la kiutawala kimataifa ndio akafunga safari kwenda kutafuta pakutokea kwa Tundu Lisu, hahahahaha na bado
Na safari ikapitia Ufaransa kwanza maana ingekua straight Ubelgiji, ingekua wazi mno.
 
Mbona una hasira???
 
kuna mijitu mijinga kweli, rejea press ya ikulu ya nani kaomba kuonana na nani. MMM na Maria wanawashika makalio
Hivi ulitegemea press iandikwe vinginevyo!? Huyo ni Rais wa nchi lazima awe respected kwa kuiweka hivyo ilivyowekwa.
 
Tulia mafundi wa Siasa wawachezeshe. CCM chama bora kabisa Cha kisiasa katika Afrika, political score, mlisubiri kushinda kortini mpate political mileage? Sasa imekuwa hijacked
Jina linaakisi fikra zako.
 
Uelewa wako ni mpana sana. Hustahili kupewa nafasi ya U-DC.
 
Sijui kama wanakuelewa.

Cc Ritz chinembe Crimea comte johnthebaptist YEHODAYA Pulchra Animo
 
Kuna wana CCM baadhi hawatapenda kitendo cha kiuungwana alichoonyesha mama kukutana na Lissu huko ughaibuni.

Wao wanataka tubakie na siasa zilezile za chuki, kuwindana mitaani mchana mchana na kuundiana kesi za kubambika.

Sasa wana CCM wenzangu ni kwamba hizo siasa zishaondoka; sote ni watanzania na ni ndugu.

Katiba mpya oyeee
 
Lissu hajawahi kuwa na shida na Samia, ilikua ni suala la muda tu. Aliyemfanya Lissu awe nje ya nchi unamjua.
 
Kuweka sawa. Mara ya kwanza alikutana na TL akiwa kwenye kitanda cha maumivu tarehe 28 Novemba 2017, Nairobi Hospital nchini Kenya.
Jana, walikutana Brussels, Ubelgiji.

Tuache siasa pembeni. SSH ameonesha ni binadamu kindaki ndaki.
Tusirithi maadui.
 
Mwambie asubiri Judge atakavyoiainisha hiyo kesi kesho tr 18/02/2022.

Cc Kilatha
 
Wewe kiwango chako cha kuelewa mambo ya sheria ni cha Inspector Swila.

Bila bila
 
Hiki ni kitendo cha kiuungwana mno, kwa hili mama kula TANO za kwangu.

Ni mwanzo mzuri mno wa Lissu kukutana na IKULU ya Tanzania 🇹🇿 kwa mazunguzo; siasa si uadiu kama vile baadhi ya wana CCM walituaminisha.

Kwa aliyopitia Lissu ni haki yake kupata neno fupi la matumaini toka kwa Rais wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…