BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Tatizo la samia ni dogo tu bado anafuga majitu fulani yaliyo kuwa yanatumiwa na magufuli kuumiza watu
Uko sahihi kabisa. Kuna watu inafaa mama aachane nao. Simon Sirro awekwe pembeni, amemuaminisha mama uongo juu ya kesi ya Freeman Mbowe hadi mama akaongea na BBC (chombo cha kimataifa), kwamba Mbowe ni gaidi.

Hii list ya kina Kingai wanatakiwa wahojiwe vizuri baada ya hili la Mbowe na wenzake kufika mwisho
 
Asichokielewa Lissu ni kwamba Chief Hangaya anataka kuendelea kuwa Rais baada ya term hii, kwa gharama yoyote ile. Kwahiyo, kufikiria kwamba Chief Hangaya somehow atatengeneza a level playing field kabla ya uchaguzi wa 2025 ni kujipa matumaini hewa!
Hata asipotengeneza kabla ya 2025, anaweza kutengeneza kabla ya 2030, Tanzania bado ipo sana mkuu.
 
"Huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu na kuwa wamoja kama taifa, ni wakati wa kufarijiana, kuonyesha upendo, udugu wetu, kudumisha amani yetu, kuenzi utu wetu, uzalendo wetu na utanzania wetu.

Huu si wakati wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni wakati wa kutazama mbele kwa matumaini na kujiamini. Huu sio wakati wa kutazama yaliyopita lakini ni wakati wa kutazama yaliyo mbele.

Huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu. Si wakati wa kunyosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono. Ni wakati wa kufutana machozi ili tuweke nguvu zetu pamoja na tujenge Tanzania yetu, Tanzania mpya."

By Mhe. Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania_19 Machi, 2021

Samia-na-Lissu.jpg
Samia-na-Lissu2.jpg
 
Baada ya kuona kesi ya ugaidi inaenda kumchimbia kaburi la kiutawala kimataifa ndio akafunga safari kwenda kutafuta pakutokea kwa Tundu Lisu, hahahahaha na bado
Na safari ikapitia Ufaransa kwanza maana ingekua straight Ubelgiji, ingekua wazi mno.
 
Wale waliokuwa wanagomea vikao na serikali hapa nchini wanachanganyikiwa, Lissu level nyingine, anajua maana ya Siasa, tofauti na mburura zilizo hapa nchini.

Zitto kabwe alisema mapema, Chadema wakambeza, Sasa Lissu anafata muelekeo wa ZZK, anaachana na Chadema wenye mawazo mgando, ya kizamani, wanaimba katiba tu kama kasuku, mwenzao anaozea jela, wao wanakusanya Hela wanagawana.

Kama nyie wanaume mshambulieni Lissu mitandaoni tuone
Mbona una hasira???
 
kuna mijitu mijinga kweli, rejea press ya ikulu ya nani kaomba kuonana na nani. MMM na Maria wanawashika makalio
Hivi ulitegemea press iandikwe vinginevyo!? Huyo ni Rais wa nchi lazima awe respected kwa kuiweka hivyo ilivyowekwa.
 
Tulia mafundi wa Siasa wawachezeshe. CCM chama bora kabisa Cha kisiasa katika Afrika, political score, mlisubiri kushinda kortini mpate political mileage? Sasa imekuwa hijacked
Jina linaakisi fikra zako.
 
Ukweli ni kwa Samia ndiyo aliyetaka kukutana na Lissu na wameweka hivi kwa heshima tu. Hii safari ya kutoka France haikuwa na ulazima hakuna mkataba wowote wala nini lengo ni kumuona Lissu lakini kisiasa ni lazima Lissu aseme ndiye aliyeomba. Mama ameona ukweli baada ya kudanganya kwenye issue ya mbowe hasa na IGP sirro ndiyo maana wame set up kamati ya kumtimua Sirro. Ukweli ni kwamba Mama anampenda Lissu kuliko zamani kuanzia hata wakati wa Magufuli Hii ndiyo ilikuwa tofauti yao kubwa. Hata safari ya kenya ya kumuangalia Lissu Mama alilazimisha . Ni ngumu sana kumchukia Lissu very likable guy na clean. Lakini kwa uelewa wangu Chadema walikataa kukutana kama group na wengine hawajawahi kukutana na Raisi moja kwa moja.
Uelewa wako ni mpana sana. Hustahili kupewa nafasi ya U-DC.
 
Kuna Utaratibu upo ndani ya Chama Tawala kusifia chochote anachosema au kufanya Mwenyekiti wao.Toka Enzi za Baba wa Taifa, chini ya kauli mbiu ya "Zidumu Fikra za Mwenyekiti"

Ni jambo jema kusifia,lakini ni vizuri tuwe na msimamo! Leo Rais kakutana na Wapinzani unasifia,kesho amekataa kukutana nao unasifia pia! Tusiwe watu wa njia mbili,mpaka hatujulikani tunachokiamini na kukisimamia.

Tusifie kimantiki,sio kwa adhima ya kumfurahisha unayemsifia ili ujenge ukaribu na mazingira ya kupewa wadhifa!

Mungu ibariki Tanzania
Sijui kama wanakuelewa.

Cc Ritz chinembe Crimea comte johnthebaptist YEHODAYA Pulchra Animo
 
Kuna wana CCM baadhi hawatapenda kitendo cha kiuungwana alichoonyesha mama kukutana na Lissu huko ughaibuni.

Wao wanataka tubakie na siasa zilezile za chuki, kuwindana mitaani mchana mchana na kuundiana kesi za kubambika.

Sasa wana CCM wenzangu ni kwamba hizo siasa zishaondoka; sote ni watanzania na ni ndugu.

Katiba mpya oyeee
 
Baada ya MH. Rais Samia kukutana na Tundu Lisu huko Ubeligiji ni dhahiri shahiri sasa uhasama ulio kuwapo kati ya Lisu na Serikali umeisha.

Picha zinaonyesha Lisu akiwa na furaha na tabasamu lisilo kifani mbele ya Rais Samia ni ishara tosha kuwa amemaliza chuki na uhasama.

Sasa ni wakati wa wanachama wote wa Chadema tuunge mkono Serikali hii ya awamu 6 chini ya Amiri Jeshi Mkuu Mama yetu Samia Suluhu Hassa.

Mungu Ibariki Tanzaania.
Lissu hajawahi kuwa na shida na Samia, ilikua ni suala la muda tu. Aliyemfanya Lissu awe nje ya nchi unamjua.
 
Kuweka sawa. Mara ya kwanza alikutana na TL akiwa kwenye kitanda cha maumivu tarehe 28 Novemba 2017, Nairobi Hospital nchini Kenya.
Jana, walikutana Brussels, Ubelgiji.

Tuache siasa pembeni. SSH ameonesha ni binadamu kindaki ndaki.
Tusirithi maadui.
Screenshot_20220217-114842.png
 
Hapa unajiona msomi wa sheria kumbe mjuaji wa KAWAIDA SANA. Tuoneshe point ya mens rea iliyothibidtishwa na seruskali toka kwa Mbowe.

Msg kwamba Mbowe na URIO walichart kwako ndo mens rea inapostand? Au maelezo ya onyo yaliyokanushwa na washtakiwa ndo mens rea ulipoiona?
Mwambie asubiri Judge atakavyoiainisha hiyo kesi kesho tr 18/02/2022.

Cc Kilatha
 
Orodha ni ndefu acha mawasiliano tu

Miamala
Kutafuta watu
Vitendea kazi
And so forth

Tatizo wapelelezi walikuwa na haraka tu ya kumtia hatiani, au mission ilikuwa abandoned wakaona wafungue kesi kwa ushahidi hafifu huo huo walionao.

But clearly the intention to commit a crime was there.

Good Morning
Wewe kiwango chako cha kuelewa mambo ya sheria ni cha Inspector Swila.

Bila bila
 
Kuweka sawa. Mara ya kwanza alikutana na TL akiwa kwenye kitanda cha maumivu tarehe 28 Novemba, Nairobi Hospital nchini Kenya.
Jana, walikutana Brussels, Ubelgiji.

Tuache siasa pembeni. SSH ameonesha ni binadamu kindaki ndaki.
Tusirithi maadui.
View attachment 2121935
Hiki ni kitendo cha kiuungwana mno, kwa hili mama kula TANO za kwangu.

Ni mwanzo mzuri mno wa Lissu kukutana na IKULU ya Tanzania 🇹🇿 kwa mazunguzo; siasa si uadiu kama vile baadhi ya wana CCM walituaminisha.

Kwa aliyopitia Lissu ni haki yake kupata neno fupi la matumaini toka kwa Rais wa nchi.
 
Back
Top Bottom