Ingekuwa ajabu sana asingeonana naye na pengine kila mtu angeshangaa...
Whether we like it or not, na bila kujali udhaifu na mapungufu yake kama binadamu, Rais Samia ndiye kiongozi mkuu wa nchi yetu na kauli yake katika jambo lolote huwa ndiyo ya mwisho. Mungu amjalie na aone ukweli wa mambo upande wa pili yanayotokea ktk nchi yake...
Kitendo cha kuikataa roho mbaya ya chuki na ya kiuaji ya mwendazake John P. Magufuli na kuonana na huyu ndugu uso kwa uso na kuzungumza bila kujali kama ni Tundu Lissu ameomba au Rais mwenyewe ameamua hivyo, ni jambo jema sana na kupongezwa...
This is the new beginning ya CHADEMA. Hopefully pia wakimbizi wote wa kisiasa waliokimbia mdomo wa dictator John P. Magufuli na kukimbilia nchi za kigeni, mlango uko wazi sasa kurejea ktk nchi yao....
Hongera TL, hongereni CHADEMA na hongereni wana harakati wa haki za binadamu na utawala bora wote...