BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Kitendo cha Mh. Mbowe kunyoosha mkono mahakamani tafsiri yake ilikuwa amekubali yaishe ni tofouti na watu wa nje walivyoitafasiri..

Mbona Pasaka anailia nyumbani kwake mwaka huu..
Mbowe hakuomba kesi iishe, bali aiitaarifu Dunia kuwa Serikali ya Tanzania imewanyima chakula washitakiwa wa kesi bambikizi kwa muda miezi 5 mfululizo.
 
Vile mataga watakavyo piga Uturn..haijawahi toke..njaa ya ikiingia kichwani ni hatari kwa uhai wa nchi.

#MaendeleoHayanaChama
 
naona Mama anajaribu kuishi kama JK....good progress..

Angalizo: afahamu tu hawezi kumridhisha kila mtu...
Hii ni afya kwa nchi. Wote ni watanzania ni viongozi na wana wafuasi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia, amekutana na kufanya Mazungu na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tindu Lissu.

Ni baada ya Lissu kuomba kuonana naye.

Walizungumzia mambo mbalimbali kuhusu usitawi wa Tanzania.

Pia, soma

1). Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

2). Tundu Lissu afutiwa kesi zote za uchochezi
View attachment 2121277
View attachment 2121284View attachment 2121285
Safi sana Madam President SSH, safari yako kwenda Brussels isingenoga kama ungalikwepa kukutana na kichwa hiki chenye akili kubwa. Aliyekutangulia katika ofisi yako nyeti aliogopa mno kukabiliana naye na kubadilishana naye mawazo kama ambavyo umefanya wewe.

Licha ya kuwa katika nafasi ya Makamu wa Rais, hukusita kwenda kumtembelea alipokuwa hoi kwenye kitanda cha matibabu pale Nairobi nchini Kenya. Natambua ulikuwa ukiitambua chuki ya bosi wake dhidi yake, lakini katika nyakati hizo za kuogofya ulithubutu kufanya tendo la kiutu kwake.

Natambua unaufahamu uhalifu mkubwa wa kibinadamu na kidemokrasia uliofanywa toka mwaka 2016 mpaka 2021 na mtangulizi wako dhidi ya CDM na makada wake makini. Natambua unaweza kuweka mwanzo mpya na kufanya maridhiano na chama hiki kikuu cha upinzani hapa nchini.

Dhuluma na hujuma zote zilizokwisha kufanyika zinaweza kuwekwa kando na kuchukuliwa kama makovu ya kisiasa. Ni lazima tutangulize maslahi ya taifa letu kwanza, ndipo yafuate maslahi ya vyama vyetu.
 
Wote wamoja, wametoka mbali, wana Bosi mmoja George Soros pure evil.
Masikini Mbowe aidha akubali kuachia Uwenyekiti kwa Makamu au aozee Jela, Samia na Tundu Lisu lao moja!

Shauri zako, acha kujifanya CCM kindakindaki. Mwenyekiti wa ccm kakutana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema kuyajenga, wewe unatultea story za George Soros wa marekani. Tatizo nyie watu wa Chini ndio mnaojifnya kuipenda CCM wakati watoto wakubwa wanapewa uwaziri.
 
Taarifa kutoka Ikulu ya Dar es Salaam

67368840.jpg


Sent from my TECNO LB7 using JamiiForums mobile app
 
Wale waliokuwa wanagomea vikao na serikali hapa nchini wanachanganyikiwa, Lissu level nyingine, anajua maana ya Siasa, tofauti na mburura zilizo hapa nchini. Zitto kabwe alisema mapema, Chadema wakambeza, Sasa Lissu anafata muelekeo wa ZZK, anaachana na Chadema wenye mawazo mgando, ya kizamani, wanaimba katiba tu kama kasuku, mwenzao anaozea jela, wao wanakusanya Hela wanagawana.

Kama nyie wanaume mshambulieni Lissu mitandaoni tuone
Ninadhani wewe ndio mburura haswa. Chadema na Lissu walitaka kupata a negotiated position, siyo msamaha wa Rais ambao hauna justification. Chadema atatoka hapa triumphantly. Judge ataamua kuwa akina Mbowe hawana kesi ya kujibu; Jamhuri ilipeleka mashitaka fake mahakamani. Ushindi kwa Chadema.

Wale wabunge viti maalum wataondolewa Bungeni na kisha Chadema ipeleke walioteuliwa na chama chao kwa mujubu wa sheria. Mwenyekiti wa NEC tayari amekwisha kuondolewa. Ni ushindi kwa Chadema. Yote haya ni payoff ya msimamo wa Chadema; viongozi na wanachama wao. Siasa za heshima hazihitaji easy going, umalaya na kujipendekeza kwa watawala kama alivyotaka Zitto Kabwe.

Umeelewa chinembe?
 
Samia rais wa watu,za chini chini ni kuwa lissu amempigia magoti na kumbembeleza Sana mama Samia amuhurumie Dj Mbowe na ikiwezekana amwachie huru,keep calm wafuasi wa Mbowe huenda wakatabasamu this week.
Baba yako ndiye aliyembambikizia kesi?
Hopeless.
 
Hiii habari chungu sana kwa Bavicha
Mkuu hivi unajua kusoma?
Taarifa ya Ikulu inasema Samia amekutana na Lissu nchini ubelgiji baada ya kuombwa na Lissu akutane naye.

Kwa kukusaidia tu, fahamu haya:
1. Wito wa kukutana uliletwa na CHADEMA kupitia Lissu.
2. Mkutano umefanyika Ubelgiji mahali anapoishi sasa Lissu.

Sasa tukuulize, BAVICHA wataumiaje kwa hili tukio wakati msingi wake umeanzia CHADEMA na umehitimishwa ndani ya CHADEMA?
 
Mbowe hakuomba kesi iishe, bali aiitaarifu Dunia kuwa Serikali ya Tanzania imewanyima chakula washitakiwa wa kesi bambikizi kwa muda miezi 5 mfululizo.
Ile lugha iliyotumika pale ni watu wachache waliielewa, huoni baada ya kunyoosha mkono kesho yake serikali iliona hakuna haja ya kuleta mashahidi wengine.

Mbowe alikubali kosa hivyo serikali imeona haina haja ya kuendelea kumshtaki, hivyo hivi karibuni anatoka mahabusu.
 
Sasaa hivi Lissu ataitwa msaliti
Hivi kwa akili yako hapo aliyeshinda ni nani? CHADEMA siku zote dhumuni lao ni kuongea na Rais na siyo msaidizi atakayepindisha baadhi ya maneno. Mkutano wa vyama vya siasa walisema wazi Samia aende kama mshiriki na siyo mgeni rasmi mkamzuia.
 
Moja ya jambo moja muhimu sana kwa Rais kufanya! Hata katika hali ya kibinadamu SSH alimtembelea Lissu hospitali Nairobi. On a personal level angependa kuona yule aliyemtembelea hospital ana hali gani baada ya siku nyingi.

Kuna chuki itakuja kutoka upande mmoja dhidi ya Rais wakidhani huu ni udhaifu. La hasha, this is strength!
 
Ninadhani wewe ndio mburura haswa. Chadema na Lissu walitaka kupata a negotiated position, siyo msamaha wa Rais ambao hauna justification. Chadema atatoka hapa triumphantly. Judge ataamua kuwa hakina hawana kesi ya kujibu; Jamhuri ilipeleka mashitaka fake mahakamani. Ushindi kwa Chadema. Wale wabunge viti maalum wataondolewa Bungeni na kisha Chadema ipeleke walioteuliwa na chama chao kwa mujubu wa sheria. Mwenyekiti wa NEC tayari amekwisha kuondolewa. Yote haya ni payoff ya msimamo wa Chadema; viongozi na wanachama wao. Siasa za heshima hazihitaji easy going na kujipendekeza kwa watawala kama alivyotaka Zitto Kabwe.
Umeelewa chinembe?
Jaji hatatoa uamuzi, mwanasheria wa serikali ataondoa shauri kabla ya uamuzi, mmekula sana Hela zetu kwa kisingizio Cha kumchangia Mbowe, Maria Sarungi ana mabilioni kayaficha kwa kisingizio anakusanya Hela za Mbowe za kesi
 
Back
Top Bottom