Tetesi: Bunge Kuwaka Moto hadi Zanzibar ijadiliwe kwa Dharula

YEHODAYA mbona huna akili kiasi hiki

Amiri mkuu wa Tanzania ni MMOJA TU ambaye ni Rais wa Jamhuri

Rais wa Zanzibar hana jeshi lolote isipokuwa KKKM...Ambalo sio jeshi bali kikosi cha kuzuia magendo

Ficha Upumbavu wako
 
Wanataka tu kupoteza muda na fedha na kujipatia ujiko wa kisiasa,ukawa hawana tena ajenda ya ufisadi,wamehamia zanzibar.
Bunge la muungano halina mamlaka ya kumtangaza rais wa zanzibar wala kuamuru uchaguzi urudiwe.Ni ZEC tu mwenye mamlaka,tutazunguka wee mwisho tutarudi kwa jecha.
Hicho kikao kitakua kama cha harusi tu,maamuzi hayatakua na impact yoyote.
Maalim awaandae wafuasi tu kumpigia kura tena anaogopa nini kama hakuiba?
 
YEHODAYA mbona huna akili kiasi hiki

Amiri mkuu wa Tanzania ni MMOJA TU ambaye ni Rais wa Jamhuri

Rais wa Zanzibar hana jeshi lolote isipokuwa KKKM...Ambalo sio jeshi bali kikosi cha kuzuia magendo

Ficha Upumbavu wako
Labda kwa vile anaona KMKM na MAFUNZO wanachezza gwaride basi kwake hayo ni majeshi!
Mbona chipukizi wa ccm na Green guards nao wanacheza gwaride kwani nao ni majeshi? Usalama na amani ya Zanzibar viko chini ya serikali ya muungano ndio maana hata Kenya au yeyote akivamia sehemu yeyote ya visiwa hivyo ndio mtauona moto wa Magufuli na Mwamunyange kwa vile wameigusa TZ
 


Uwa nikimsikiliza yule makamu wa pili wa SMZ natamani hata kutapika...uje umsikie katibu msaidizi wa CCM Zenji ndio utatamani kufa kabisa. Yani hawa watu wana kiburi cha uzima, ni walafi wa madaraka bila kujali maisha ya watu Wazanzibar. Nawaunga mkono wabunge watakaosimama kidete kujenga hoja makini juu ya hili. Hakuna mtu yeyote ndani ya CCM akatakayeweza kulimaliza hili, hata Pombe mwenyewe anajua kuna lipi nyuma ya pazia.
 
Nikuulize swali

Inakuwaje siku ya matokeo ya uchaguzi jeshi la jamuhuri ya muungano kuvamia eneo la bwawani na kumchukua mwenyekiti wa uchaguzi akafute uchaguzi? Jee huioni ya kwamba mumeingilia na kuuvuruga uchaguzi ulio huru?

Nani alie ivuruga amani? Hutoweza kunipa majibu nikakuelewa
 
Kuna haja gani ya sisi kujiita watanzania?
 
Kwa hiyo bunge linaichukua hiyo kazi?
Kwani kujadili ndiyo kuchukua kazi ya Tume .............!!? Tume yenyewe imeshindwa mpaka leo kutueleza kinachoendelea ....... inaelekea Jecha bado yuko mafichoni!!
 

Hili lingeandikwa na Jingalao nisingeshangaa kutokana na jina lenyewe, leo mnasema nyie watanganyika kwa vile tu kuna wanzanzibari kesho wazanzibari wakiondoka mtasema nyie wanyakyusa au wasukuma
 

Aliyevuruga Uchaguzi ni Seif Hamad ALIYEJITANGAZA kuwa mshindi wa uraisi bila kutangazwa na tume na kabla ya matokeo kukamilika hivyo kuleta taharuki ya usalama hivyo kusababisha ulinzi uongezwe kila mahali ikwemo kwa mkurugenzi wa ZEC Kwa ajili ya usalama wake.Kujitangaza kule ilikuwa ni uhaini hivyo wanajeshi kuingia barabarani kulinda raia na mali zao baada ya mhaini Seif KUJITANGAZA ILIKUWA NI SAHIHI.

Na utakubaliana nami kuwa baada ya mhaini kujitangaza wanajeshi walikuwa maeneo yote ya Zanzibar si Bwawani tu.
 

Gentleman u must be fcked up

Swala la Ufisadi sio la kupiga Porojo...wewe subiri wabunge wa UKAWA watakavyoibeba hiyo Hoja....Hakuna haja ya kelele nyingi

CCM ndio wezi wakuu nchi hii...ndio walezi wakuu wa wizi wa nchi hii....
 
huna lolote .
 
Wabunge kutoka Zanzibar wanahudhuria bunge na walishaapishwa. Kilichobaki ni kile kinachohusu Zanzibar kama nchi. Maadam Tanzania ina serikali na mambo yanaenda hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na issue ya serikali ya Zanzibar. Unless useme kuna maslahi ya kisiasa kama ilivokuwa ule msiba wa mawazo. Kikatiba mnaweza kujadili na kila mbunge wa ukawa anapewa nafasi ya kuongea lakini kiuhalisia mtakuwa mnavunja katiba na kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar. Na chochote mtakachoamua hakina uhalali wa kutumika Zanzibar. Ingekuwa unaongelea issue ya Zanzibar kama Mkoa sawa na mtwara hapo ungeeleweka. Lakini ukiongelea Zanzibar kama nchi huna haki ya kujadili mambo yasiyo ya muungano kwenye bunge la muungano. Mind you this. Halafu hakuna alieapishwa kule wala hakuna aliepewa ushindi na wala hakuna alietangazwa mshindi na zaidi sana hakuna vurugu wala vita. Watu wanaongelea kuhusu kurudia uchaguzi au la. Sasa kufanya vurugu kwenye bunge la muungano ni kuhamasisha vurugu. Ni uchochezi. Ni ujinga na ni siasa za kipumbavu. Mbona wao wa zanzibar hawaongelei issue ya kafulila kudai kaibiwa ubunge wake. Mi naona siasa ni mchezo mbaya ambao lengo lake ni kunufaisha wachache. Ukawa wakifanya vurugu watatolewa bungeni na bunge litaendelea na miswada kibao itapitishwa. Yaan ikifika apo utaona kuwa hakukuwa na haja ya kuwapigia kura wabunge wa ukawa kama tulikuwa na uhakika kuwa lowasa hawezi kushinda Urais. Kuna tofauti kati ya mawazo ya watu na sheria inavosema. Ni hivi. Nchi huwa haziongozwi na mawazo tu ya watu. Watu wamelala na mahawala zao uko then tuamke asubuhi tusikie sheria imebadilika. Tunaongozwa na sheria na ili kubadilisha kuna taratibu zake. Wabunge wa ukawa wanatakiwa wawe makin katika hayo na mengine makubwa sio kufanya vurugu kwa sabb za kipuuzi ambazo hata kisheria hazikubaliki. Tutabaki nyuma mpaka lini. Inamaana hata matendo yetu tutatenda kwa kuwanufaisha akina lowasa. Hatuwawazii kabisa maskini wanaopata shida ya maji na Chakula wanakula mlo mmoja kwa siku
 
Mhaini na bado yuko mtaani? Wadanganye watoto. Seif hakujitangaza mshindi kataja kura zake kulingana na fomu za mawakala zilizo sainiwa na anazo mkononi. Sasa Jecha hilo lingeweza kumzuia asitangaze zake?
Hivi Hamadi angekuwa ni yeye katangaza kura zake 600 alizopata Uchaguzi ungefutwa? Au Seif angekuwa kapata kura 30% akazitangaza Uchaguzi ungefutwa?
 
Siwezi kukubaliana na wewe, ikiwa maalim kajitangaza mshindi kutokana na hati miliki zilizo tolewa kila kituo cha kupiga kura na kusainiwa na mawakala wa tume ya uchaguzi na kubandikwa katika vituo.

Hoja ya Jecha ya kufuta uchaguzi sio maalim kutangaza ushindi, labda urudie tena kumsikiliza ipo video yake youtube.

Maalim aliongea na waandishi wa habari 26 October na tarehe 28 Oct ndio uchaguzi umefutwa, kama kunatokea hitilafu zozote katika vituo vya kupiga kura, kuna form za malalamiko zipo na CCM hawakutoa mpaka siku ya 28 Oct uchaguzi unafutwa na Jecha.

Kisheria hana mamlaka ya kufuta uchaguzi, na JWTZ chini ya Jk limeshiriki kikamilifu kupindua demokrasia
 
Tatizo ni balozi Idd maana anajua muafaka ukipatikana hana kazi. Ndiyo maana wakikaa kikao yeye anawahi waandishi kuropoka kwamba uchaguzi upo.
Wabunge itapendeza sana kama mtaiwajibisha Serikali kueousha machafuko Zanzibar.
 
Seif hakujitangaza mshindi kataja kura zake kulingana na fomu za mawakala zilizo sainiwa na anazo mkononi. Sasa Jecha hilo lingeweza kumzuia asitangaze zake?
Kuna kitu hujijui kuhusu sheria ya uchaguzi.Kazi ya tume ni pamoja na kujumlisha matokeo.Huwezi kulala na hawara yako kitandani ukachukua matokeo toka vituoni na kuanza kujijumlishia na hawara yako halafu uende kutangaza kuwa kwa mujibu wangu na hawara yangu matokeo tuliyojumlisha ni haya! Tume itoe ya kwao ilinganishe na yale tulliyojumlisha kitandani na hawara yangu!!!!!! Tume ndie mjumlishaji pekee anayetambulika kisheria sio MHaini SEIF au mtu mwingine yeyote.

Tume ingetoa yake kwanza ndipo kama ana dispute yeye ndie alinganishe matokeo yake na ya tume sio tume ilinganishe matokeo yake na Yale ya Seif SHARRIF HAMAD.Mgombea hawezi kuwa yeye mpigiwa kura,mhesabu kura na mjitangaza mwenyewe kama mshindi ndicho Seif ALICHOFANYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…