Km nilazima Serikali ya Mapinduzi iwepo Nikwanini pia TANGANYIKA icwepo! kwanini nyie watu wa CCM mnatufanya km Watt wadogo,,!
Hili si tatizo kwani ndivyo sheria inavyotaka na ndivyo utaratibu uliokubaliwa. Kama walio wengi Bungeni wataamua kufanyia marekebisho vipengele vyovyote vya rasimu na ikaitwa kura na wakashinda basi vipengele hivyo vitakuwa katika Katiba Inayopendekezwa. Kama wananchi hawatakubaliana nayo basi wataikataa kwenye kura ya maoni.
Kwa hiyo maoni yote ya wananchi ni changa la macho?
Acha kupotosha we Mzee, kwa maana hiyo kulikuwa na maana gani ya sisi kutoa maoni yetu?
Akili zikizidi sana zinageuka kuwa hasara.
Maoni si yalikuwa ni maoni tu? Kwani sheria ilisema maoni ni lazima yakubaliwe? Hata kama maoni yalitolewa na watu wengi sheria haisemi maoni hayo ni lazima yakubaliwe! Yalikuwa ni maoni tu na mapendekezo. Yanaweza kukataliwa...
Wakipitisha katiba isiyokidhi viwango basi haitadumu itabadilishwa tena ndani ya miaka kumi.
Mimi hata ije rasimu ingine bora tu iweke mbele maslahi ya nchi na haki ya mtanzania mmojamoja ipatikane.
Mkuu sijakupata vyeka unaposema Bunge la Katiba na Bunge la siku zote yapo sawa kwa kuwa yanatunga sheria. Lakini pia unasema hili Maalum linatunga sheria ambayo inaitwa Katiba. Kama ndivyo na unaikubali dhana ya Constitutional supremacy na kwamba sheria yoyote itakayotungwa na chombo chochote itakuwa batili kama itakinzana na Katiba (ambayo imetungwa na bunge maalumu) basi ukuu huu wa katiba unaipa ukuu pia Bunge la Katiba dhidi ya Bunge pa kawaida.
Hatua tuliyofikia ni
1:CCM wapitishe Rasimu yao kinyume na matakwa ya umma
2:Tusiwe na katiba mpya- Hii ni kwa sababu wanajua wakipitisha rasimu yao ni ama ikubaliwe au ikataliwe na hivyo tuendelee na katiba ya sasa
CCM hawataki katiba mpya sasa
Mkuu rasimu ikitoka bungeni, lazima ipitishwe na kura za wananchi!
Wananchi wakiikataa, rasimu inarudi bungeni kwa mara ya pili, na hapo ikikataliwa tena na wananchi, TUNATUMIA KATIBA HII HII TUNAYOTUMIA SASA!
Maoni si yalikuwa ni maoni tu? Kwani sheria ilisema maoni ni lazima yakubaliwe? Hata kama maoni yalitolewa na watu wengi sheria haisemi maoni hayo ni lazima yakubaliwe! Yalikuwa ni maoni tu na mapendekezo. Yanaweza kukataliwa...
Wewe kwa mawazo yako unaona watanzania wana ujasiri kweli wa kupiga kura ya hapana? inshort imekula kwetu.
I am trying to make sense of what you wrote, but I am not getting it. What exactly did you want to say?
Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa hii!. Naomba nikiri sasa nimeanza tena kumuona Mzee Mwakijiji yulee niliyemfahamu wakati nilipojiunga JF!, yule Mzee Mwanakijiji wa KLH News!, Mzee Mwakijiji wa "Cheche za Fikra!", ndio huyu Mwanakijiji wa leo!, ambaye amekuja na ukweli halisi as it is, not as it ought to be!, no matter ni mchungu kiasi gani kumeza, kilichopakuliwa ndicho hiki, watu wameze, wateme ni shauri yao ukweli huu ndio utasimama!.Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.
Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.
Well.. habari ndiyo hiyo...
Umenipata vyema. Nilikuwa nakumbusha tu ukuu wa bunge lolote kutunga sheria, dhidi ya chombo chochote ambacho si bunge. Warioba naTume ya Katiba wanataka ukuu huo usiwepo. Lakini wazo kuwa bunge la aina moja ni juu ya lingine si lazima kimantiki, kinadharia na ki-uzoefu. Muhimu ni ukuu wa baraza la kutunga sheria. Naongezea kuwa ukuu wa Katiba unaozungumzwa mara nyingi haufikii ukuu wa Bunge. Ndiyo maana Waingereza hawautambui. Badala yake wanatambua parliamentary supremacy, lakini huu uwe mjadala mwingine.
Maoni si yalikuwa ni maoni tu? Kwani sheria ilisema maoni ni lazima yakubaliwe? Hata kama maoni yalitolewa na watu wengi sheria haisemi maoni hayo ni lazima yakubaliwe! Yalikuwa ni maoni tu na mapendekezo. Yanaweza kukataliwa...
Hatua tuliyofikia ni
1:CCM wapitishe Rasimu yao kinyume na matakwa ya umma
2:Tusiwe na katiba mpya- Hii ni kwa sababu wanajua wakipitisha rasimu yao ni ama ikubaliwe au ikataliwe na hivyo tuendelee na katiba ya sasa
CCM hawataki katiba mpya sasa