Bunge Live larudi. Kuoneshwa kuanzia Aprili 5, 2022 katika mkutano wa saba wa Bunge la Bajeti

Bunge Live larudi. Kuoneshwa kuanzia Aprili 5, 2022 katika mkutano wa saba wa Bunge la Bajeti

kilio chenu kimesikika bado mmeanza kuleta sababu zingine yaani akili zenu mnazijuwa wenyewe ni sawa na demu unaingia naye mpaka gest halafu anakuuliza humu tunakuja kufanya nini?
Kawadanganye mazuzu wenzako
 
hata mkipewa katiba mpya mtakuja na lingine maana hamueleweki kabisa nyie bora tuwapuuze tu
Wewe ni sawa na sisimizi tu kwenye maamuzi ya wanao dai katiba mpya.
 
yaani nyie hamnaga hoja za maana zinazowahusu wananchi wa hali ya nchini mnachojali ni siasa ambazo wengi haziwasaidii sana bei ya vitu kupanda siyo agenda yenu maisha bora kwa mtanzania siyo agenda yenu mnacho haha nacho ni katiba mpya ambayo haileti unafuu wa maisha kwa mtanzania zaidi ya uchiu wenu wa madaraka tu
Pumbaf
 
Bunge halina mvuto afadhali kuangalia tamthilia za kilkorea
 
Mbunge la kuunga hoja na kupiga makofi tu.
Upuuuz mtupu,
 
kilio chenu kimesikika bado mmeanza kuleta sababu zingine yaani akili zenu mnazijuwa wenyewe ni sawa na demu unaingia naye mpaka gest halafu anakuuliza humu tunakuja kufanya nini?

Hilo sio bunge Ni kikao Cha CCM kupitisha matakwa yao. Spika alishasema Rais ana Uhuru wa kukubali au kukataa ushauri wa Bunge.
 
Sawa bunge live ndiyo kilio cha Chadema.
Kupanda bei vitu na kukatika umeme siyo jambo la maana sana kwao

Kilio cha cdm kutazama bunge la majizi ya kura? Uko usingizini ww.
 
Sawa bunge live ndiyo kilio cha Chadema.
Kupanda bei vitu na kukatika umeme siyo jambo la maana sana kwao
Ceremonial Parliament nani anataka hata kusikiliza?. Labda wafia Kijani kama wewe..
 
mfukuzeni kwanza yule mbunge wenu wa nkasi ndiyo mseme kuwa hakuna wapinzani bungeni la sivyo mnapayuka tu
Afukuzwe kwani kuna hata anayetambua kama yuko bungeni?
 
Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vitaanza kurushwa live. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge. Ndg. Nenelwa Mwihambi.

Nenelwa amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 05 Aprili 2022 wakati Mkutano wa Saba wa Bunge mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali utakapoanza Bungeni Jijini Dodoma.

Januari mwaka 2016, waziri wa habari wa wakati huo, Nape Nnauye alitoa tangazo bungeni la kusitisha matangazo ya Bunge ya moja kwa moja akitoa sababu ya kupanda kwa gharama kwenye shirika la utangazi la Taifa(TBC) zilizofikia bilioni 4.2 kwa mwaka.

Nape alisema TBC ilikuwa ikigharamia matangazo ya Bunge kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato kama matangazo madogo ya kibiashara. TBC katika kupunguza gharama na kubana matumizi ikaona busara kurusha baadhi ya matangazo live na mengine kurekodiwa kisha kurushwa kwenye kipindi maalum usiku ambayo ingewapa pia fursa watanzania walio wengi kwani mchana huwa wana kazi za kiofisi au ujenzi wa Taifa.

PIA, Soma=>TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Ni upotevu wa pesa ya wananchi. Wanajiita wabunge wakati hakuna aliyewachagua.

Nani ana hamu ya kuwasikia??
 
Tanzania ina maajabu eti kwa sasa anayetoa hoja kinzani ndio akina msukuma.
 
CCM na ACT wazalendo wameshirikiana kuunda serikali.

Wabunge 20 hawajulikani wako chama gani kwani kule wanakodai wao ni wanachama wamekataliwa

Mbunge wa upinzani ni mmoja tu, mwanamama kutoka CUF Ntwara.

Bunge la namna hii ni sawa kabisa na bunge la chama kimoja kwa sababu litakuwa linatekeleza ilani ya CCM na hakuna namna yoyote ile ya kulikemea itakayobadilisha " chochote"

Wakati wa Mwalimu Nyerere RTD ilitumika sana kutoa elimu ya Kilimo cha kisasa nadhani TBC hiyo kodi ya kurusha bunge live waipeleke kwenye makala za kilimo labda na teknolojia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Naunga mkono hoja mkuu, atakayekaa kulitizama bunge la safar hii akili yake itakuwa haiko sawa.
 
Bunge live ni jambo jema kwani haya mambo ya kumsifiasifia Kiongozi na kulazimisha apendwe linachosha sana.
Sasa ili kuondoa hiyo hulka ni kujua matumizi ya fedha alizokopa ni kiasi gani na alitumia vipi ili watanzania wote tujue na kuangalia je anastahili hizo sifa
 
Back
Top Bottom