Bunge Live larudi. Kuoneshwa kuanzia Aprili 5, 2022 katika mkutano wa saba wa Bunge la Bajeti

Bunge Live larudi. Kuoneshwa kuanzia Aprili 5, 2022 katika mkutano wa saba wa Bunge la Bajeti

Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vitaanza kurushwa live. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge. Ndg. Nenelwa Mwihambi.

Nenelwa amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 05 Aprili 2022 wakati Mkutano wa Saba wa Bunge mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali utakapoanza Bungeni Jijini Dodoma.

Januari mwaka 2016, waziri wa habari wa wakati huo, Nape Nnauye alitoa tangazo bungeni la kusitisha matangazo ya Bunge ya moja kwa moja akitoa sababu ya kupanda kwa gharama kwenye shirika la utangazi la Taifa(TBC) zilizofikia bilioni 4.2 kwa mwaka.

Nape alisema TBC ilikuwa ikigharamia matangazo ya Bunge kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato kama matangazo madogo ya kibiashara. TBC katika kupunguza gharama na kubana matumizi ikaona busara kurusha baadhi ya matangazo live na mengine kurekodiwa kisha kurushwa kwenye kipindi maalum usiku ambayo ingewapa pia fursa watanzania walio wengi kwani mchana huwa wana kazi za kiofisi au ujenzi wa Taifa.

PIA, Soma=>TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Bunge live la praise and worship litaisaidia nini nchi yetu?
 
Wananchi walipiga sana kelele kuhusu Bunge kuwa live lakini hata Wahe. Mawaziri wa Awamu ya Tano walikuwa waoga sana kwa mkubwa wao.
 
Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho Jumanne Aprili 5, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo Jumatatu Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, amesema bunge live litaanza kesho katika mkutano wa saba wa bunge la bajeti.

Huu ni muendelezo wa Rais Samia kufuta kero nyingi zilizokuwa zikisemwa saana hususan na vyama vya upinzani. Baada ya ,uda watakuwa hawana la kuongea ukiachana na hilo la KATIBA MPYA ambalo Rais Samia amesema wazi kwamba lisubiri na kuna kila dalili litafanyika katika awamu yake ya pili ya uongozi.

maxresdefault (3).jpg
 
yaani nyie hamnaga hoja za maana zinazowahusu wananchi wa hali ya nchini mnachojali ni siasa ambazo wengi haziwasaidii sana bei ya vitu kupanda siyo agenda yenu maisha bora kwa mtanzania siyo agenda yenu mnacho haha nacho ni katiba mpya ambayo haileti unafuu wa maisha kwa mtanzania zaidi ya uchiu wenu wa madaraka tu
Una akili ndogo sana, katiba inasema wananchi kupitia bunge wakiipinga bajeti ya serikali kuu, bunge linavunjwa. Sasa hata Chadema wapinge vipi mfumuko wa bei au bunge live lijadili mapendekezo ya bajeti mwisho wa siku itapitishwa tu maana mkipinga bunge litavunjwa.

Sasa kwa staili hiyo unadhani katiba ya sasa itajibu kiu ya mfumuko wa bei??

Ndio maana CHADEMA wanapropose katiba mpya maana itaongeza meno ya bunge, ufanisi wa vyama vya siasa kuisimamia serikali, na kuongeza uwajibikaji maana hata wananchi wanaweza kumng'oa mbunge kama asipofikisha kero zao ikiwemo "mfumuko wa bei"

Bado hauoni faida yake?
 
Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vitaanza kurushwa live. Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge. Ndg. Nenelwa Mwihambi.

Nenelwa amesema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge na Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 05 Aprili 2022 wakati Mkutano wa Saba wa Bunge mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali utakapoanza Bungeni Jijini Dodoma.

Januari mwaka 2016, waziri wa habari wa wakati huo, Nape Nnauye alitoa tangazo bungeni la kusitisha matangazo ya Bunge ya moja kwa moja akitoa sababu ya kupanda kwa gharama kwenye shirika la utangazi la Taifa(TBC) zilizofikia bilioni 4.2 kwa mwaka.

Nape alisema TBC ilikuwa ikigharamia matangazo ya Bunge kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato kama matangazo madogo ya kibiashara. TBC katika kupunguza gharama na kubana matumizi ikaona busara kurusha baadhi ya matangazo live na mengine kurekodiwa kisha kurushwa kwenye kipindi maalum usiku ambayo ingewapa pia fursa watanzania walio wengi kwani mchana huwa wana kazi za kiofisi au ujenzi wa Taifa.

PIA, Soma=>TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Pigo jingine kwa sukuma gang.
 
Sawa bunge live ndiyo kilio cha Chadema.
Kupanda bei vitu na kukatika umeme siyo jambo la maana sana kwao
Ukiambiwa huna akili unaanza kulialia wakati huna akili.

Kwani cdm ndiyo wanao umia pekee yao kwa tatizo la upandaji wa bei ya mahitaji ya wananchi?
 
Wanaenda kuonyesha live kikao cha CCM ambapo kila mbunge wa CCM atakua anasimama na kumpongeza rais.
 
Hii nchi ina unafiki sana, na hili atasingiziwa JPM kwamba ndo alizuia, kumbe waliozuia wapo humohumo ndo wananafikia sasa!!
Aliyelizuia bunge kurushwa live ni Jiwe na hilo halina ubishi.

Na kwa kuruhusiwa kurushwa live tena ni pigo kubwa kwa sukuma gang.
 
Back
Top Bottom