Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah nayo sheria sasa.Ndio
JK kanuna
Lowasa na Sumaye wametajwa
Mkuu Jk, Mkapa hawajatabasamu hata kidogo.
Wale wabunge wakususia Leo hawajatoka??Leo tarehe 16 Juni 2020, Rais Magufuli analivunja bunge kwa ajili ya kufanya matayarisho ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, ambapo uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika kwa wakati mmoja.
Bunge la 11 lilifunguliwa na Rais Magufuli Novemba 20, 2015 baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tutawaletea kile kinachojiri kutoka bungeni.
FUATILIA:
UPDATES:
Marais Wastaafu, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu Dr Gharib Bilal wakiwa Bungeni mjini Dodoma wakisubiri kusikia hotuba ya kulivunja Bunge Leo kutoka kwa kwa Rais Dk John Magufuli
09:24am - Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wameshafika katika Ukumbi wa Bunge na pia wapo Viongozi wa zamani
09:36 Rais Magufuli awasili kwenye viwanja vya Bunge, akaribishwa kwa Wimbo wa Taifa na kukagua Gwaride Maalum
09:49 Rais Magufuli aingia Bungeni kusaini kitabu cha wageni
10: 00 Rais Magufuli aingia katika ukumbi wa Bunge
10: 10 Spika wa Bunge asema Miswada 60 imepitishwa kuwa sheria katika Bunge la 11
10: 13 Spika amkaribisha Rais kuhutubia Bunge
10:14 Rais aanza kulihutubia Bunge
Rais alitaka Bunge kusimama kuwakubuka wabunge na waliptangulia mbele za haki.
Ashukuru uwepo wa marais na viongozi wastaafu wakiwemo Lowassa na Sumaye na kusema
“Kwa wakati nikizindua Bunge hili nilieleza mipango mingi na ninashukuru tumeweza kuitekeleza”
“Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita tumetimiza wajibu wetu kwa kiasi kikubwa”
“Watangulizi wangu waliweka misingi imara iliyowezesha kufikia mafanikio tuliyopata kwa miaka 5 iliyopita…ushauri wao umenisaidi kwa kiasi kikubwa”
“Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha Amani na mipaka yetu imeendelea kuwa salama. Kama tunakumbuka, tulikuwa na wimbi la uhalifu wa kutumia silaha huko Kibiti lakini tulifanikiwa kudhibiti”
Mkuu anasoma hotuba hicho kioo unachokiona mbele yake kinaitwa teleprompter ye anaona hotuba pale anasoma walioko nyuma hawaoni hebu tazama macho yake muda wote yametazama hicho kiooNacheki hapa Mkulu akitoa hotuba ya kufunga Bunge. Najaribu kuangalia kwa umakini hizi takwimu anatema kama anasoma mahali,sioni kwa kweli au ni mimi tu?Mr President ni hatari kwenye kumeza maandishi walah..makofi kwake tafadhali.
Unaona hicho kiio kimewekwa hapo mbele yake .... kina kazi yake ..wacha kukurupukaNacheki hapa Mkulu akitoa hotuba ya kufunga Bunge. Najaribu kuangalia kwa umakini hizi takwimu anatema kama anasoma mahali,sioni kwa kweli au ni mimi tu?Mr President ni hatari kwenye kumeza maandishi walah..makofi kwake tafadhali.