Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa

Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa

Leo tarehe 16 Juni 2020, Rais Magufuli analivunja bunge kwa ajili ya kufanya matayarisho ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, ambapo uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika kwa wakati mmoja.

Bunge la 11 lilifunguliwa na Rais Magufuli Novemba 20, 2015 baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutawaletea kile kinachojiri kutoka bungeni.

FUATILIA:

UPDATES:
Marais Wastaafu, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu Dr Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu Dr Gharib Bilal wakiwa Bungeni mjini Dodoma wakisubiri kusikia hotuba ya kulivunja Bunge Leo kutoka kwa kwa Rais Dk John Magufuli

09:24am - Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar wameshafika katika Ukumbi wa Bunge na pia wapo Viongozi wa zamani

09:36 Rais Magufuli awasili kwenye viwanja vya Bunge, akaribishwa kwa Wimbo wa Taifa na kukagua Gwaride Maalum

09:49 Rais Magufuli aingia Bungeni kusaini kitabu cha wageni

10: 00 Rais Magufuli aingia katika ukumbi wa Bunge

10: 10 Spika wa Bunge asema Miswada 60 imepitishwa kuwa sheria katika Bunge la 11

10: 13 Spika amkaribisha Rais kuhutubia Bunge

10:14 Rais aanza kulihutubia Bunge

Rais alitaka Bunge kusimama kuwakubuka wabunge na waliptangulia mbele za haki.

Ashukuru uwepo wa marais na viongozi wastaafu wakiwemo Lowassa na Sumaye na kusema

“Kwa wakati nikizindua Bunge hili nilieleza mipango mingi na ninashukuru tumeweza kuitekeleza”

“Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita tumetimiza wajibu wetu kwa kiasi kikubwa”

“Watangulizi wangu waliweka misingi imara iliyowezesha kufikia mafanikio tuliyopata kwa miaka 5 iliyopita…ushauri wao umenisaidi kwa kiasi kikubwa”

“Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha Amani na mipaka yetu imeendelea kuwa salama. Kama tunakumbuka, tulikuwa na wimbi la uhalifu wa kutumia silaha huko Kibiti lakini tulifanikiwa kudhibiti”
Wale wabunge wakususia Leo hawajatoka??
 
Nacheki hapa Mkulu akitoa hotuba ya kufunga Bunge. Najaribu kuangalia kwa umakini hizi takwimu anatema kama anasoma mahali,sioni kwa kweli au ni mimi tu?Mr President ni hatari kwenye kumeza maandishi walah..makofi kwake tafadhali.
 
Wizara zinatakiwa ziingizwe kwenye katiba ili mtu asije kujiamlia tu na kutunga Wizara
 
Nacheki hapa Mkulu akitoa hotuba ya kufunga Bunge. Najaribu kuangalia kwa umakini hizi takwimu anatema kama anasoma mahali,sioni kwa kweli au ni mimi tu?Mr President ni hatari kwenye kumeza maandishi walah..makofi kwake tafadhali.
Mkuu anasoma hotuba hicho kioo unachokiona mbele yake kinaitwa teleprompter ye anaona hotuba pale anasoma walioko nyuma hawaoni hebu tazama macho yake muda wote yametazama hicho kioo
1.jpg
2.jpg
 
Huyo ni geneus mkuu alizoea kumeza equations za chemia na physics aje ashindwe kumeza propaganda za siasa kweli..

#the best president in Africa.. viva JPM
 
Nacheki hapa Mkulu akitoa hotuba ya kufunga Bunge. Najaribu kuangalia kwa umakini hizi takwimu anatema kama anasoma mahali,sioni kwa kweli au ni mimi tu?Mr President ni hatari kwenye kumeza maandishi walah..makofi kwake tafadhali.
Unaona hicho kiio kimewekwa hapo mbele yake .... kina kazi yake ..wacha kukurupuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom