Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia

Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia

Chademaa wazee wa drama ilimradi wawe relevant tuu.
 
K
Kweli chadema ina watu wajinga sana!

Yani Malisa nae kajiunga na kigogo kumuita Halima mzee?

Historia inaonesha kwamba pale chadema kila mtu huwa anasurubiwa kwa wakati wake kulingana na nyakati!

Zitto pamoja na kupigana hadi jasho la damu lakini lilipokuja suala la maslahi ya Mbowe alikiona cha moto

Slaa pamoja na kuvunjika hadi mikono akipigania chadema lakini lilipokuja suala la maslahi ya Mbowe alikiona cha moto.

Sasa hivi ni zamu ya Mdee!

Huyu Malisa ni kidagaa tu pale chadema, ningekuwa mimi ningejikalia kimya tu bila kumkejeli Halima.
Kama haujapanic basi una kaugonjwa kanakotibiwa Mirembe, yaani katika hoja yote aliyojenga Malisa wewe umeona kumuita Halima mzee Halima tu basi?
 
Chadema ni imani nimekuelewa sana
2017, CCM ilimfukuza Sophia Simba (akiwa mwenyekiti wa UWT na mbunge wa VM) kwa tuhuma zikiwepo kumuunga mkono Edward Lowassa (aliyehamia CCM wakati huo). Lakini Ndugai hakusimama kusema CCM hii ya Magufuli inawanyanyasa wanawake. Ikawasamehe wanaume na kumpa adhabu mwanamke.
 
Ndungai na wana ccm wenzake inatosha tu kusema ni viumbe wa hovyo haijawahi kutokea.
 
Bwana Ndugai anahitaji msaada wa haraka wa saikolojia.

Malisa GJ

Mosi; Huu uchungu anaouonesha Ndugai sio wa Mzee Halima na wenzake kupigwa, ni uchungu wa kupoteza yale matrilioni ya wafadhili. Ameshaona dalili zote kwamba hata akiwalinda akina Mzee Halima na wenzake waendelee kuwa wabunge, wafadhili wanaweza kugomea kutoa yale matrilioni.

Pili; Mzee Halima na wenzake hawakupigwa kwa ajili ya Mbowe. Walipigwa kwa sababu ya kutetea haki zao. Walipotolewa Segerea askari magereza waliwapiga kama vibaka kwa sababu tu walienda kupokelewa na wafuasi wao. Mashinji alipokelewa na msafara wa wafuasi wa CCM wakiongozwa na Chakubanga lakini hakupigwa. Double standards. Kama kweli Ndugai ana uchungu angewakemea wale askari waliofanya unyama ule sio Mbowe.

Tatu; Mzee Halima na wenzake hawajafukuzwa bila kusikilizwa. Walipewa haki ya kusikilizwa (audi alteram partem) lakini wakakataa kuitumia. Waliitwa kwa maandishi kwenye kamati kuu ili wasikilizwe wakagoma. Sasa Bwana Ndugai alitaka chama kifanyeje? Hata mahakamani mtuhumiwa akikataa kujitetea bila sababu za msingi, mahakama hulazimika kuamua kwa kusikikiza upande mmoja.

Nne; Maamuzi ya Chadema hayakufanywa na Mbowe. Yalifanywa na Kamati kuu ambayo ina wajumbe zaidi ya 40. Ni ujinga kuamini wajumbe wote hawakua na sauti isipokua Mbowe peke yake. Ndugai elewa kwamba Mbowe sio kamati kuu ya Chadema.

Tano; kumbe Ndugai anajua Mzee Halima na mwenzake walipigwa hadi wakazimia pamoja na kuvunjwa mikono na askari magereza? Unyama huu aliwahi kuulaani popote? Aliwahi kumuita Kamishna Mkuu wa Magereza kwenye kamati za bunge ajieleze kwanini Askari wake walifanya unyama ule tena kwa wabunge wanawake? Au aliona ni sawa tu kwa sababu walikua Chadema. Leo wamefurushwa ndio anasikia uchungu.

Huu utaratibu wa mtu kuonewa lakini unakaa kimya kwa sababu sio wa chama chako sio ubinadamu kabisa. Ningemuona Ndugai ana hoja kama angekemea tukio lilipotokea. Sasa Mzee Halima ameshapona na kusahau ndio Ndugai anasikia uchungu leo? Haina tofauti na mkeo kulia kwa uchungu na kukuomba msamaha kwa sababu ya vita vya majimaji eti babu yake alishirikiana na wakoloni kuwapiga wazawa. Wendawazimu.!
Kwa akili yangu,kumlinda mzee halima na wenzake maana yake ni kuiambia dunia kwamba serikali hii haifuati sheria,kwa hiyo wewe kama unataka kwenda kuwekeza Tanzania,just go at your own risk
 
Jamani pigeni kazi huku mkitanguliza Uzalendo mbele Over...! Sijuhi Ndugai kakosea hizo story acha haraka sana.
 
CCM walimwita Bibi Kidude, tasa na msagaji kwa maana ya shoga. Hapo una twambiaje mkuu?
Malisa too low for you kumuita Halima Mdee..Mzee Mdee..

Wewe Malisa kuna wengi tunakuheshimu

Unaweza kuandika hoja bila kuingia kwenye matusi ya mitandaoni...

Halima hata kama sasa kawa adui
Ana mchango wake na heshima yake..kama mwanamke na kama binadamu kwanza..

Msisahau mlivyomtukana Zitto kipindi kile
Leo ni mshirika wa upinzani hadi Tundu Lissu kaenda kumpigia kampeni jimboni kwake..

Kuna maisha baada ya siasa
 
Hivi sijui.kwanini CCM mara zote huwa hawajibu hoja badala yake humshambulia mtu na kuacha hoja za msingi. Sasa ukisikiliza majibu ya Ndugai utaamini kuwa ni mtu mwenye sifa ya kuwa spika wa bunge? Mbona ni kama mjinga fulani asiyekuwa na elimu yoyote kichwani?
Hivi mmesahau kuwa Ndugai mwaka 2015 aliwahi kumtwanga kwa fimbi kichwani Mshindi halali kwenye kura ya maoni??
Toka siku nyingi hakuwa na sifa ya kuwa Spika.
 
Mimi hizo sababu zako zote natofautiana ila la msingi ni kwamba ndugai atajidhalilisha kama ataruhusu wabunge wasiokua na chama bungeni.

Wanachohitajika kufanya CHADEMA ni kulifahamisha bunge rasmi kuhusu kuwatimua chama hao wabunge wao.

Tena CHADEMA waweke wazi kwa wananchi kuhusu hatua hiyo kisha tuone kama ndugai hatawatimua kina halima bungeni.

Isije kua janja na hila za mbowe na mnyima kuvunga na kufanya propagandakwa kumbe taarifa rasmi kwa ndugai hawajatoa wala hawatatoa.
Watamfahamishaje kama nani?! wakati hawamtambui spika wala uwepo wa bunge lenyewe
 
Katiba inasema chama chochote kikifikisha asilimia 10+ ya kura kwenye uchaguzi mkuu lazima kiteue wabunge wa viti maalum.
Katiba haisemi kwamba uchaguzi mpaka ukiwa huru na haki ndiyo uteue

Kwa maana hiyo kukataa kuteua wabunge wa viti maalum kwa kisingizio cha uchaguzi haukuwa huru ni kuvunja katiba ya nchi.
 
If nyerere were alive.....

Naomba mabingwa wa English mmalizie hii sentence kwa kutumia condition type three kwa kuoanisha na hali ya kisiasa ya nchi yetu.
 
Ni kweli bro msaada unahitajika lakini kwa taarifa za wataalam wa matibabu ya lile gonjwa sugu ni kwamba ikifikia "stage" ARV zikishazidiwa nguvu (stage ya moto inaitwa) mgonjwa anaanza kubwabwaja kila kimjiacho kinywani na mara nyingi anakuwa ni mtu wa hasira kali an visilani...tumsamehe tu kwani tayari watanzania wengi tunajitambua na kikubwa zaidi tunaelewa ila za watawala wa sasa
Hapo kwenye "tumsamehe" ina maana asamehewe kwa kuharibu au asamehewe kwa lipi!!!
 
Kuwaambia waandishi wa habari wasiende kuwahoji wastasfu akina Msekwa kwamba hawajui mambo yalivyobadilika imenitia shaka kidogo!
Ndiyo ujue sasa kuwa mambo yameharibika na usiweshabiki mandazi pasipo kujiuliza au kujua unashabikia nini. Huwa na soma mandiko yako sana nakosaga hata cha kukoment. To be honest tusipokuwa makini na kuungana kulinda heshima ya nnchi yetu tutakuwa kituko juuu ya vituko vya watawalaaa.
 
Katiba inasema chama chochote kikifikisha asilimia 10+ ya kura kwenye uchaguzi mkuu lazima kiteue wabunge wa viti maalum.
Katiba haisemi kwamba uchaguzi mpaka ukiwa huru na haki ndiyo uteue

Kwa maana hiyo kukataa kuteua wabunge wa viti maalum kwa kisingizio cha uchaguzi haukuwa huru ni kuvunja katiba ya nchi.
Katiba inasema uchaguzi mkuu ni nini?
 
Nikionacho ni kjwa viongozi kadhaa wa nchi hii walikuwa hawajamaliza masomo!
 
Back
Top Bottom