Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Kuwa muelewa,nilitaka kumfafanulia huyu dogo kuwa distance sio sababu kutojenga uwanja wa ndege.

Kumfurahisha ili iweje? Kwani ataishi milele?
 
Mbona mkoa mmoja wa kaskazini ulipewa barabara za ramani, maji,na hata wazawa wa mkoa huo walisambazwa mikoa yote na kukiuka idadi ya quota system?
Acha unafiki,Tanu aka CCM ndio iliruhusu watu wa mkoa huo kuja Dar bila kibali,kwani Mwingereza aliwapiga marufuku.
 
Wamepita marais wangapi kwanini hawakukumbuka kwao?wali delay au walikuwa wabinafsi
Mtu kwao bwana ......kwa mwafrika

Ova
Wangekuwa wabinafsi wangejenga kwao!Sasa siasa za nchi hii zinachukua sura mpya,tutaanza kuchaguana kikabila ili tu maendeleo yawahi maeneo ya ukanda wa kabila la Rais!Huku ndiko mnataka tufike?
 

..miradi ya maendeleo isambazwe ktk mikoa yote ya kanda ya ziwa siyo kupendelea kijiji na jimbo la bwana mkubwa.
 
Rais Mstaafu Kikwete bado yuko hai na ni miaka 5 na miezi 3 tu iliyopita alikuwa madarakani, lakini sina kumbukumbu, na nakiri sikubuki ni lini Dhifa ya Kitaifa ilifanyika Msoga.
 
Kwamba hakuna hata kimoja chenye ukweli kati ya aliyosema.
1.Hakuna uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini Chato.
2.Hakuna Hospitali ya rufaa Chato kijijini

Utetezi ni kwamba vyote hivyo vimejengwa nchini, sijajua kama Mobutu alijenga Morocco, au Zuma alijenga India.
 
..miradi ya maendeleo isambazwe ktk mikoa mingine ya kanda ya ziwa.

..siyo haki kulundika miradi mingi kiasi hicho kijijini na jimboni kwa bwana mkubwa.
Miradi mingi kama ipi imerundikwa Chato?

Mikoa mingine kanda ya ziwa haipelekewi miradi ya maendeleo? Unaifahamu Mara vizuri kabla ya 2015?
 

Kuna dalili zote kuwa hujamwelewa Tundu Lissu...

In fact , unajibu hoja za TL kwa hasira za "tofauti za kiitikadi za kisiasa" tu na si kwa sbb ya hicho unachosema "upotoshaji"...

Unasema Magufuli asilinganishwe na kina Mobutu Seseseko, Dr. Hastings Kamzu Banda, Felix H. Bouigny na wengineo...

Na unasema kuwa lengo la kitabu la Peter Kenyon, "Dictatorland: Men Who Stole Africa" hakizungumzii viongozi wa aina ya Magufuli ambao lengo lake ni kuwaletea maendeleo watu nadhani kwa wewe kufikiri hawa wanaotajwa kwenye kitabu hicho hawakuwa na lengo hili: kuwaletea wananchi wao maendeleo..

Unaendelea kutetea hoja yako kwa kusema, kuwa, kitabu hicho kinazungumzia viongozi walioiba na kujitajirisha kupitia rasrimali za nchi zao na John Pombe Magufuli hawezi kuingia kwenye kundi la viongozi hao kwa vigezo na sababu anazozitaja Tundu Lissu na kinachofanyika Chato kijijini kwa Rais Magufuli...

Kwanza pole sana kwa sababu unadhani viongozi madikteta wezi huufanya wizi wao kama wezi au vibaka wa kawaida wanaovamia na kuvunja benki na kisha kukwapua mabegi ya pesa...

Laiti ungejitendea haki kwa kusoma kwa umakini uchambuzi wa Tundu Lissu na kisha uka - acknowledge tu na ukatulia, ungekuwa na busara sana....

Lakini Bahati mbaya kivuli cha itikadi za kisiasa zimekufunika na unaonekana u - kipofu wa fikra na kwa hiyo huwezi kuona chochote kizuri toka kwa watu wengine mnaotofautiana nao kiitikadi hususani mtu kama Tundu Lissu...

Nikuulize swali hili moja: Hivi wewe unadhani Rais Magufuli ni mtu mzuri na mtakatifu sana eti eeh...?

Pole sana. Sijui utajibu nini. Lakini najua ni vilevile tu. Nami nakuambia, UNAJIDANGANYA wewe na nafsi yako. Ninachoweza kukushauri, endelea kumwombea kama kiongozi wako ili arudi njia kuu, atoke kwenye upotofu, ukaidi na aache roho ya tamaa na uuaji...!

Ukifanya hivi, utakuwa unamsaidia sana...

Rais Magufuli hana tofauti na hao kina Felix F. B, Dr Hastings Kamzu Banda, Mobotu na wengine wanaosemwa na Peter Kenyon ktk kitabu chake...

Kwa kuwa Magufuli humuoni kusafiri nje ya nje unadhani siyo mwizi, ni mtu mwema sana na anawajali wananchi wake...

Deogratius Mutungi, dictator huwa haibi kwa njia hiyo unayodhani wewe...

Viongozi madikteta huiba kwa kutumia mifumo dhaifu ya kiutawala ya kiserikali na kinchi ambapo ktk uchambuzi wake Tundu Lissu amefafanua na kueleza kwa uzuri na urahisi sana kwa mtu yeyote mwenye akili na ufahamu mzuri kuelewa...

Dalili zote za dikteta mwizi ni haya anayoyafanya Rais Magufuli kwa kutupa kwenye dustbin vipaumbele vya kitaifa na kufanya maamuzi yake binafsi na kuyasimama kama vipaumbele vya taifa...

Viingozi wezi na madikteta hawajali sheria wala katiba. Kauli zao na maamuzi yao binafsi ndiyo sheria. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni hili...??

Viongozi madikteta mfano wa Magufuli, huendesha vikundi vya maauji, utekaji, na torture ya wapinzani wao kwa siri kubwa. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni na kuamini...??

Viongozi madikteta wa aina ya Magufuli wana hasira, hujipenda wenyewe, hawapendi watu wengine, ni wabinafsi na ma - ant-democracy. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni hili wewe...??

Hawa kina Mobutu, Houpgheiny - Bouigny, Kamzubanda na wengine ndivyo exactly walivyofanya...

Ngoja siku watu waje kuja na orodha ya mali na account za benki za kwake, rafiki zake, na ndugu zake zenye mafedha huko ndiyo utakuja kushangaa na kuishia kujijutia kwa kusema..

".....ala kumbe nilikuwa natetea shetani badala ya malaika bila kujua..!!

Pole sana. By then it could already been too late...!!
 
Miradi mingi kama ipi imerundikwa Chato?

Mikoa mingine kanda ya ziwa haipelekewi miradi ya maendeleo? Unaifahamu Mara vizuri kabla ya 2015?

..International Airport.

..Hospitali ya Rufaa.

..Ofisi za Mahakama.

..Uwanja wa mpira wa kimataifa.

..Ofisi za Tra.

..Ofisi za Msd.

..Chuo cha Veta.

..Benki ya Crdb.

..siyo haki kujenga miradi yote hiyo ktk jimbo moja wakati majimbo mengine ktk kanda ya ziwa nayo yana uhitaji.

..hakuna jimbo lolote lile ktk kanda ya ziwa ambalo limepewa miradi mingi ya maendeleo kama ilivyofanyika Chato.
 
... jibu hoja acha vioja.
 
... kwa hiyo ni nguvu za wananchi wa Chato zinatekeleza miradi yote ile tena ndani ya muda mfupi baada ya "hamasa kubwa"?
Ni nguvu ya wananchi kwa kutumia kanuni za nchi kufika hapo walipo. Wanachato wamejipanga kimaendeleo kwa kutumia sheria zilizopitishwa na bunge. Hakuna upendeleo hapo.

Je hujawahi ona majimbo mawili ya uchaguzi, yanayofanana kijiografia yanaweza kutofautiana kimaendeleo kutokana na aina ya usimamizi wa mbunge waliomchagua?
 
Watanzania hatupenda Sana kujua jambo na sababu zake. Mbali na ukweli kwamba Chato ipo Tanzania, zipo zababu muhimu Sana za maslahi ya kitaifa juu ya kinachoendelea Chato. Kwa bahati nzuri Leo asubuhi tulijadili hili hapa hapa JF.

 
Wangekuwa wabinafsi wangejenga kwao!Sasa siasa za nchi hii zinachukua sura mpya,tutaanza kuchaguana kikabila ili tu maendeleo yawahi maeneo ya ukanda wa kabila la Rais!Huku ndiko mnataka tufike?
Yule aliyetoka kusini kwao watu walimsema
Oh mbona kuko ovyo
Tatizo sisi wanadamu hatueleweki kabisa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…