3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 5,350
- 15,426
Unasikilizia wapi mkuu??Tamasha la utalii pana upigaji wa takribani 1.5 B maana tamasha hili halikuwemo ktk bajeti za wizara ila iliamuliwa kila mamlaka chini ya wizara kutoa 250m kufanikisha ila fedha hizi CAG hakupata vielelezo, ambapo Clouds walilipwa 600+m na TBC 250+m lakini malipo haya hayakuwa na uthibitisho maana risiti za kielektroniki hazikutolewa
Tuanze na uyu mleta taarifa.Uwajibikaji na uwajibishwaji uanzie hapo
Nimepitia kwa millard ayo mkuuUnasikilizia wapi mkuu??
Tuanze na uyu mleta taarifa.
... unapenda kweli kuwahi kuleta habari but with no details or very shallow. Usiwe unakimbilia ku-post; unaziba nafasi ya mwenye nia ya kutuletea habari kwa ukamilifu! Hata hizo UPDATES zako zitakuwa very shallow I guess!
Hivi anayoyasema huyu CAG yalifanyika chini ya uongozi gani jamani π’π’π’π’?
Huu upigaji unaosemwa na CAG tena katika awamu iliyojinasibu kupambana na ubadhirifu unaweza kuhitimisha kwa maneno machache kuwa Pamoja na simba kuwa mkali lakini anazaa
Sijui yule rais wa wanyonge alikuwa anafanya nini na mtandao wake wa wasukuma nchi nzima.CAG Kicheere anaongea na waandishi wa habari muda huu.
Updates;
========
CAG: NILIBAINI WAKALA NNE ZA SERIKALI ZILIKUWA ZINADAIWA BILIONI 783.39
TANROADS ilikuwa na deni kubwa lenye thamani ya bilioni 770.1 kutoka kwa wakandarasi na wahandisi washauri kutokana na kuchelewa kupata fedha za kutekeleza miradi kutoka hazina, wakala wa majengo bilioni 1, RUWASA bilioni 12 na TARURA milioni 125
-Ni madeni ya wakandarasi, watoa huduma na washauri katika hizo taasisi nne
CAG: MIRADI INAYOTEKELEZWA INA TOZO YA RIBA YA BILIONI 14.9
Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(CAG) amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ina riba ya bilioni 14.9 kama adhabu ya kuchelewesha kulipa hati za madai ya wakandarasi kinyume na masharti ya mikataba
-CAG amesema malipo hayo hayana tija kwani yangeweza kuepukika kwani baadhi ya pesa ni za wafadhili ambazo zipo lakini mlolongo mrefu wa malipo kwa serikali unakwamisha
MALIASILI NA UTALII
CAG: Nilifanya ukaguzi maalum wizara ya maliasili na utalii, nilibaini bilioni 6.8 zililipwa kutoka kwenye mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii bila idhini ya afisa masuuli kinyume na kanuni ya fedha. Pamoja na haya nilibaini matumizi ya jumla ya bilioni 16 yalifanyika bila kuwa na hati za malipo pia yalibainika matumizi ya bilioni 11 ambayo hayakuwa na nyaraka toshelezi na milioni 89 zilizotumiwa na makumbusho ya Taifa kwa matumizi yasiyoendana na shughuli za utalii.
Kwa maoni yangu mkurugenzi wa utalii na mhasibu waliokuwa wanahusika walitumia vibaya fedha za tozo ya utalii jumla ya Tshs Bilioni 34
Na wapo wakupata Z sio F ........ Afanaleki nipo kwenye taharuki kubwa yaani 18Bn zinakusanywa then hazipelekwi benki doooh!Kazi ya CAG ni kusema
Wanaopokea report zao ni kama vile wanafunzi wanavyopokea majibu ya mtihani wao wa mwisho wa mwaka. Wapo wa kupata A, B, C, D......
Tatizo ni kwamba either alikatazwa au alisahau kusema, na aliyejaribu kusema alijikuta hana huo U-CAGKazi ya CAG ni kusema
Wanaopokea report zao ni kama vile wanafunzi wanavyopokea majibu ya mtihani wao wa mwisho wa mwaka. Wapo wa kupata A, B, C, D......