Kama yalikuwa makosa,uwanja ushajengwa japo haujakamilika kabisa.kuuacha hivi itakuwa tumezalisha hasara.Tunaweza kujaribu baadhi ya mambo kupunguza hasara:
1.Labda tuukodishe kama tumeshindwa kuutumia,ili kurudisha fedha za umma.
2.Tuchonge mdomo kwa nchi za jirani za Afrika Mashariki ,kuwashawishi utumike kama Rapid deployment base ya ndege na helicopter kwenye nchi zenye majanga kama vita,njaa,wakimbizi,ajali za majini,magonjwa mabaya ya kuabukizwa kama ebola n.k
3.Uwe Air base ya Kijeshi.
4.Chato iwekwe chuo cha kujifunza urubani wa ndege za kiraia na za kijeshi.
5.Uwanja ugeuzwe hub ya ndege za kubeba mizigo kama maparachichi,Minofu ya samaki,maua,mboga mboga,ndizi,n.k.
Labda miaka 30 ijayo wakati Chato itakapo fikia kiwango kikubwa cha maendeleo ,uwanja unaweza kutumika pia kwa ndege za abiria n.k