Carol Ndosi: Rais Samia aache kusisitiza kila mara kuwa yeye ni Rais mwanamke, haipendezi

Carol Ndosi: Rais Samia aache kusisitiza kila mara kuwa yeye ni Rais mwanamke, haipendezi

Mwana harakati na Mjasiriamali carol Ndosi kupitia kipindi cha Joto Kali la Asubuhi TV-E ameweka wazi kukerwa kwake na kitendo cha Rais Samia kila anapopata nafasi kuongea na Watanzania basi lazima aseme kuwa yeye ni Rais mwanamke na yeye ni mwanamke. Amesema kuwa amekuwa akirudia mara kwa mara kila apatapo nafasi kuwa yeye ni mwanamke wakati kila mtanzania anajua kuwa yeye ni mwanamke.

Carol Ndosi anasema kuwa Rais Samia yeye ni Rais hapaswi kuendelea kujificha nyuma ya kimvuli cha uanamke kwani hilo si jambo zuri na haipendezi kwa Rais kuwa na hofu ya uanamke wake bali anatakiwa ajue watu wanamuamini kama Rais si kama mwanamke.

Amesema pengine Rais Samia anapitia mambo mengi kwenye chama chake au kwa watu wanaomzunguka kwa sababu ya uanamke wake lakini yeye kama Rais atakiwi kuitumia kama ngao kwani yeye ni Rais na watu wanajua ni mwanamke atakiwi kuwakumbusha watu, haipendezi.

Chanzo: TV-E/E-FM
Hiyo inaonyesha sio rahidi mwanamke kua rais. Anasema anafuata umagufuli lakini tayari fisadi wanamyumbisha kutaka kumtoa kwenye reli waiongoze nchi. Tumuheshimu kwa sababu ni matwaka ya katiba.
Na wale wenye kusema ccm haiheshimu katiba wakome. Inshalah 2025 mama atatuongoza kupata magufuli mpya.
 
Carol huwa ana kiherehere flani hivi Rais naye ana utashi kuongea hisia zake sio dhambi as long as havunji sheria anapoongea, waache kumu undermine Rais ingekuwa magufuli asinge dhubutu kusema hvo
 
Am i the only one feeling this is a lil harsh..

Sijui yani..

Mbona kama anamfokea Mama yetu?.
Hizi kauli za mara kwa mara za Mheshimiwa Raisi kuhusu Uraisi wake, na jinsia zinaashiria uwezekano mmoja. Inaelekea kulikuwepo ubishi ndani ya CCM na kutoamini kuwa Meshimiwa Samia angeweza kuwa Raisi. Hilo jambo inaonekana lilimkwaza sana Raisi na pengine limebaki kama kovu kwenye moyo wake ndiyo maana huzungumza mara kwa mara
 
Huyu mwanaharakati uchwara yani badala ya kukosa teuzi anahangaika tu, apambane na hali yake tu hakuna namna walimshauri anyoe rasta na aache bangi hakusikia
 
Hata yeye hajui kitu,mwanamke hakuumbwa aongoze watu hata angekuwa yeye huyo Ndosi lazima angekuwa na wenge.miezi saba sasa inakatika still anathibitisha jinsia yake kwa wananchi kwani wao hao wananchi hawamjui mwanamke kwa kumtizama?avue nguo basi ili tufunge hesabu!!!

Hakuna mwanamke anayeweza kufanya kitu kwa 100% akaweza bila kumshirikisha mtu hii yote inatokana na uwezo wao mdogo wa kuhakiki mambo that's why anajificha nyuma ya pazia la jinsia yake.
Kwahyo Hadi aliyekuzaa ana akili ndogo?
Why undermining women kwa wrong perction ulizoaminishwa za enzi za kijima, I'm sure wewe kama mwanaume zaidi ya kumiliki suruali na dudu la yuyu hujawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi na huna Cha maana ulichofanyia taifa lako zaidi tu ya kutoa wrong assumptions za ku undermine wanawake
 
Am i the only one feeling this is a lil harsh..

Sijui yani..

Mbona kama anamfokea Mama yetu?.
Carol yuko a bit harsh mwanzo alikuwa anamusifia Sasa alipoacgwa UDC ikawa shida, kuwa Rais wa nchi hakukuondolei ku show what you feel hasa anavoshambuliwa vile ni mwanamke
 
Naona unalia lia tu, wacha watu watoe maoni yao usiwatungie uongo ili kujiliwaza na umpendaye.
Mbona na Samia akitoa opinions zake za moyoni mnamshambulia na kumkosoa?
Kikubwa tuheshimu opinions za wenzetu hata kama hazitufuraishi that's maturity
 
Ndiyo Kisha sema sasa yeye ni Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kwani uwongo? Naye Carol Ndossi ni mwanamke wa kwanza mchoma nyama.

Hivi Carol Ndossi angepata ule u DC aliokuwa anautegemea sana, leo angeweza kwenda redioni na kuongea aliyoongea?
Kila mmoja ashinde mechi zake, usimpangie
Caro angepata UDC asingesema hivo
 
Carol huwa ana kiherehere flani hivi Rais naye ana utashi kuongea hisia zake sio dhambi as long as havunji sheria anapoongea, waache kumu undermine Rais ingekuwa magufuli asinge dhubutu kusema hvo
Kwanza huyu Carol anamume kweli?
 
Huyu mwanaharakati uchwara yani badala ya kukosa teuzi anahangaika tu, apambane na hali yake tu hakuna namna walimshauri anyoe rasta na aache bangi hakusikia
Dah kumbe anavuta ganja aisee?
 
Tunao msapoti Samia tunajua kuna makosa atafanya ni ruksa kukosolewa..
Nyinyi mnae abudu Marehemu ndo kazi kwenu ..
Marehemu keshakufa hata mkimpamba ndo keshakufa
ah ah le big boss LE MBEBEZ LE MUTUZ
 
Ni kituko anayekosolewa kupanga akasolewe vipi, ni ujuha.
Inaweza kuwa ni kweli , huwezi kujipangia, ila vipi weee ulishaacha kupakuliwa kule na kuaach utaa hila ?
 
Tunao msapoti Samia tunajua kuna makosa atafanya ni ruksa kukosolewa..
Nyinyi mnae abudu Marehemu ndo kazi kwenu ..
Marehemu keshakufa hata mkimpamba ndo keshakufa

mama anaupiga mwingi kamanda[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Carol huwa ana kiherehere flani hivi Rais naye ana utashi kuongea hisia zake sio dhambi as long as havunji sheria anapoongea, waache kumu undermine Rais ingekuwa magufuli asinge dhubutu kusema hvo
Carol Ndosi ni opportunist mkubwa, alijaribu kumfikia Samia kupitia Nyama choma, ikabumba. Lengo ilikuwa kutafuta uteuzi.

Sasa naye amejiongeza kwenye kundi la wanaharakati na wapinzani wanomkosoa Rais kama Maria Sarungi, Fatma Karume, God bless Lema na Tundu Lissu.

Samia piga kazi tu usiwasikie hawa PIMBI
 
Nadhani wengi wametafsiri negatively Bi mkubwa anapokumbushia kwamba yeye ni raisi mwanamke. Kubwa ni kutukumbusha kwamba hatuwezi kuruka asili kati ya mwanaume na mwanamke.

Ninapata faraja kuona baadhi ya makada wa ccm wanaanza kujibu hoja kwa ustaarabu. Mfano Nape Nnauye jana alijiunga Maria spaces na akashusha somo moja kuhusu uchaguzi na akaeleweka bila chadema kuwa na mihemko. Lazima turuhusu dialogue ili tusonge mbele mfano Criminal justice ina shida kubwa na inahitaji kubomolewa kabisa na kujengwa upya. Yaani nchi mtuhumiwa na mfungwa hawana haki kabisa.
 
Back
Top Bottom