Case Study: Ni nadra sana kukuta kijana wa kiislam hajaoa lakini inazidi kuwa kawaida kumkuta kijana wa kikristo anakwepa ndoa, Nini chanzo ?

Hii mada ina content mzuri lakini watu wanacomment kiudini sana bila kuzingatia ujumbe uliopo ndani yake.
What if tukiainisha sababu za msingi kama gharama na talaka ambazo huchangia vijana wa kiislamu kuoa mapema kuliko wenzao wa kikristo.

Je, vijana wa kikristo wanapenda kukaa na wenza wao bila kuoana hadi kufikia hatua ya kupata watoto? Na kama hawapendi kwa nini kusiwe na sababu ya kuangalia na kurekebisha (ikibidi) kanuni za kikristo zinazohusu ndoa na talaka ili kuleta urahisi katika maswala haya ya kijamii kuliko kusema uislamu unakariri wamekariri kuoa au Christians are westernized? Ikukumbukwe siyo kila umagharibi ni maendeleo.

Nadhani ni bora kuwa objective na kuangalia kwa nini kuna utofauti huo na je kuna haja ya kuondosha gap baina ya vijana wa dini hizi mbili?
Babu yangu aliwahi kunambia "Penda unapotakiwa kupenda na uchukie inapotakiwa kufanya hivyo"
 
Na hapa nazungumzia hasa vijana wa chini ya miaka 30 ambao ni umri uliozoeleka kwa kijana kuoa na kupata mtoto ndani ya ndoa.

Nikiangalia niliohitimu nao chuo degree, rika letu kwa sasa ni miaka 32 hadi 33, vijana wote wa kiislam walishaoa mapema kabla hawajavuka miaka 28, huku kwa wakristo hadi sasa ni asilimia 50 tu waliooa, wasio na ndoa wapo wenye watoto huku kwenye suala la mahusiano kubadili wanawake kwao ni kula ujana.

Shirika nililoajiriwa huwa kuna muda nasupervise matawi tofauti tofauti hata ya mikoa ya karibu, imekuwa ni kawaida sana kukuta vijana wa kiislam kuwakuta tayari wameshaoa lakini kwa upande wa vijana wa kikristo utawakuta waliooa ni watano kato ya kumi.
Uzuri wenzetu waislam, kijana akifeli, mzazi anatoa huduma zote, ikiwa ni pamoja na nanhiii. [emoji1787][emoji1787]

Kijana wa kikristo akishaoa, ajibebe kwa kila kitu.
 
Ila kuachwa ni kuachwa tu,iwe rahisi au kigumu,upendo ukishapotea hakuna mapenzi tena,hata musumbuane miaka kumi,
Tatizo watu ving"ang'anizi sijui tukoje. Unakuta ndoa ilishakufa miaka mingi, huko ndani ni kama maadui lkn wanalazimisha kuendelea kuishi pamoja kwa kuogopa maneno ya watu. Haileti afya hata kidogo
 
Wanaogopa! Maandiko ya kifo kiwatenganishe! Huku ndani unateseka huna raha wala amani!
 
Wewe inaoneka umesoma ila bado unaujinga % ya wasomi kati ya wagalatia na waislamu almost on the same par, isipo kua wengi wsoslamu wanajiajiri kazi nyingi makaafiri wana bagua waislamu, ndo maana uaoni sanaa huko.
keep cool, tulia, poza hasira halafu uandike. Unaweza kuwa na hoja lkn umeandika kwa hasira na makosa mengi kwenye sentensi zako. Face reality and be ready to defend it with reason from higher mental faculty reasoning
Kwani wakiristo wa pwani wanatofauti gani na waislamu wa pwani mbona wote ni wale wale, kama ni elimu wote wanafanana.
Muislamu Mzaramo, mndengereko etc wana tofauti na muislamu wa Kagera katika life style inayoongozwa na dini. Kagera madrasa si hivyo sana na kipaumbele ni formal shooling. Pwani is the opposite of that
 
Nikiangalia niliohitimu nao chuo degree, rika letu kwa sasa ni miaka 32 hadi 33, vijana wote wa kiislam walishaoa mapema kabla hawajavuka miaka 28, huku kwa wakristo hadi sasa ni asilimia 50 tu waliooa, wasio na ndoa wapo wenye watoto huku kwenye suala la mahusiano kubadili wanawake kwao ni kula ujana.
Gharama Mzee Baba, waislamu hata 10,000/- hadi 100,000/- km mahari wanapokea unafungishwa ndoa kiroho safi kabisa, wakristu Ndoa ni gharama kishenzi ukitaka kuoa andaa kitita Cha kutosha kuanzia 1.5M / 2M na kuendelea
 
keep cool, tulia, poza hasira halafu uandike. Unaweza kuwa na hoja lkn umeandika kwa hasira na makosa mengi kwenye sentensi zako. Face reality and be ready to defend it with reason from higher mental faculty reasoning

Muislamu Mzaramo, mndengereko etc wana tofauti na muislamu wa Kagera katika life style inayoongozwa na dini. Kagera madrasa si hivyo sana na kipaumbele ni formal shooling. Pwani is the opposite of that
Mimi nacho jua waislamu wana fanana kwote kwote, madrasa ni lazima kabla ya kuanza shule za circular, labda ada ndo ikosekane tu
 
Watu mnaoa na kuachana kama jogoo anavyoyapanda majike unalinganisha na sisi. Nenda hapo kaa wazigua waislam, utadhani hawatumii ubongo, ni kuoa na kuacha kila siku. Hovyo kabisa.!!
 
Mimi nacho jua waislamu wana fanana kwote kwote, madrasa ni lazima kabla ya kuanza shule za circular, labda ada ndo ikosekane tu
Thamani ya formal class differs a lot from one place to another . Naona hapa ninapokaa mzazi doesn't care mtoto kwenda shule, but afanye mchezo kwenye madrasa atapata cha moto! Bukoba for example is quite different..... nimeona waislamu wanasema dini atasoma akipenda mwenyewe huko mbele..... si huku pwani, never.. hata pwani wasomi wanalitambua hilo...dada mmoja rafiki yetu anasema mwanangu huko haendi, kuna fimbo usiombe akakataa
 
Na hapa nazungumzia hasa vijana wa chini ya miaka 30 ambao ni umri uliozoeleka kwa kijana kuoa na kupata mtoto ndani ya ndoa.

Nikiangalia niliohitimu nao chuo degree, rika letu kwa sasa ni miaka 32 hadi 33, vijana wote wa kiislam walishaoa mapema kabla hawajavuka miaka 28, huku kwa wakristo hadi sasa ni asilimia 50 tu waliooa, wasio na ndoa wapo wenye watoto huku kwenye suala la mahusiano kubadili wanawake kwao ni kula ujana.

Shirika nililoajiriwa huwa kuna muda nasupervise matawi tofauti tofauti hata ya mikoa ya karibu, imekuwa ni kawaida sana kukuta vijana wa kiislam kuwakuta tayari wameshaoa lakini kwa upande wa vijana wa kikristo utawakuta waliooa ni watano kato ya kumi.
Simple tu hiyo,
Ni kwasababu ya urahisi wa kuoa na kuacha.Waislamu ndoa zenu simple sana hazina mambo mengi na kuachana na hivyo hivyo.

Nimeishi na kufanya kazi Mtwara aisee mdada anaolewa leo baada ya wiki mbili kaachika.Mtwara 98% ya watu ni waislamu.
 
Back
Top Bottom