Cassie amfungulia mashtaka Diddy yakiwemo madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia

Cassie amfungulia mashtaka Diddy yakiwemo madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia

MAREKANI: Msanii wa Muziki wa Rap, Sean "Diddy" Combs na Msanii wa R&B, Casandra "Cassie" Ventura wamemalizana Kisheria siku moja baada ya Cassie kumshtaki Diddy kwa tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa Kingono

Taarifa ya pamoja ya Wawili hao imesema walifikia makubaliano ya kusuluhisha suala hilo kwa amani siku ya Ijumaa, Novemba 17, 2023 bila kufichua maelezo zaidi

Kesi iliyofunguliwa Novemba 16, 2023, Cassie alidai Diddy alimpiga, kumbaka, kumuingiza katika Matumizi ya Vileo na Dawa Za Kulevya na kumhusisha na biashara ya ngono kwa zaidi ya Miaka 10 walipokuwa katika uhusiano wa kimapenzi

View attachment 2817462

Sent from my Pixel 3 XL using JamiiForums mobile app
Demu alikuwa na hamu tu ya kumchokoza mwamba
 
Tangu 2005 ndio anakuja kushtaki Leo alikua wapi🤔🤔 tapeli huyu lakini kwa vile wanawake ndio wenye haki huko uzunguni mwanetu kayakanyaga
 
Washamalizana tayari nadhan didy kamlipa cassie pesa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hapo didy kajichanganya kwa hiyo tusubiri episode nyingine. Maana makaburi ya baby momma wake Kim poter yashaanza kufukuliwa na mtu kafariki kitambo

Ila cassie kala kibunda 😁😁, 30m na wakati utajiri wake wote haufiki 10m.
 
View attachment 2816118

Cassie amefungua kesi ya dola milioni 30 dhidi ya Diddy akimtuhumu kwa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. Mwanadada huyo anasema muda mfupi baada ya kukutana na Diddy mwaka 2005, akiwa na umri wa miaka 19, alianza tabia ya kumdhibiti na kumnyanyasa ikiwa ni pamoja na kumlazimisha kutumia dawa za kulevya, kumpiga na kumlazimisha kulala na malaya wa kiume huku akirekodi filamu hizo.

Kesi hiyo imeibua hisia za watu wengi mtandaoni wakidai kuwa inaweza kuibua watu wengi waliofanyiwa vitendo kama hivyo na Diddy na kudai kuwa inaweza kuwa ndio mwisho wa Diddy.

cassie n shost yake Rita Zainabu [mention]Ritz [/mention]
 
Hapo didy kajichanganya kwa hiyo tusubiri episode nyingine. Maana makaburi ya baby momma wake Kim poter yashaanza kufukuliwa na mtu kafariki kitambo

Ila cassie kala kibunda 😁😁, 30m na wakati utajiri wake wote haufiki 10m.
Yameanza fukuliwa kim porter alikuwa anataka kuachia kitabu chake kuhusu maisha yake akafa ghafla na kifo hakieleweki
Wale aloanzisha nao lebo yake nao wamekufa wakitaka kuachia vitabu inaonekana kuna mengi ,mdogo wake kim p anasema didy alimbikiri Justin bieber ila kama kuna yana ukweli apate yanayomstahili tu siku hizi malipo hapa hapa dunian
 
Diddy anafahamika kwa roho mbaya.
Natumai siku taja ambapo atapatilizwa kwa yote aliyoyafanya..
No wonder Makaveli alikuwa hawapendi hawa wakora wa bad boy!
 
Yameanza fukuliwa kim porter alikuwa anataka kuachia kitabu chake kuhusu maisha yake akafa ghafla na kifo hakieleweki
Wale aloanzisha nao lebo yake nao wamekufa wakitaka kuachia vitabu inaonekana kuna mengi ,mdogo wake kim p anasema didy alimbikiri Justin bieber ila kama kuna yana ukweli apate yanayomstahili tu siku hizi malipo hapa hapa dunian
Duhhh ishakuwa story kubwa sasa. Ngoja niingie Twitter
 
Attachments

  • 4969C947-A85B-47B9-ABBE-155310B983B3.png
    4969C947-A85B-47B9-ABBE-155310B983B3.png
    653.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom