CCM mtandao watajuta milele kuruhusu Magufuli awe Rais wa Tanzania

Ni tabia yetu Watanzania kuiona jana ni afadhari kuliko leo!
Wakati wa Mzee Ruksa tuliona Nyerere alikuwa afadhari,wakati wa Mkapa tuliona Mwinyi alikuwa afadhari.
Sasa atakayekuja tutasema Mama alikuwa afadhari!
 
Maguf.uli alianzisha uhuni wa kuteka na kupoteza watu
Magufuli alinajisi tume huru ya uchaguzi na kuipendelea CCM kuanzia urais, ubunge, diwani hadi serikali za mitaa
Alitumia njia zingine vibaya, ila ukweli utabaki kuwa alifunua mambo mengi sana yaliyokuwa yamefichwa.
 
Bila Hayati Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wengi tungekuwa bado tunaamini Tanzania ni nchi masikini sana isiyoweza kujenga reli yake ya umeme, isiyoweza kukomesha tatizo la mgao wa umeme .

Bila Magufuli kuwa rais Mh Jakaya Kikwete angekuwa anaonekana mzee wa maana Sana ndani ya nchi na hata Samia angekuwa anaitwa mama wa huruma wa taifa.

Ujio wa Magufuli ndio ulioweka hadharani uwezo wa kuongoza na uzalendo wa akina Nape, January, Prof Muhongo, Zito Kabwe na wengine wengi kwamba hawana uzalendo wowote na nchi hii na wanachojali ni kupiga dili kwa masilahi yao binafsi.

Bila Magufuli kuwa Rais huenda ccm mtandao wangeendelea kunufaika na Freeman Mbowe kwa miaka mingi ijayo maana wengi waliaminishwa ni mpigania haki na mzalendo wa kwelikweli.

Kwa ufupi nyeti za ccm mtandao ziko hadharani na unasubiriwa muda kidogo tu wagawane mbao.
Usimsifu sana Magufuli, ndiye aliyeasisi utekaji na kuwamaliza watu kimya kimya.
Uzuri wa Mungu, mtu analipa hapahapa duniani.
 
Bila Hayati Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wengi tungekuwa bado tunaamini Tanzania ni nchi masikini sana isiyoweza kujenga reli yake ya umeme, isiyoweza kukomesha tatizo la mgao wa umeme .

Bila Magufuli kuwa rais Mh Jakaya Kikwete angekuwa anaonekana mzee wa maana Sana ndani ya nchi na hata Samia angekuwa anaitwa mama wa huruma wa taifa.

Ujio wa Magufuli ndio ulioweka hadharani uwezo wa kuongoza na uzalendo wa akina Nape, January, Prof Muhongo, Zito Kabwe na wengine wengi kwamba hawana uzalendo wowote na nchi hii na wanachojali ni kupiga dili kwa masilahi yao binafsi.

Bila Magufuli kuwa Rais huenda ccm mtandao wangeendelea kunufaika na Freeman Mbowe kwa miaka mingi ijayo maana wengi waliaminishwa ni mpigania haki na mzalendo wa kwelikweli.

Kwa ufupi nyeti za ccm mtandao ziko hadharani na unasubiriwa muda kidogo tu wagawane mbao.
Watagawanaje mbao ilihali Mwamba Burhani yupo mzigoni ??! 😁
 
Back
Top Bottom